Wasomali wateka meli ikileta mafuta Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomali wateka meli ikileta mafuta Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 7, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MAHARAMIA wa Kisomali wameiteka nyara meli ya mafuta karibu na Madagascar ikileta mafuta nchini na kuipeleka pwani ya Somalia, wamiliki wa meli hiyo wa Norway wameiambia Reuters.

  Meli hiyo yenye jina la UBT Ocean, ilikuwa na mafuta kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kwenda Tanzania, Svenn Pedersen, wa kampuni inayomiliki meli hiyo, Brovigtank, alisema.

  Uharamia umefanya eneo la bahari ya Hindi katika Pembe ya Afrika kuwa moja ya maeneo hatari zaidi duniani, licha ya kuwapo merikebu za majeshi ya kimataifa. Utekaji nyara huo huongezeka katika miezi ya Machi na Mei wakati ambao bahari huwa imetulia.

  Pedersen alisema juzi kuwa wamiliki wa meli hiyo walipokea simu kutoka kwa nahodha akisema maharamia wamewavamia melini. "Baada ya taarifa hiyo mara moja tukapoteza mawasiliano na meli," Pedersen aliiambia AFP.

  Meli hiyo ina usajili wa visiwa vya Marshall. Kutekwa nyara kwa meli hiyo kumetokea siku mbili tu baada ya maharamia kuiteka nyara meli nyingine ya mafuta ya Saudi Arabia na mabaharia wake katika Ghuba ya Aden na kuipeleka katika mji wa Garacad, Somalia.

  Majeshi ya wanamaji ya kimataifa yanafanya doria katika eneo hilo la Ghuba na Bahari ya Hindi, lakini bado yameshindwa kuzuia uharamia huo unaofanywa na Wasomali.

  Wiki moja iliyopita, wanamaji wa Marekani walifanikiwa kuinusuru meli yenye bendera ya Tanzania dhidi ya kutekwa nyara na maharamia wa Kisomali.

  Helkopta SH-60B Seahawk kutoka manowari ya Jeshi hilo, USS Farragut, ilishambulia mashua iliyokuwa ikitumiwa na maharamia hao na kuweza kukamata wanane.

  Kwa mujibu wa Ubalozi wa Marekani nchini, meli hiyo mv Barakaale 1, ilishambuliwa mara mbili na maharamia kabla ya timu ya wanajeshi hao kuwasili eneo la tukio. Somalia haina serikali imara tangu mwaka 1991.
   
 2. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Source??
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hivi kwanini nchi zetu hazitumi majeshi kuzibiti hawa wajinga? nimechoka kusikia hizi habari kila siku kwnai inaonesha nchi nyingi hazijali kuhusu hawa waharamia.
   
 4. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Navy ta Tanzania iko wapi?
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mpaka bei ya mafuta ipande
  ndo utasikia watu kuamka...
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani Tanzania na nchi zingine zinazofaidiaka na bahari ya Hindi zifanye mkakati wa makusudi kufundisha jeshi la wasomali wenyewe ili waweze kuifanya somalia kuwa na serikali yake imara. Kama kila nchi itafundisha wanajeshi sema kama 50,000 tu kwa miaka 2 kwa nchi kama tano au kumi unadhani somalia itakuwa na jeshi kubwa kiasi gani? Na ndipo watakapoweza kushinda vita dhidi ya maharamia. Kuleta meli na manowari za kivita za marekani na nchi za kimagharibi sio jawabu la kudumu.

  Bernad Membe hii ndio point ya kukupa ujiko peleka hiyo proposal kwenye jumuiya ya kimataifa kuwa mnataka kutrain wasomali ili waweze kulinda serikali yao na pwani ya nchi yao, alafu uzishawishi nchi nyingine kufanya hivyo hivyo na zile tajiri kuchangia bajeti na vifaa.
   
 7. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  huko Nyuma niliwahi kusema hivi: Ilikuwa 4th December 2009, na leo bado naona nilikuwa na point, na nasimamia kwenye hii hoja.

  Sina uhakika kama hii thread niianzishe kwenye jukwaa la habari za kimataifa au hapa.
  Kama tunavyojua kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwenye suala la ukombozi wa bara la Afrika. Tumesaidia kukomesha ukoloni, kutawaliwa na ubaguzi wa rangi kwa nchi zilizoko kusini mwa bara la afrika. Pia tumewasaidia Polisalio, tumesaidia Uganda, na nchi zote za ukanda wa maziwa makuu kutatua migogoro yao (ingawa hili la kuwauzia siraha tena, mmh! linatia doa). Tumepeleka majeshi yetu kulinda amani kwenye nchi zenye matatizo ya migogoro ya wenyewe kwa wenyewe. Bila kusahau operation ya JWTZ hivi karibuni huko Anjouan.


