WASOMI: Tatizo si Mawaziri ni Mfumo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WASOMI: Tatizo si Mawaziri ni Mfumo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, May 5, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jumamosi, 05 Mei 2012

  Na Fidelis Butahe | Mwananchi

  BAADA ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza lake la mawaziri ikiwa ni pamoja na kuwaondoa mawaziri sita waliokuwa wakishinikizwa wajiuzulu, wasomi wamesema kuwa kinachotakiwa kubadilishwa ni mfumo wa utawala na siyo sura mpya za mawaziri.

  Wasomi hao waliozungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya Rais Kikwete kufanya uteuzi huo walisema mfumo ndio unaosababisha mambo kutokwenda sawa katika wizara na idara mbalimbali za serikali.

  Mawaziri walioondolewa ni pamoja na Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii, William Ngeleja wa Nishati na Madini, Omar Nundu wa Uchukuzi, Cyril Chami wa Viwanda na Biashara, Hadji Mponda wa Afya na Ustawi wa Jamii na Mustafa Mkulo wa Fedha.

  Mawaziri walionusurika katika sakata hilo ambapo pia walikuwa kashfa ni wawili, George Mkuchika na Jumanne Maghembe ambao hata hivyo wamehamishwa kwenye wizara zao za awali; Tamisemi na Kilimo. Akizungumza na Mwananchi akiwa nchini Ureno Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Emmanuel Mallya alisema licha ya kuwa mabadiliko yamefanyika lakini sio suluhisho kutokana na nchi kuwa na mfumo mbovu wa utawala.

  Alisema mawaziri waliokumbwa na kashfa mbalimbali walitakiwa kusimamishwa kazi ili wachunguzwe na kama ingebainika hawana hatia wangerudishwa kazini. "Kama wangekutwa na hatia wangefunguliwa mashitaka, hii ingewafanya wengine kuogopa kutafuna mali za umma kwa kuhofia kuwa watasimamishwa kazi na kuchunguzwa" alisema Mallya. Alifafanua kwamba kitendo cha baadhi ya viongozi kuteuliwa si kizuri na kusisitiza kuwa inatakiwa liwapo baraza maalum la kuwafanyia usaili watu wanaofanya kazi za kuwatumikia wananchi na kuwatolea mfano Majaji.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alimpongeza Rais Kikwete kwa kufanya uteuzi huo ikiwa ni pamoja na kuwang' oa mawaziri waliokuwa wakilalamikiwa, lakini alionyesha wasiwasi wake katika suala zima la mfumo wa uongozi na kusema kuwa ndio unaowafanya wananchi kulalamika kila kukicha.

  "Rais amekidhi matakwa ya wabunge, wananchi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kuwaondoa mawaziri waliokuwa wakilalamikiwa, uamuzi huo unatosha na unaonyesha usikivu wake" alisema Dk Bana. Hata hivyo, Dk Bana alisema kubadilisha sura za mawaziri sio dawa na kwamba dawa ni kubadilisha mfumo mzima wa utawala.

  "Kitendo cha waliokuwa manaibu waziri kupandishwa kuwa mawaziri ni jambo zuri, binafsi nadhani manaibu mawaziri wamekuwa wengi, angeweza kuwapunguza na utendaji wa kazi ungeendelea kuwa safi" alisema Dk Bana. Profesa mwingine wa chuo hicho, Gaudence Mpangala alisema mawaziri hao walitakiwa kujiuzulu baada ya ripoti ya CAG na ripoti za Kamati za kudumu za bunge kuanika kashfa zinazowakabili.

  "Ilinishangaza kuona wengine wakijitetea wakati ripoti zilikuwa zinaeleza kila kitu, mtu ukiwajibika sio lazima uwe umetenda kosa, mbona Rais Ali Hassan Mwinyi aliwajibika kwa makosa ya wengine na baadaye akawa rais wa Tanzania," alisema Mpangala.

  Hata hivyo, Profesa Mpangala alisema kuwa tatizo sio kubadili baraza la mawaziri, kubadili mfumo mzima wa utawala na kusema kuwa uteuzi huo sasa unaonyesha wazi kuwa utamaduni wa kulindana ndani ya CCM unafika.

   
 2. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Kwenye mfumo mbovu hata mtu mwaminifu anakuwa mwizi, lakini kwenye mfumo imara hata mtu mwizi anakuwa mwaminifu !

  Serikali za ulaya hazikumbani na matatizo kama haya kwa kuwa mifumo yao ni imara.

  Kwetu TZ mfumo imara ni ngumu kupatikana kwa kuwa mifumo mibovu ina manufaa makubwa kwa hao wakubwa wenye hiyo dhamana ya kubadili mifumo.

