Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,580
Waonya ushabiki wa kisiasa, wataka kikao cha haraka
na Lucy Ngowi
KUIBUKA kwa vurugu bungeni kwa nyakati tofauti Jumatano na Alhamisi ya wiki hii, na kusababisha wabunge watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutimuliwa ndani ya Bunge, kumeibua hoja nzito nje ya Bunge.
Wakati CHADEMA wao wakidai hali hiyo imetokana na uongozi mbaya ndani ya Bunge, Chama cha Mapinduzi (CCM) wamewatupia lawama wabunge wa chama hicho, kadhalika wasomi nao wakionya juu ya ushabiki wa kisiasa.
<b>Kauli ya wasomi</b>
Wasomi na wanaharakati mbalimbali nchini, wameutaka uongozi wa Bunge ukutane kwa haraka ili kushughulikia malumbano yaliyopo kwenye vikao vya Bunge vinavyoendelea hivi sasa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, wasomi hao na wanaharakati walisema kuwa kuendelea kwa hali hiyo, kutawafanya wananchi wapoteze imani kwa Bunge lao wanaloliamini.
Msomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), katika Idara ya Sayansi ya Siasa, Bashiru Ally, alishauri wasimamizi wa Bunge watoe maelekezo stahiki kwa wabunge waliopo kwani kauli zao ama vitendo vyao vina athari za muda mrefu.
Suala hili la ushabiki wa kisiasa, chuki binafsi viongozi wa Bunge watawajibika, inawabidi wafanya kikao waliangalie suala hili kwa undani, kwani ni zito ili waweze kurudisha imani kwa wananchi, alisema.
Kwa upande mwingine alisema kuwa wabunge ni viongozi wa wananchi, hivyo matendo, kauli, mavazi ama kusinzia kwao bungeni, vinawaathiri. Kama viongozi wa siasa watahukumiwa kwa matendo yao.
Msomi huyo wa UDSM, alisema hali inayoonekana hivi sasa, inawezekana tabia za wabunge, matakwa na fikra zao zina msukumo zaidi kuliko taratibu zilizopo, na pia kuna aina fulani ya Bunge kushindwa kusimamia kwa kanuni zilizopo.
Viongozi wasipokuwa makini, Bunge litapoteza imani kwa wananchi, kwa kuwa matarajio ya wengi ni kuona mijadala inaendeshwa kwa uhuru na hoja.
Matokeo imani yao itashuka. Mbele ya safari maamuzi yanayotolewa na Bunge yanaweza yasiheshimiwe na wananchi, alisema Ally.
Alieleza kuwa inawezekana kuwa kuwepo kwa hali hiyo ni kutokana na kanuni kupitwa na wakati au kuna ukiukwaji wa makusudi au hakuna taratibu.
Msomi mwingine, wa UDSM kutoka idara hiyo hiyo, Profesa Gasper Mushi, alisema kuwa anachokiona hivi sasa, ni kwamba Bunge limepoteza mwelekeo na kuacha kusimamia mambo muhimu, na badala yake linasimamia mambo binafsi ya vyama.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Uongozi, Hebron Mwakagenda, alisema kuwa mambo yanayoendelea bungeni hivi sasa ni utoto wa kichama, kwa kuwa uanachama umezidi, yote hayo ni kwa sababu hakuna maslahi ya taifa bali ya chama.
Watu wasiotarajiwa kufanya hivyo, wameingia kwenye mtego huo. Nchini India mtu akichaguliwa kuwa mbunge anakwenda chuoni kwa ajili ya kufundishwa jinsi ya kutawala, alisema Mwakagenda.
Alisema, kinachotia moyo hivi sasa kuna fursa ya kutengeneza Katiba mpya ambayo itaainishwa ni nini cha kufanya kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Acha utoto uendelee hapo ndipo tunachuja chuya na mchele, ili tujue viongozi bora ni kina nani, alisema mkurugenzi huyo.
<b>Dk. Slaa asikitishwa </b>
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa malumbano ya dhahiri yanayoendelea hivi sasa bungeni baina ya viongozi wa Bunge, wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala cha CCM, ni matokeo ya uongozi mbaya ndani ya Bunge hilo.
Slaa alisema hayo alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima, kuhusu malumbano yanayoendelea katika Bunge linaloendelea mjini Dodoma.
Nafikiri kama uongozi wa Bunge hautabadilisha mwelekeo wake wa kuilinda CCM na serikali, hali hiyo haitavumilika, kwani Bunge haliongozwi kama mtu anavyotaka, akiamka siku hiyo.
Kwa mfano jana (juzi), Naibu Spika wa Bunge tokea asubuhi alisema atawatoa watu, na kweli aliwatoa mpaka nje ya geti. Lakini ukiangalia kauli hiyo ya Ndugai, haikuwa popote, alisema Slaa.
Slaa aliongeza kuwa hata katika hotuba ya wapinzani iliyosomwa bungeni, hakuna jambo lolote lililozungumzwa kule ambalo halipo, kwani yote yaliyozungumzwa ni ya kweli.
