Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Nilikutana na kijana mmoja wa kwetu Pemba ambae siku nyingi sijamuona hapa Dar. Nikamuuliza vipi salama na mabomu ya Mbagala na mbona sijakuona siku nyingi kwetu Pemba ? Alinijibu, ya Mbagala salama lakini hayo mabomu ya Pemba ndio yalionikimbiza na sina hamu ya kurudi kwa miaka hii. Ndipo akanipa mkasa huu hapa chini:
Kuna wakati fulani wa Uchaguzi, kulizuka kile kilichoitwa uripuaji wa mabomu Pemba. Yeye alikuwa ni mmoja katika vijana waliokamatwa Pemba akihusishwa na uripuaji huo.
Akapelekwa katika kikao kimoja wapo cha dola kuhojiwa. Wakati anahojiwa, Mkuu wa Mkoa, akamwambia Kamanda wa Polisi, "Huyu niachie miyee"
Mkuu wa Mkoa akamuuliza yule kijana, "Wewe umesoma skuli?" Jibu "Ndio" Gavana akauliza tena "Mpaka darasa la ngapi?" Jibu, "Form IV" Gavana akaendelea, " Umesoma masomo gani?". Jibu likawa, "Masomo yote" Akaendelea Mkuu, " Hapana, nataka unitajie hassa"
Kijana akaanza kutaja, " English, Kiswahili, Gegraphy ....n.k. Alipofika Physics, Mkuu wa Mkoa akamwambia Kamanda " Huyu aweza".
Ndipo kijana huyo akenda kuchezea mkong'oto uliomhamisha kwao mpaka leo.
Wana JF, hio ndio evidence ambayo ili m-convict huyo kijana, na yote kutokana na wasomi wa CCM ,ambao eti mtu kasoma somo la fizikia basi atakuwa na uwezo wa kutengeneza na kupasua mabomu.
Na huo ndio mkasa niliotaka na nyinyi muusikie!!!