  Lakini pamoja na yote hayo sasa hivi kuna tishio kubwa tishio jipya, tishio linalohatarisha sio usalama wa majirani zetu lakini ni tishio linaloweza kuua biashara na mahusiano yetu na dunia nyingine. Tatizo linalofanya kuwe na makonteina yanayopita ndani ya aridhi yetu kama yana mizigo kumbe ndani yamebeba watu wanaokimbia nchi yao.Tatizo hili ni tatizo katika ghuba ya Aden, iliyoko kwenye pembe ya Afrika. Naliona ni tatizo kutokana kuongezeka kwa vitendo vya utekaji nyara wa meli zinazotoka au kuja pwani ya afrika mashariki.

  Kitendo cha maharamia wa kisomali kuendelea kupata malipo kutokana ana utekaji nyara wa meli hizo na raia wa kigeni hakitaisha leo wala kesho kama hatua za makusudi hazitachukuliwa. Maharamia wanajua kabisa kuwa hawawezi kukamatwa wala kushindwa kutoka na miundo mbinu yao waliyojiwekea ndani ya Somalia.

  Lakini nadhani, kama Tanzania ikiamua, Kama Tanzania itadhamiria kweli uwezekano wa kumaliza tatizo la Somalia upo na unatekelezeka.

  Kama ningekuwa waziri wa ulinzi wa JMT leo hii ningemshauri amiri jeshi mkuu, JK, kuanza operation maalumu ya kuisaidia Somalia. Kuisaidia Somalia kuwa na serikali yake imara yenye nguvu na jeshi imara lenye adabu na utiikwa serikali yao.

  Ningemshauri Tanzania ianzishe kambi maalumu za mafuzo kwa vijana wa kisomali ambao watakuwa tayari kulitumikia jeshi jipya la nchi yao. Vijana hawa wawe recruited na kupigwa msasa kabambe ndani ya aridhi ya Tanzania, wapewe mafunzo ya kijeshi na kinadharia ya kuipenda nchi yao na kujua umuhimu wa kuwa na serikali yenye nguvu.

  Kama tunaweza kufanikiwa kuzishawishi na nchi zingine kama South Afrika, Msumbiji, Zambia nk kila nchi ikazalisha wanajeshi wa kisomali sema kwa miaka mitatu mfululizo, kama kila mwaka tunatengeneza asikari 50,000 na nchi zingine zikafanya hivyo, ningekuwa na uhakika kuwa ifikapo mwaka 2015 hakuna tatizo la utekeji nyara meli na watu wasio hatia pwani ya Somalia.

  Naamini nchi zilizoendelea zipo tayari kutoa michango na misaada kutaka kusaidia kuhakikisha kuwa Somalia inatawalika, kwani nazo zimechoka kuendelea kutengeneza vichwa vya habari kwenye media kutokana na watu wao kila siku kutishiwa kukatwa vichwa na magaidi wa kisomalia. Obama angefurahi sana mpango huo kwani ungemsaidia kuibomoa ngome mpya ya Al Qaeda inayodaiwa kuanza kujengwa kwenye nchi isiyo na serikali wala jeshi, angetoa support. Na Tanzania ingepata kujenga uhusiano wake na marafiki zake wa nje kwa ukaribu zaidi. Tanzania inaweza, nia na sababu tunazo, tuwasaidie wasomalia jamani!!!!
   
 8. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  Elizabeth Gupta - BBA Revolution, Mwaka huu ni wetu pia

  mzee badili hii signature imepitwa na wakati
   
 9. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwa kweli hawa wasomali ni noma sana,sielewi kwa nini hawasambaratishwi!
   
 10. T

  Tall JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  point
   
 11. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mkuu hii signature mbona bado inalipa, mbona bado inaenda na muda, mpaka tutakapokuwa na BBA V na kuona mwakilisha mwingine ndio itabadirika. Hii signature inategemeana unaiangalia kutoka kona gani, kwa mfano kama unamuuganisha Elizabeth baada ya Richard ilikuwa inaamaanisha ni mwaka wetu mwingine wa mafanikio kwenye BBA, kama unaunganisha Elizabeth na kuboronga kwa Latoya basi utakuwa unasema huu ni mwaka wetu wa aibu. Kwa hiyo mafanikio au aibu tutaendelea kuibeba mpaka BBA nyingine itakapoanza. Kama kulia lia n.k Nadhani umenielewa mkuu, turudi kwa wasomali
   
Loading...