Kusema ni uchochezi ni kinyume cha kutoa uhuru kwa kila mtu, alisema Slaa.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, mambo yote yanayotokea bungeni ni dalili ya kuwa uongozi wa Bunge uliopo hauna uwezo wa kuongoza Bunge la vyama vingi, ama kwa tafsiri nyingine, wanalinda serikali, matokeo Bunge litafika mahali pabaya.
Nimepigiwa simu nyingi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, tunapongezwa, wanasema tuongeze nguvu na vijana walioko bungeni waongeze nguvu.
Wajue kazi ya vyama vya upinzani si kupiga makofi bali ni kukosoa serikali. Tusifike mahali tusilaumiwe kuwa vijana wetu wanaleta vurugu. Kanuni zipo wazi, tafsiri hazitegemei jinsi Naibu Spika alivyoamka siku hiyo, alisema.
Alisema kuwa utaratibu uliopo hivi sasa wa spika wa Bunge Anne Makinda na naibu wake Ndugai, kuomba uthibitisho kila siku kwa mambo mbalimbali yanayozungumzwa bungeni na wapinzani na pale unapotolewa haufanyiwi kazi, ni sawa na kufanya mazingaombwe.
Vijana wangu karibia saba waliambiwa watoe uthibitisho wa yale waliyoyazungumza, lakini walipowasilisha vielelezo, Spika na wenzake wamekaa kimya. Wanatafuta visingizio vya kupotosha ukweli. Uthibitisho unapopelekwa unawekwa kwenye kabati, alisema Slaa.
NCCR nao wazungumza. Naye Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema kuwa kinachoendelea bungeni hivi sasa ni matokeo ya mfumo mzima uliopo.
Alisema, ili mtu apate haki yake inabidi apambane, kwa kuwa mfumo tuliojikita ni wa kifisadi, umeacha pengo kubwa kwa walichonacho na wasichonacho.
Hali hii ni matokeo ya mfumo mzima uliopo, mfumo wa biashara ama mfumo wa siasa, ili upate haki yako hapa nchini inabidi upambane, alisema Mbatia.
Aliongeza kuwa vyombo vya kufanya maamuzi vinaonekana havifanyi kazi zake vizuri, athari yake ni maangamizi kwa taifa.
Mbatia alisema Bunge ndiyo linasimamia serikali na kuishauri, lakini kinachoonekana hivi sasa, hakuna kuaminiana kati ya Bunge na serikali.
Alisema, kinachoonekana bungeni hivi sasa watu wana shauku ya kuzungumza lakini wanaminywa uhuru huo, na wengine wanapata nafasi ya kuzungumza wanachotaka.
<b>CCM watoa taarifa </b>
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es salaam Kilumbe Ngenda amesema kuwa vurugu, utovu wa nidhamu, jazba na ubabe vinavyojitokeza kwa baadhi ya wabunge katika kikao cha Bunge mjini Dodoma haionyeshi kuwa dhana ya kupata wabunge wenye sifa imezingatiwa.
Katika kikao chake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema kuwa vitendo vinavyofanywa bungeni na baadhi ya wabunge vinawatia aibu wanasiasa wote ukiacha tofauti zao za kiitikadi.
Tunataka wabunge watulie kwenye viti vyao na wafanye masuala ya msingi kama walivyoagizwa na wananchi wao na si kuendekeza masuala yasiyo kuwa ya msingi, alisema Ngenda.
Aidha alisema kuwa hatua hiyo ya baadhi ya wabunge kukosa nidhamu ya kutofata taratibu walizojiwekea wawapo bungeni ni kielelezo cha wazi kuwa vyama vyao havikuwachuja vizuri na wananchi hawakupata walichokusudia.
Hata hivyo alitetea vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi bungeni akisema kuwa CCM na serikali yake ni vyombo vya wanadamu na vinaongonzwa na wanadamu hivyo hutegemei yasiwepo mapungufu na kwamba ni ukweli na imani kuwa kazi ya mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke haikosi mapungufu.
Kutokana na hilo Ngenda alisema katika kuchagua viongozi unatafuta yule ambaye hata kama ana mapungufu ni bora kuliko wenzake, na hali hiyo imejidhihirisha bungeni kwa sasa kuwa wabunge wa CCM ni afadhali kuliko wale wa CHADEMA.
Hivi unaweza ukaunda serikali yako ukaletewa jina la Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini ambaye ndiye Waziri Kivuli wa mambo ya ndani iwapo CHADEMA ingeunda serikali, tutategemea ndiye angekuwa waziri wa wizara hiyo?
Ungeletewa jina la Shamsi Vuai Naodha Waziri wa mambo ya Serikali, unaweza kweli ukaamua Waziri awe Lema? Ambaye anaweka Jazba, Kiherehere na Ubabe kama vitendea kazi muhimu vya akili yake sidhani! alisema Ngenda.
Ngenda aliwapongeza wabunge wa CCM na viongozi wote wa Bunge, akimpongeza kwa kumtaja jina mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe ambaye alisema kuwa aliona uchungu na nje ya Bunge aliwaaasa wabunge wenzie waliotoka nje baada yu kutolewa mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje kwa amri ya mwenyekiti.
Alimalizia kwa kumkumbusha Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni awe kweli ni kiongozi wa wapinzani na kwamba aonyeshe hilo kwa kulaani vitendo vya wabunge kukosa nidhamu wawapo bungeni.