Msomi anayechukua upande kwenye siasa ni msomi wa kutiliwa shaka kwa sababu, kwa aina ya siasa zetu, atatakiwa ashangilie kila kitakachofanywa na chama chake hata kama ni cha kipumbavu na aponde kila kitakachotoka upande hasimu hata kama kina tija kwa taifa.
Na kama katika kuchukua upande huo unakuwa upande wa oppressors unageuka kuwa kituko zaidi kumlinganisha na yule anayechukua upande wa wanaokandamizwa. Hivi ni msomi wa aina gani anayeweza kushangilia kuona ukandamizwaji wa upinzani huku kukiwa na dalili ya kuleta political monopoly?
Hivi ni msomi wa aina gani asiyeweza kuogooa kuona nia ya CCM kutaka ibaki peke yake kwenye siasa za Tanzania?!
Nilitarajia vijana wadogo kama hawa wawe ndio chachu ya kupigania taifa kuliko kuwa sehemu ya kupigania chama.