Wasiwasi wa polio wazuka nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasiwasi wa polio wazuka nchini

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 1, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  KUNA wasiwasi mkubwa wa kuibuka kwa ugonjwa wa polio, ambao husababisha kupooza, baada ya ugonjwa huo kugundulika kwenye nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, serikali imeeleza.

  Ugonjwa huo, ambao huambukiza na pia hushambulia uti wa mgongo, umegundulika kwenye Wilaya ya Kalemie nchini Congo na serikali imewataka wanachi wa mikoa ya Kigoma na Rukwa kutoa inayopakana na taifa hilo taarifa sahihi pindi wanapoona watu wenye dalili za ugonjwa huo.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa ugonjwa huo, ambao husababisha kupooza, ulibainika nchini Congo Agosti 7.
  "Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilichukuwa hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini," alisema Nyoni.
  Alisema moja ya hatua mabazo serikali imezichukua ni pamoja na kuwapatia watoto wenye umri chini ya miaka mitano chanzo ya ugonjwa huo.

  Hata hivyo, katibu huyo alifafanua kuwa chanjo za ugonjwa huo zitatolewa kuanzia Oktoba 4 hadi 7 kwenye mikoa hiyo miwili.
  "Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuhamasisha viongozi wa ngazi zote juu ya suala hili; kutoa chanjo ya polio kwa watoto wote walio na umri chini ya miaka mitano kwa njia ya kampeni; kuimarisha utoaji wa taarifa za wagonjwa waliopata ulemavu wa ghafla na kuimarisha utoaji wa chanjo za kawaida," alisema Nyoni.

  Alisema chanjo ya polio itatolewa na watoa huduma za afya waliopata mafunzo ambao watapita nyumba hadi nyumba na kwamba wanaomba ushirikiano wa wananchi katika kutekeleza kampeni hiyo.
  "Chanjo hii itatolewa kwa njia ya matone kinywani kwa watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano bila kujali kama alipata chanjo au hajapata," aliongeza.

  Alisema watoto wote watakaopata chanjo wakati wa kampeni hiyo watawekewa alama kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto kwa kutumia wino maalum ili kusaidia ufuatiliaji na uhakiki idadi yao.

  Chanzo: Wasiwasi wa polio wazuka nchini

  huo ndio mwanzo wa kuzuka huo ugonjwa wa Polio tusipokuwa waangalifu kutatokea maradhi mengi tena ya ajabu ajabu, tuwe waangalifu sana kukabiliana na maradhi na tuwe wasafi siku zote maradhi hayata kuwepo.
   
Loading...