PreGE2025 Wasira apiga marufuku wajawazito kutozwa fedha

PreGE2025 Wasira apiga marufuku wajawazito kutozwa fedha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Bw. Stephen Wasira amewasili Mkoa wa Mbeya kwa ziara ya siku nne kuanzia Machi 17-20, huku akitoa maagizo mazito kwa halmashauri zote nchini kuacha mara moja kutoza fedha wanawake wajawazito wanaofika kwenye vituo vya afya kujifungua.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Bw. Wasira amelazimika kutoa maagizo hayo baada ya kufika eneo la mji mdogo Mlowo, Mkoa wa Songwe na kupata wasaa wa kusikiliza kero, ndipo mmoja wa wananchi akajitokeza kulalamikia gharama kubwa aliyotozwa alipofika kituo cha afya kujifungua.

 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepiga marufuku wajawazito wanaokwenda kujifungua hospitalini kutozwa fedha, kwani huduma ya kujifungua ni bure na maelekezo tayari yalishatolewa.

Akizungumza mbele ya wananchi wa Mlowo, katika Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, akiwa katika ziara yake ya kikazi, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Stephen Wasira, amesema sera ya CCM inaeleza wazi kuwa huduma ya kujifungua pamoja na watoto wenye umri kuanzia mwaka 0-5 hawatatozwa fedha, hivyo ni marufuku kuwatoza fedha.

Akiwa katika eneo hilo, Wasira alipokea malalamiko ya wananchi hao, wakidai kwamba wanawake wajawazito wanapokwenda kujifungua wanatakiwa kulipa Sh. 300,000 ili kupata huduma ya kujifungua.

Hali hii ilimshangaza na akaagiza kupiga marufuku kutozwa fedha kwa huduma ya kujifungua.

Chanzo: Global TV
 
Majizi ya Ccm hayana akili , unakataa watu kutozwa fedha wakati mgonjwa akifika kituo cha Afya anakuta hamna gloves wala dawa bila mtu kujiongeza anapoteza maisha
 
Bw. Wasira amelazimika kutoa maagizo hayo baada ya kufika eneo la mji mdogo Mlowo, Mkoa wa Songwe na kupata wasaa wa kusikiliza kero, ndipo mmoja wa wananchi akajitokeza kulalamikia gharama kubwa aliyotozwa alipofika kituo cha afya kujifungua.
Chalamila anasemaje
 
Tyson anajua hali halisi ilivyo huko mahospitalini au anajiropokea tu? Siyo yale yale ya elimu bure halafu mamichango kibao tena ya lazima huko mashuleni?

Hii ni kauli ya kisiasa tu isiyo na maana yo yote katika uhalisia. Huu ni mwaka wa uchaguzi! 🚮
 
Na kuna wapumbavu wataaamini hii..

Ukienda hospitali kujifungua au kliniki, hautozwi kile kitendo cha kumtoa mtoto tumboni. Hiyo ni bure.

Utakavyotozwa ni gharama za vipimo, kitanda nk.

Ukizaa leo kisha kesho ukaruhusiwa, hapo gharama inakuwa ndogo tu.

Ila ukizaa kisha ukapata complications zitakazokuweka muda mrefu, tegemea bill ije ndeefu! Hapo mambo ya "Kujifungua ni bure" hayaingii tena.
 
Hapa zahanati ninapofanya kazi tu tunawatoza..
Aje atukamate
 
Back
Top Bottom