  From me Goodrich, 05 May 2012.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  ..siyo kweli.

  ..matatizo yanayotokea hapa Tanzania ni hayahusiani kabisa na kasoro ktk mfumo wetu bali ni hujuma za waziwazi.

  ..mfumo wetu umempa madaraka Raisi wetu ya kutekeleza ajenda na malengo yake bila kukwamishwa na wanasiasa wenzake.

  ..nitawapa mfano: wakati wa kampeni Raisi Obama aliahidi kufanya marekebisho makubwa ktk mfumo wa utoaji huduma za afya Marekani. Alipoingia madarakani wapinzani wake toka chama cha Republican wamemkwamisha kutekeleza mpango huo. Sasa kuna serikali za majimbo kadhaa ambazo zinapinga waziwazi mpango huo wa Raisi Obama.

  ..Richmond,EPA,IPTL,ATC, bandari, etc haikusababishwa na mfumo mbovu bali tamaa za watu kutafuta utajiri wa haraka bila kufanya kazi.

  ..Waziri Mkuu anapodai hawezi kuwachukulia hatua mawaziri wenzake, au hata makatibu wakuu wa wizara, ni uongo wa mchana kweupe.

  ..mbona CD Msuya alipendekeza Mrema afukuzwe kazi baada ya kukiuka utaratibu wa collective responsibility ktk kikao cha bunge??

  ..mbona RM Kawawa alipendekeza Kingunge Ngombale Mwiru atimuliwe ktk nafasi yake ya ukuu wa mkoa baada ya kupinga mswada uliowasilishwa na serikali bungeni?

  ..mbona AL Mrema alipendekeza Silvano Adel[PS mambo ya ndani] na Tryphon Maji[rpc dsm] wafukuzwe kazi kwa kumtoa mfanyabiashara mhindi toka mahabusu kinyume na utaratibu/maagizo??
   
 4. n

  nunu Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nami naungana na wenzangu kumpongeza Mtukufu Rais hasa pale alipotamka uwajibikaji utashuka hadi kwa watendaji. Ni muhimu sasa Katiba mpya ijayo iyaone haya yote na iboreshe mfumo mzima wa utendaji/ufanisi na swala zima la uwajibikaji. Ni takribani mwezi sasa muda mwingi umetumika kujadili jinsi baraza jipya la mawaziri litakavyokuwa wakati idadi kubwa saana ya wananchi hawaridhiki na huduma za jamii ikiwemo kilo ya sukari kufikia ths 3000 karibu dola 2 kwa mwananchi anayeishi chini ya kiwango hicho kwa siku.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  nunu,

  ..lakini Raisi amekuwa madarakani kwa miaka 7 sasa.

  ..alijiandaa kuchukua Uraisi kwa miaka 10 toka 95 mpaka 2005.

  ..halafu amekuwa serikalini sasa kwa zaidi ya miaka 20.

  ..hivi inaingia akilini kwamba sasa ndiyo anakumbuka kwamba uwajibikaji uende mpaka wa civil servants mawizarani???

  ..mimi nadhani kwa kauli hiyo ya Raisi, wa-Tanzania tulipaswa tuwajibishe yeye mwenyewe.

  ..kama anafikiri makatibu wakuu ndiyo wenye matatizo basi alipaswa kuwatimua makatibu wakuu na kuwaacha mawaziri wake anaotaka tuamini ni wachapakazi.
   
 6. n

  nunu Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Una hoja hapo ila ni kazi sana ku manage damage kuliko ku control. Nafikiri pia uendeshaji wa serikali si wa Rais pekee kwani kama kila mtu angetimiza wajibu wake kikamilifu mapungufu mengi kama haya yasingetokea. Naamini si bunge tu litawabana wenye dhamana zao bali hata mkuu nae ataendelea kuwawajibisha kwa kasi mpya.
   
 7. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  RAIS Jakaya Kikwete ameingia kwenye wakati mgumu baada ya kudaiwa kushindwa kutimiza kiu ya Watanzania, kwa kuchagua baraza kubwa la mawaziri pamoja na kuwajumuisha wale wasiotakiwa.

  Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa uteuzi huo sasa umezusha upya vita ya makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikalini ambayo kwa kiasi kikubwa itasababisha kudorora kwa utendaji wa shughuli za kila siku.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa Rais Kikwete ameongeza mzigo zaidi kwa Watanzania kwa kuteua mawaziri na naibu mawaziri 55 kutoka 50 wa awali.

