Wasomi kugoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi kugoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 21, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,137
  Trophy Points: 280
  Wasomi kugoma

  na Deogratius Temba
  Tanzania Daima~Sauti ya watu

  VYUO vikuu vyote nchini, vimepanga kuitisha mgomo usiokuwa na kikomo mwishoni mwa mwezi ujao, kuishinikiza serikali kufuta sera ya elimu inayolazimisha wanafunzi kuchangia gharama za masomo.

  Nia hiyo ya wasomi wa vyuo vikuu kugoma ilitangazwa jana na Katibu Mkuu wa Umoja wa marais wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAHLISO), Mtatiro Julius kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

  Mtatiro alisema wanafunzi wa vyuo vikuu vyote nchini wamethibitisha kushiriki katika mgomo huo wa kuishinikiza serikali kuondoa sera hiyo ambayo inapingana na sera ya elimu ya juu nchini ya mwaka 1999.

  Mtatiro, ambaye alikuwa akisoma taarifa ya pamoja ya umoja wa marais wa vyuo vikuu nchini, alisema maandalizi ya mgomo huo yameshakamika na utaratibu maalumu unaowataka wanafunzi wote kushiriki mgomo huo, umeshapelekwa katika vyuo vikuu vyote nchini.

  “Mgomo huu utakuwa wa kitaifa na utahusisha taasisi zote za elimu ya juu Tanzania Bara na Visiwani na tumethibitisha kuwa wanafunzi wote wanauunga mkono kwa zaidi ya asilimia 90. Hautakuwa na kikomo, sote kwa pamoja tumeamua kuishinikiza serikali iifute sera kandamizi ya kikatili ya uchangiaji wa elimu ya juu.

  “Ili kuhakikisha wanafunzi wote tunashiriki, tumepanga Oktoba 25, kufanya maandamano yatakayowashirikisha wanataasisi wote wa elimu ya juu. Maandamano haya yatazunguka ndani ya vyuo tu na yatakuwa maandamano ya amani, haya yatakuwa salamu zetu kwa wahusika juu ya mgomo wetu tuliopanga kuwa utaanza Oktoba 27,” alisema Mtatiro.

  Akizungumza jinsi mgomo utakavyokuwa, alisema utakuwa tofauti na migomo mingine ambayo imekuwa ikifanyika kwa fujo, jambo ambalo hawataruhusu litokee kwa sababu wamekubaliana kugoma kuingia madarasani na kufanya maandamano kuzunguka maeneo ya vyuo tu.

  Alisisitiza kuwa mgomo huo ni lazima ufanyike kwa sababu wanafunzi wamekatishwa tamaa na kauli za kejeli ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, kila wanafunzi hao wanapowasilisha malalamiko yao katika wizara hiyo.

  Alisema kejeli hizo za Waziri Maghembe zimewadhihirishia wanafunzi wa elimu ya juu kuwa serikali haitaki kusikia wala kutatua matatizo hayo, licha ya jitihada zao za kupeleka barua inayoelezea malalamiko yao kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Shamsi Vuai Nahodha.

  Wakati hali ikiwa hivyo kwa vyuo vikuu nchini, kwa upande wa Chuo Kikuu cha Ardhi cha Dar es Salaam, hali inaonekana kuwa tete zaidi baada ya wanafunzi wa chuo hicho kutishia kugomo kuanzia kesho Jumatatu, wakipinga hatua ya uongozi wa chuo hicho kutowapatia matokeo ya mitihani ya muhula wa pili wa mwaka wa masomo 2007/08 ambao hawajakamalisha kulipa karo.

  Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (ARISO), Antony Massawe, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa wameutaka uongozi wa chuo hicho kutangaza matokeo hayo yaliyozuiwa haraka, ili wanafunzi wote wajue kama wamefaulu au wanapaswa kufanya mitihani ya marudio inayoanza kesho.

  “Chuo kinafunguliwa Jumatatu kwa wanafunzi kufanya mitihani ya marudio, lakini wengine mpaka sasa hawajapata matokeo yao kwa kigezo cha kutomaliza karo ambayo wameshindwa kuchangia baada ya Bodi ya Mikopo kuwalipia kiasi kidogo, hili litaleta shida.

  “Hatutavumilia kuona mwenzetu yoyote anashindwa kuendelea na masomo, kufukuzwa chuo au kurudishwa mwaka nyuma, itatugharimu uhai kuliko kunyamazia hilo. Tunachosisitiza ni kwamba, kesho chuo kitafungwa tena kwa kutoingia madarasani mpaka hapo tatizo la wenzetu litakapo tatuliwa.

  “Umma wa Watanzania utuelewe kuwa kama wenzetu hawatapewa matokeo yao, hawatafanya mitihani kesho, tutafunga chuo mpaka hapo watakapopewa matokeo yao na kuruhusiwa kuendelea na masomo bila ya shida yoyote,” alisema Massawe.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Sep 21, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Wasitudanganye, tumejua siku nyingi kuwa mgomo huu ni one of CCM's government strategies to gain popularity towards 2010! sounds ridiculous!!, watagoma, watasikilizwa Kikwete atapendwa tena! Mtatiro hebu zungumzia hili.....,

  Kwa nini msiandamane Kikwete ajiuzulu?

  Waberoya
   
Loading...