Wasiwasi wangu ni Pemba kujitenga ikiwa CUF wataporwa ushindi

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
32,995
60,485
..nina wasiwasi sana na kinachoendelea sasa hivi Zanzibar.

..zipo taarifa za kuaminika kwamba CCM hawajawahi kushinda nafasi ya Uraisi Znz tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

..wengine tayari tulikuwa watu wazima wakati wa uchaguzi mkuu wa 1995. ninakumbuka hali ya uhasama na uadui iliyotokea Unguja na Pemba baada ya CCM kupora uchaguzi wa Znz.

..yako maandamano ya wana-CUF ambayo yaliyozimwa kwa nguvu za kijeshi na kupelekea wananchi kupoteza maisha na wengine kukimbia na kwenda kuishi ukimbizini.

..CUF ni chama ambacho kimejikita zaidi Pemba, wakati CCM imejikita zaidi Unguja. Tunaposhindwa kutoa haki ktk uchaguzi mazingira yaliyoko Zanzibar tunakaribisha sentiments kwa upande unaoona umeonewa.

..Kwa mtizamo wangu suala la uchaguzi wa Znz si la kuchezewa-chezewa kama ambavyo CCM wanajaribu kufanya. Suala hili linagusa usalama wa nchi yetu, na linatishia uwepo wa Tanzania kama Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar[Unguja na Pemba].

..Nina wasiwasi hali inaweza kuwa mbaya kuliko ilivyokuwa miaka ya 90 na hata kuamsha hisia za Pemba kutaka kujitawala wao wenyewe.
 
Please leaders sort things out in right way, otherwise the nation as a whole can be in total chaos. If there is no peace in the Islands same will be in the Mainland, and this is for sure.
 
Mada kama hizi katika nchi hii zinabatizwa jina la kinafikii kuwa ni mada/habari za "uchochezi"!!
Mara nyingi ukweli ni kama shindano ambayo imeshikwa na mtu na unaona kabisa anataka kukuchoma jichoni kwahiyo salary slip tulia utalipwa tu kuliko kutetea unyang'anyi
 
Mada kama hizi katika nchi hii zinabatizwa jina la kinafikii kuwa ni mada/habari za "uchochezi"!!

..hata mimi nimefikiria sana kabla ya ku-post mada hii.

..unajua ukifuatilia historia ya ZNZ utaona kwamba hata ASP walikuwa wanafanyiwa hivihivi wanavyofanyiwa CUF na matokeo yake ni yale MAPINDUZI.

..fast forward to 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, unafikiri hawa CUF watachukua hatua gani ikiwa kila ukifanyika uchaguzi wanaporwa ushindi?

..Kuna ulazima gani kwa CCM kulazimisha ushindi wakati kuna serikali ya umoja wa kitaifa?
 
hii inaweza kuwa plan b , lakini mimi siikubali , cuf isithubutu kuitelekeza unguja , kwa utafiti wangu inakubalika kwa zaidi ya 60% pale , kiukweli hakuna ccm unguja na pemba .
 
sio unguja tu, tz nzima ccm inalazimishaa, ipo siku kila kanda itadai uhuru wake
 
..nina wasiwasi sana na kinachoendelea sasa hivi Zanzibar.

..zipo taarifa za kuaminika kwamba CCM hawajawahi kushinda nafasi ya Uraisi Znz tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

..wengine tayari tulikuwa watu wazima wakati wa uchaguzi mkuu wa 1995. ninakumbuka hali ya uhasama na uadui iliyotokea Unguja na Pemba baada ya CCM kupora uchaguzi wa Znz.

..yako maandamano ya wana-CUF ambayo yaliyozimwa kwa nguvu za kijeshi na kupelekea wananchi kupoteza maisha na wengine kukimbia na kwenda kuishi ukimbizini.

..CUF ni chama ambacho kimejikita zaidi Pemba, wakati CCM imejikita zaidi Unguja. Tunaposhindwa kutoa haki ktk uchaguzi mazingira yaliyoko Zanzibar tunakaribisha sentiments kwa upande unaoona umeonewa.

..Kwa mtizamo wangu suala la uchaguzi wa Znz si la kuchezewa-chezewa kama ambavyo CCM wanajaribu kufanya. Suala hili linagusa usalama wa nchi yetu, na linatishia uwepo wa Tanzania kama Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar[Unguja na Pemba].

