Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
Wassira achukizwa Dk Slaa
Wednesday, 16 March 2011 20:02
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Steven Wassira
Sosthenes NyoniWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Steven Wassira, amemtaka Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willibrod Slaa, kutumia elimu yake ya udaktari kuzungumza mambo ya kitaalamu badala ya kutaka kusikika.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum na Kituo cha televisheni ya ITV juzi, Wassira alisema kinachofanywa na Dk Slaa ni kutaka kusikika.
"Kitendo cha Dk Slaa kupita jimboni kwangu Bunda na kuwaambia wananchi kwamba mimi sifai kwa kuwa nimewasababishia njaa, kinaonyesha jinsi anavyoshindwa kutumia taaluma yake kujenga hoja za msingi," alisema Wassira.
Kwa mujibu wa Wassira, Dk Slaa aliwaeleza wananchi hao kuwa amewaletea njaa licha ya kwamba alikuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Umwagiliaji."Simwelewi Dk Slaa, siasa sio kuzungumza zungumza tu hata kama huna hoja za msingi.
Kwanza yeye ni daktari halafu ni mtu mzima, anawaambia wananchi wangu kule Bunda kwamba mimi nimeleta njaa," alisema Wassira na kuhoji:"Amefanya utafiti akabaini njaa ya Bunda sababu ni mimi?
Sasa kuna Jumanne Magembe na Mwanga kuna ukame, je yeye ndio kasababisha?Wassira alisema akiwa waziri mwenye dhamana ya kuwatumia Watanzania wote, asingeweza kuchukua raslimali za sehemu nyingine na kuzipeleka Bunda kama Dk Slaa anavyotaka, isipokuwa maendeleo ya Bunda yatapatikana kwa jitihada za pamoja kati yake na wakazi wa jimbo hilo."Yeye anafikiri ukiwa waziri basi unaweza kufanya chochote.
Maendeleo ya jimbo yanapatikana kwa mipango na ushirikiano kati ya mbunge na wakazi wa jimbo husika. Huwezi kuchukua rasilimali za sehemu nyingine ya nchi na kuzipeleka kwenu, eti ukawafurahishe wananchi wakati umebeba dhamana ya Watanzania wote," alisema Wassira.
Pia, Wassira aliwataka viongozi wa Chadema kuacha sera za kuhamasisha wananchi kuondoa madarakani serikali iliyopo kwa njia ya maandamano.
Alisema sio sahihi kulinganisha mfumo wa siasa ya Tanzania na nchi kama Misri au Libya kwa sababu, hapa muda uliowekwa kikatiba kwa Rais kukaa madarakani ni miaka 10.Mwisho
SOURCE: Mwananchi