  Wanabainisha kuwa ukubwa wa baraza si tija iwapo wale walioteuliwa ni wachapakazi na wenye historia nzuri ya uwajibikaji lakini wengi wa waliorejeshwa walikuwapo kwenye baraza lililopita ambalo lilishutumiwa kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo.

  Miongoni mwa mawaziri waliotuhumiwa kutowajibika vizuri ni Profesa Jumanne Maghembe, aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Chakula ambaye sasa amehamishiwa Wizara ya Maji na George Mkuchika, aliyekuwa Tamisemi sasa amehamishiwa Ofisi ya Rais Utawala Bora.

  Wachambuzi hao waliweka bayana kuwa Mkuchika hakupaswa kuwamo kwenye baraza hili jipya, kwakuwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma ulifanyika kwenye halmashauri ambazo yeye alikuwa waziri wake.

  Wanaweka bayana kuwa Mkuchika alitakiwa na wabunge ajiuzulu lakini kutokana na ukaribu wake na Rais Kikwete amerejea kwenye uwaziri kwa kupewa wizara ambayo itakuwa ikiwajibika kwa kiongozi mkuu wa nchi.

  Uhamisho uliofanywa kwa Maghembe nao umeonekana kulitia doa baraza la mawaziri kutokana na utendaji usioridhisha wa kiongozi huyo, ambaye alishindwa kuzuia ubadhirifu wa mbejeo za kilimo, zikiwamo mbolea za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa wakulima.

  Katika utawala wa Maghembe wakulima walikuwa wakilalamikia kushuka kwa bei ya pamba, korosho, ununuzi wa kahawa mbichi na kuuziwa matrekta madogo kwa bei ya kulanguliwa, ilhali serikali ilitangaza mkakati wa kukinyanyua kilimo na kufuta kodi kwenye bidhaa hizo.

  Jambo jingine ambalo linaonekana kuwakera baadhi ya watu ni kurejea kwa Celina Kombani kwenye baraza hilo, huku akiwa ni miongoni mwa mawaziri wanaodaiwa kufanya vibaya zaidi TAMISEMI, alikokuwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Ripoti ya CAG, iliyosomwa hivi karibuni bungeni na kubainisha ubadhirifu mkubwa ni ya mwaka 2009/2010, ambapo Kombani alikuwa waziri lakini sasa amehamishiwa Ofisi ya Rais-Utumishi.

  Tanzania Daima Jumapili lilidokezwa kuwa baadhi ya mawaziri walioondolewa kwenye nafasi zao bado wamekuwa na kinyongo kwa madai kuwa hawakufanya makosa bali fitina, hila na mbinu chafu ndizo zilizotumika.

  Miongoni mwa walio lia na rafu hizo ni Omari Nundu (aliyekuwa Uchukuzi), Cyril Chami (Viwanda na Biashara) na Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), ambao kwa nyakati tofauti inadaiwa waliwasilisha utetezi mzito wa kulinda ‘vibarua’ vyao.

  Inadaiwa mmoja wao alibubujikwa machozi kwenye kikao kimoja baada ya kuona wajumbe wakimsisitiza awajibike kisiasa ili ailinde serikali na chama tawala.

  Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa sasa mpasuko uliokuwapo baina ya makada wa CCM utazidi kuimarika na kuna uwezekano mkubwa chama hicho kikazidi kupoteza wanachama ambao inasemekana wanalenga kuhamia upinzani.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaainisha kuwa baraza jipya sasa litakuwa na kazi kubwa ya kupambana na makada wenzao, kushughulikia matatizo ya wananchi pamoja na kuwatumikia wananchi wa majimbo yao.

  Wanaweka bayana kuwa huu utakuwa wakati mgumu kwa baraza hilo, kwa sababu wengi wao wataangalia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ikiwamo kutafuta kundi la kuliunga mkono katika nafasi ya kuwania kiti cha urais.

  Kwa muktadha huo, wachambuzi hao wanabashiri kuwa utawala wa Rais Kikwete utapata wakati mgumu zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

  Dk. Slaa anena

  Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kubadilisha baraza la mawaziri si ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wananchi au ubadhirifu, bali kinachotakiwa kufanywa hivi sasa ni kuufumua mfumo wa utawala.

  Alisema utawala wa sasa ndio wenye kulea, kuwalinda na kuwatetea wabadhirifu, hivyo hata kama mabadiliko yatafanyika mara kwa mara tatizo husika halitakwisha.

  “Kubadilisha mawaziri ni sawa na mtu aliyekuwa akila mkate mkavu akatokea mtu mwingine na kumpakia siagi kisha akampa aule, hapa huwezi kusema kuna mabadiliko kwakuwa mkate ni ule ule,” alisema.