..Nina wasiwasi hali inaweza kuwa mbaya kuliko ilivyokuwa miaka ya 90 na hata kuamsha hisia za Pemba kutaka kujitawala wao wenyewe.
wapemba walioko bara hawataki kusikia biashara hiyo. wameshawekeza bera mamilioni kwa mamilioni. wana magorofa ya biashara pale kariakoo alafu uwaambie wajitenge kwenda wapi?? na wameshatoa tamko kwamba kama Seif anataka kuanzisha nchi yake aende akatafute kwingine na sio pemba
 
Tatizo liko kwenu nyinyi wezentu kutoka Tanganyika, sio wote, Lakini wengi wenu munabishana kitoto.
Utakuta mtu na Elimu yake pengine ni Professor anasema hayo ni mambo ya ndani ya Zanzibar na watayamaliza Kinzanzibari.
Tuseme leo Wazanzibari Wafungue Kesi ya Kimataifa washinde na waje UN wawatangazi uhuru wao . Sio haohao wataosema hayo ni mambo ya ndani ya Tanzania?
Hivi sasa mwache magufuli aseme hayamuhusu, yatakumuhusu wakati tutapopiga referendom ya kujitenga lakini itakuwa too late.
 
Zanzibar toka enzi za Mohamed Abdulrahman Babu na Kassim Hanga haki haijawahi kutendeka, kuna watu wachache wanajiona miungu watu, wenye kutoa maamuzi yao binafsi kwa maslahi ya Zanzibar.
 
Suluhu la Zanzibar waingie mkataba tu, wawe wanapokezana miaka mitano mitano.

CUF ya Pemba miaka mitano CCM ya Unguja miaka mitano.
 
Mada kama hizi katika nchi hii zinabatizwa jina la kinafikii kuwa ni mada/habari za "uchochezi"!!

Uko sahihi mkuu, nina mashaka kama mods wataruhusu uzi huu ili ukweli uendelee kujadiliwa hapa. Hili neno "uchochezi" linatumiwa vibaya na watawala kukandamiza na kuzika "ukweli", ila ukweli daima lazima usemwe kwa nguvu zote! Na kwa hoja mujarab kama hizi.
 
Suluhu la Zanzibar waingie mkataba tu, wawe wanapokezana miaka mitano mitano.

CUF ya Pemba miaka mitano CCM ya Unguja miaka mitano.

Mi nauliza tu hivi Dr. Shein si naye ni wa Pemba mbona wanamtosa huko kulikoni ??????????!!
 
..nina wasiwasi sana na kinachoendelea sasa hivi Zanzibar.

..zipo taarifa za kuaminika kwamba CCM hawajawahi kushinda nafasi ya Uraisi Znz tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

..wengine tayari tulikuwa watu wazima wakati wa uchaguzi mkuu wa 1995. ninakumbuka hali ya uhasama na uadui iliyotokea Unguja na Pemba baada ya CCM kupora uchaguzi wa Znz.

..yako maandamano ya wana-CUF ambayo yaliyozimwa kwa nguvu za kijeshi na kupelekea wananchi kupoteza maisha na wengine kukimbia na kwenda kuishi ukimbizini.

..CUF ni chama ambacho kimejikita zaidi Pemba, wakati CCM imejikita zaidi Unguja. Tunaposhindwa kutoa haki ktk uchaguzi mazingira yaliyoko Zanzibar tunakaribisha sentiments kwa upande unaoona umeonewa.

..Kwa mtizamo wangu suala la uchaguzi wa Znz si la kuchezewa-chezewa kama ambavyo CCM wanajaribu kufanya. Suala hili linagusa usalama wa nchi yetu, na linatishia uwepo wa Tanzania kama Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar[Unguja na Pemba].

..Nina wasiwasi hali inaweza kuwa mbaya kuliko ilivyokuwa miaka ya 90 na hata kuamsha hisia za Pemba kutaka kujitawala wao wenyewe.
Kila mtu analalama tu na vitisho.subirini marudio
 
Zanzibar toka enzi za Mohamed Abdulrahman Babu na Kassim Hanga haki haijawahi kutendeka, kuna watu wachache wanajiona miungu watu, wenye kutoa maamuzi yao binafsi kwa maslahi ya Zanzibar.

..kabla ya Karume Snr wako waliojiona miungu watu.

..alipoingia Karume Snr naye akatawala kama mungu mtu.

..tatizo letu wa-Tgk ni kwamba tumewezesha utawala wa kimungu mtu Znz kwa miongo kadhaa sasa.

..mimi nadhani wa-Tanganyika tuna nafasi ya kusahihisha makosa yetu. Tusiwaache wa-Znz peke yao wakaumizana.
 
Wewe mnafiki wapemba hawajawahi kumwambia seif maneno hayo .acha kuwasemea wapemba
 
Back
Top Bottom