Wasio na vitambulisho wala namba za NIDA.....

Wasio na vitambulisho wala namba za NIDA.....

Mu7

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2013
Posts
1,655
Reaction score
2,003
Wadau, nina hakika kati ya wananchi milioni hizo zote za watanzania, haikosi wapo ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya NIDA, na hivyo hawana vitambulisho hivyo wala namba ya NIDA. Je, kuna option gani kwa ajili ya watu hawa kuhusu hatima ya line zao za simu?
 
mimi mmojawapo.... muda wa kupanga foleni sina kabisa...


kitambulisho cha kura, passport na my d. licence vilikuwa vinafit kila sehemu
 
Labda umefanya makusudi ya kutokutaka kitambulisho,maana Kila Wilaya sasa hivi zoezi la kuandikisha linafanyika na ukienda pale unajaza form na kuikamilisha hiyo form ndio unapewa namba ya Nida.
Maana namba inatolewa kabla Kitambulisho
 
Tanzania mambo mengi wanakurupuka sana wengi hatujapata vitambulisho badala walimalize kwanza hili wamekuja na lingine.
 
Nimeona voda wanapokea hata kitambulisho cha kura, passport, leseni
Wadau, nina hakika kati ya wananchi milioni hizo zote za watanzania, haikosi wapo ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya NIDA, na hivyo hawana vitambulisho hivyo wala namba ya NIDA. Je, kuna option gani kwa ajili ya watu hawa kuhusu hatima ya line zao za simu?
 
Kuna kitu hapa lazima tuombe rais wetu wa wanyonge atusaidie
 
Labda umefanya makusudi ya kutokutaka kitambulisho,maana Kila Wilaya sasa hivi zoezi la kuandikisha linafanyika na ukienda pale unajaza form na kuikamilisha hiyo form ndio unapewa namba ya Nida.
Maana namba inatolewa kabla Kitambulisho
Una mana hata leo mtu akienda wilayani hiyo huduma ya kuandikishwa anaipata?
 
Asilimia 90 ya wale tuliojiandikisha kwenye kituo chetu hatujapata kitambulisho cha NIDA. Tena usisahau:- Ripoti ya CAG ilisema kati ya milioni 19 waliojiandikisha ni vitambulisho milioni ni NNE TU vilitolewa. Sasa itakuwaje? Halafu bibi zetu kule kijijini tuliowanunulia simu ili tuwe tunawatumia mpesa, tigopesa n.k. hawataweza kutoka huko kijijini kwenda mjini kujiandikisha. Je, NIDA wataweka mashine kwenye vijiji?
 
Back
Top Bottom