  “Hebu fikiria mtu anapobadilisha shati, nini kinatokea? Kinachobadilika pale ni shati tu, mtu anabaki kuwa yule yule,” alisema.

  Dk. Bana alisifia

  Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, ameupongeza uteuzi huo na kusema ana tumaini kuwa Rais Kikwete aliwateua watu anaowaamini kuwa watafanya vizuri kwenye eneo husika.

  Aliwataka Watanzania kuwapa muda mawaziri wafanye kazi zao badala ya kuendelea kuwashutumu kabla ya kuanza kutekeleza majukumu waliyopewa.

  Mbowe afunguka

  Naye Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema Rais Kikwete amekiuka Katiba kwa kuteua wabunge ambao hawajaapishwa kuwa mawaziri pamoja na kuteua mbunge wa Zanzibar kuongoza wizara isiyo ya Muungano.Alisema kuwa ni hatari sana kwa kiongozi wa nchi aliyeapa kuilinda Katiba lakini anakuwa wa kwanza kuivunja, kwa kile alichosema kuwa Rais, Kikwete aliamua kumteua mtu kuwa mbunge saa nane kisha saa tisa anakutana naye, saa 10 anamtangaza kuwa waziri.

  Mbowe alisema kuwa uteuzi wa Dk. Hussein Mwinyi anayeingia bungeni akitokea Jimbo la Kwahani Zanzibar kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, haukuwa sahihi, kwani wizara hiyo si ya Muungano.

  Alibainisha kuwa kwenye awamu iliyopita ilikuwa sahihi kwa Dk. Mwinyi kuongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kutokana na kuwa aliingia bungeni kupitia Jimbo la Mkuranga, ambalo liko Tanzania Bara.

  Mbowe alisema hivi sasa anakwenda kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri vivuli ili kuliandaa vizuri na kuwasilisha bajeti mbadala kwenye Bunge lijalo linalotarajiwa kukutana mwezi Juni.
   
 8. s

  slufay JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwacheni amiri jeshi mkuu afanye kazi yake, nyie kazi yetu ni kupiga kelele tu, mbona uliruhusu mwanaharamu apite wakati uundwaji tume ya mabaduiliko ya Katiba....................?
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Katibu mkuu wa CDM Dr Wilbrod Slaa ameliponda baraza jipya la mawaziri na akasema wananchi wasitarajie chochote kipya katika maisha yao.
  Dr Slaa amesema kinachotakiwa kubadilishwa ni mfumo mzima wa utawala na muundo wenyewe wa baraza hilo.Dr Slaa amesema kubadilisha sura na kuongeza idadi ya mawaziri kutoka 50 hadi 55 si suluhisho la matatizo ya watanzania bali ni kuwaongezea maumivu zaidi.

  Source:Tanzania daima Jumapili.
   
 10. s

  slufay JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa nini huwa wapinzani hawatoi mbdala wa tatizo huwa wanaponda tu,, ,,,,, suluhisho nini,,,, toeni mbdala wa tatizo.
   
 11. mwenyenchi

  mwenyenchi JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Upuuzi juu ya upuuzi, hakuna lolote jipya mambo yatakuwa yaleyale
  Hao 'wapya' nini kitawazuia wasiibe kama wenzao?
  Unaiba, unapumzishwa (ajali ya kisiasa) unaendelea kula kilaiiiiiiiini.. (muulize EL, Karamagi, Msabaha, Chenge etc)
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja 100%.
   
 13. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Wapinzani hawawezi kuifundisha CCM namna ya kuongoza. Hiyo si kazi yao. CCM watafute wenyewe suluhisho...
   
 14. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,780
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280

  Sidhani kama ni kazi ya wapinzani kutoa mbadala au kushauri. Kama CCM hawajui au hawana suluhisho wanapaswa kuondoka madarakani na si kushauriwa. By the way waliingiaje madarakani bila kuwa na mbinu za kulikwamua taifa kutokana na matatizo lililo nayo?
   
 15. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  kubadilisha mfumo wa utawala. Yaani nyie ccm mkae pembeni Chadema iwaonyeshe kinachotakiwa kufanya. sasa wewe unataka ufuliwe socks wakati umezivaa?.
   
 16. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Magamba at work.
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hii kitu inaitwa "chupa mpya, mvinyo ule ule". Nothing new!
   
 18. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Wewe pevuka katiba uliambiwa inatokana na chama tawala pekee??Hata hapo alipo alifanya makosa ilibidi tume huru siyo hii yakibabaishaji!
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,347
  Trophy Points: 280
 20. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Mbona Dr amesema wazi suluhisho ni nini; au gamba limekubana hadi macho hayana ushirikiano?
   
Loading...