Wasomi na ndoto za Abunuasi

ukikaa na wanachuo utawahurumia jinsi walivyo na ndoto za kumaliza chuo na maisha kua kama ya messi vilee,yani ni fulu ndoto za abunuasiii.

hata mm nilkua ndoto hizohizo za abunuas nikiwa chuo sema mm Allhamdulillah nikamaliza chin ya j kikwete our dady tunae mmiss hiv sasa
sasa hawa wa mzee wa kazi amahakika kazi wanayo
 
Maisha kitaani ni degree nyingine ...huku hakunaga ndoto kama mipango hamna basi benchi litakuhusu sana.
 
NDOTO za abunuwasi mkuu umesema kweli.Unakaa mtaani miaka inapita mingi bila kupata ajira.Unaamua kupata kozi nyingine ya kukupatia ajira chapchap,unapata lakini mshahara wake ni mdogo.Unabaki na maarifa makubwa yasiyoendana na elimu uliyonayo.Bora kujijengea dhana ya kujiajiri tangu mwanzo.
 
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.

Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo!
Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako!

Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na "vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa "kujilipua".

Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!

Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!

Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.

Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!
Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni!

Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu!

Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vascoda Gama", baada ya shida kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani vyuo vimefungwa?

Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.

Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi #JIPANGE jombaaaaaaaaaa m
Nimeipata sehemubora nishee nanyi maana Kuna wanafunzi humu so ukipata boom yako jua Kuna kilimo na ufugaji baadae
Nilitamani ''nikutukane'' (aahahaaa) kwa jinsi post yako hiyo ilivyotulia lakini nimefurahi sana maana kuna philosophy na psychology kibao katika ujumbe wako huo.
Wengi wetu tuliosoma hasa miaka ya Boom la HESLB tunajua tulivyoteseka kufukuzia hilo boom kwa shida halafu unamaliza chuo kimagumashi lakini tunaonekana kituko mbele ya wanajamii.
Lakini mbaya zaidi ni wale walioonekana vipanga kustruggle kupata ajira huku wenzangu na mimi darasani ndio wakikwaa miajira kwa haraka.
Asante mzee maana pamoja na sterling kusalimika kwenye mapigano hayo lakini tunajua jinsi cha moto tulivyokiona maana mtu unakaa kitaa miaka hata mitatu hauna ramani inayoeleweka.
 
Naomba kutoa mfano wa kweli wakuu kuhusu ndoto za abunawasi kwa wasomi.Kuna jamaa alisoma vizuri tu mpaka ngazi za juu,akapata vyeti vyake vizuri tu.Jamaa akakaa mtaani muda mrefu akisubiri ajira.Akafanya usaili mara nyingi bila mafanikio.Jamaa akaenda kusoma kozi nyingine akafaulu.Karudi mtaani kusubiri ajira tena,muda unaenda ajira hapati.Kuna kozi moja ajira zake zipo nje nje jamaa kajisajili kuisomea.Bahati mbaya hii kozi jamaa alifeli na hakupata sifa kuajiriwa liacha kuwa na maarifa mengine makubwa.Umri wa ujana unapita.Jamaa ikabidi ajifunze mafanikio kwa aliowaacha mitaani miaka mingi iliyopita.Ndoto za kujiajiri hazipotei malengo.
 
Print hii kitu ukaiweke pale kwy mbao za matangazo Ud,Ifm,TIA nk manake hata ukisikia story zao tu wakiwa kwy vibweta au room utachoka matarajio ni makubwa sana kuliko uhalisia!Ni vyema wkt unasoma uku unakimbiza mishemishe ndogondogo
 
Uzi huu ulishakuja hapa jamvini..nashauri ungepitia kwanza kabla ya kutuma...yani ni copy and paste
 
Unatoka chuo unakuwa unaplane uliyoijenga kichwani kuwa nitafanya hv nitafanya vile kumbe picha ni tofauti mtaani huku maisha ni sarakas
 
Naomba kutoa mfano wa kweli wakuu kuhusu ndoto za abunawasi kwa wasomi.Kuna jamaa alisoma vizuri tu mpaka ngazi za juu,akapata vyeti vyake vizuri tu.Jamaa akakaa mtaani muda mrefu akisubiri ajira.Akafanya usaili mara nyingi bila mafanikio.Jamaa akaenda kusoma kozi nyingine akafaulu.Karudi mtaani kusubiri ajira tena,muda unaenda ajira hapati.Kuna kozi moja ajira zake zipo nje nje jamaa kajisajili kuisomea.Bahati mbaya hii kozi jamaa alifeli na hakupata sifa kuajiriwa liacha kuwa na maarifa mengine makubwa.Umri wa ujana unapita.Jamaa ikabidi ajifunze mafanikio kwa aliowaacha mitaani miaka mingi iliyopita.Ndoto za kujiajiri hazipotei malengo.
ukwel mtupuuu...
 
Print hii kitu ukaiweke pale kwy mbao za matangazo Ud,Ifm,TIA nk manake hata ukisikia story zao tu wakiwa kwy vibweta au room utachoka matarajio ni makubwa sana kuliko uhalisia!Ni vyema wkt unasoma uku unakimbiza mishemishe ndogondogo
kabisa yan mana twabweteka sn
 
Alafu wengi wanaishi maisha ya kuekti, hawako real Maisha ya Chuoni ni kwamba ukiwa kule
unakuwa una sabuni ya kuogea na naya kufulia
lakini ukirudi mtaani sabuni ya kufulia ndio
hiyo hiyo ya kuogea
 
Back
Top Bottom