GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,648
- 10,843
Unaposema wasiojulikana, ni muhimu kuweka maelezo sawa kuwa wasiojulikana kwa nani!
Hawawezi kuwa wasiojulikana kwa waliowatuma!
Hawawezi kuwa wasiojulikana kwa vyombo vya dola! Vinginevyo, tungeamini kuwa tuna vyombo vya dola vya hovyo kupitia kiasi. Vyombo vya dola vinawajua lakini havina la kuwafanya zaidi ya kuwasaidia pale wanapohitaji support yao!
Iweje waitwe wasiojulikana ilhali wanatumia mpaka miundo mbinu ya umma kutelekeleza uharamia wao?
Iweje waitwe wasiojulikana wakati ni wazi kabisa kuwa Polisi wanajitahidi kujiepusha nao?
Wasiojulikana kivipi wakati si majambazi? Wakiteka hawahangaika na mali za mtekwaji, bali maisha yake na hali yake tu! Wasiojulikana wanapata wapi hela ikiwa hawahangaika na mali za mtu wanayemteka?
Hawawezi kuwa vibaka, vinginevyo wasingehangaika na watu wa aina fulani pekee!
Siyo kweli kuwa ni wasiojulikana! Wanajulikana kwa kuwa ni "maprofessional" katili walioandaliwa na "watu" fulani kwa malengo yao haramu! Watu pekee wasisowajua ni ambao waliowaandaa "wasiojulikana" walipanga wasijue, ingawa wengi wameshajua!
Vipi wale waliomteka Sativa, walishajibu tuhuma zilizoelekezwa kwao? Au ndiyo vyeo vimeendelea kupanda?