Wasikutishe, hakuna wa kukulaani

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Na. Robert Heriel.

Huu nao ni Utumwa niliouona chini ya jua. Mtu kujitaabisha kwa ajili ya wengine. Akiwaogopa na kuwalamba viatu vyao ili apate baraka.

Nami nikasema, mambo haya ni mabaya. Nayo hayafurahishi. Tena ni mateso makubwa kwa wale wageuzwao watumwa na Wanadamu wengine. Basi nakuandikia mambo haya ili usijekuwa mtumwa kama wale waliowengi.

Hakuna awezaye kukulaani chini ya Jua. Sio Mama yako aliyekuzaa wala Baba yako aliyekuzaa. Sio Mama yako mlezi wala Baba yako mlezi. Tena sio walezi wako na Waalimu wako.

Sio Mchungaji wa kanisa lako wala sio Sheikh wa Msikiti unaoenda kufanya Ibada. Hakuna anayeweza kukulaani chini ya Jua.

Wapo Watu huwatisha watu wengine kuwa watawalaani. Wapo Wazazi na Walezi ambao huwatisha watoto wao kuwa watawalaani. Na watoto kwa ujinga wao wa ukosefu wa elimu ya Mungu wanajikuta wakiingia katika utumwa kwa Wazazi wao waliowazaa.

Wapo Wachungaji na Mashekhe huwatisha na kuwasomea visomo vya kipumbavu watu ili kuwatisha watu. Huwageuza waumini mateka na Watumwa hapa duniani.

Hata Shuleni walikuwepo Waalimu wapuuzi waliokuwa wakiwatisha Wanafunzi kuwa watafeli maisha. Walikuwa wakiwalaani lengo. Ili kuwafanya wanafunzi wao Watumwa na mateka.

Kwa kawaida watu wanaotoa toa laana au kuwahukumu wengine washindwe kwenye maisha. Huwa na tabia zifuatazo:

Mosi, Huwa na tabia ya kulazimisha heshima hata katika mambo ya kipuuzi. Kwa mfano, Waalimu wengi hupenda kulazimisha makosa kwa wanafunzi hata kama mwanafunzi hajafanya. Na kama mwanafunzi atabisha huanza kumtolea maneno ya karaha. Pia Waalimu hawapendi kubishiwa hata kwa jambo ni la kweli. Huo ni upuuzi. Mimi nilikuwa ni mwanafunzi nimeyaona hayo. Na sasa ni Mwalimu nayaona hayo.

Hata Wazazi nao kuna wakati hupenda kulazimisha heshima hata kwa mambo ya kipuuzi. Na kama mtoto hutofanya hivyo basi huanza kukutisha na kukulaani.

Pili, Hupenda kugeuza watu Mateka na Watumwa. Hupenda kunyenyekewa kama miungu watu. Hapa Wapo Wachungaji na Mashekhe. Wapo viongozi wa dini, wapo Pia wazazi. Ili umgeuze mtu mateka lazima umuogopeshe kwa Maneno ya vitisho na laana. Kwa mfano, Kuna wapuuzi wengi husema viongozi wa dini hawapaswi kunyoshewa vidole. Hawapaswi kuonywa kisa wao ni watumishi wa Mungu. Waulizeni swali, nani sio mtumishi wa Mungu.

Ukiwanyoshea kidole wanajitia kukutisha na laana kibao. Ukitaka usinyoshewe kidole fanya mapenzi ya Mungu. Sio kwa vile wewe ni mchungaji sijui sheikh. Sijui unajiita nabii ati ndio usiambiwe makosa yako unapoboronga. Lazima watu wajue kuwa ni laana kumnyooshea kidole mtu atendaye mema na haki ya Mungu. lakini sio kisa mchungaji, sijui Sheikh, sijui Mzazi na nani huko. Fanya Mema hakuna atakayekunyooshea kidole.

Narudia Mama hawezi akakulaani. Baba yako hawezi kukulaani. Wala mtu yeyote kamwe hawezi kukulaani.

Kinyume chake ni kuwa kama hakuna anayeweza kukulaani basi hakuna anayeweza kukubariki.

Wewe ndiye unaweza kujilaani au kujibariki. Wewe ndiye utabeba msalaba wako mwenyewe. Wewe ndiye unaamua ujilaani au ujibariki.

Nimesikia na kuona wala sijahadithiwa. Kuna watu wamejigeuza watumwa kwa ujinga wao. Ati Mama au Baba anakuambia njoo nikubariki au usipokuja nitakulaani. Huo ni upuuzi mkubwa sana.

Nimeona makundi kwa makundi wakienda kwa Wachungaji na masharifu kupokea maji ya baraka sijui upako. Huo ni upuuzi mkubwa na kujigeuza mwendawazimu. Hata mbuzi hawezi kufikiri kwa kiwango hicho. Ni dalili ya ukichaa.

Na ndipo hapo wajanja wanaojifanya Wachungaji hujipatia pesa kwa ulaghai wao wa kuuza maji sijui ya baraka. Sijui upako. Kuuza maji kanisani au msikitini sio dhambi. Dhambi ni kuwadanganya watu. Kwani mlishindwa kusema maji haya ni ya kanisa, tunaomba waumini mnunue maji ya Kanisa au msikiti uweze kupata faida kupitia maji. Lakini mnawalagahi watu kwa ujinga wao na udhalimu wenu.

Kama ulikuwa hujui Mtu anajilaani mwenyewe na kujibariki mwenyewe. Unapotenda haki unajibariki. Unapotenda dhuluma unajilaani.

Haki ni ipi sasa. Haki ni kufanya inayokupasa kulingana na mapenzi ya Mungu ambayo ni kanuni za asili. Kwa mfano ishi kwa upendo na watu wengine. Wape sitahaki watu kwa jinsi inavyowafaa.

Hunalaaniwi kwa maneno ya watu kama vile Wazazi wako, Waalimu wako, Viongozi wako wa dini. miongoni mwa watu wengine wanaojifanya wao ndio vihere here wakijipa mamlaka ya kutoa laana na baraka.

Laana inatokana na matendo yako. Kipi unafanya na kipi unasema.

Mtu anayedhani kuwa kuna mtu anaweza mlaani au kumbariki ni mtu asiyejitambua vyema. Ni mtumwa na mateka wa watu wengine.

Hakuna aliyepewa Mamlaka ya kulaani wala kubariki hapa duniani. Wanaojipa madaraka hayo ni kwa mapenzi yao wenyewe na upungufu wa kibinadamu. Upendeleo wao kwa watu wanaowapenda na chuki zao kwa wanaowachukia.

Mungu aliwapa Wazaz na makundi mengine mamlaka ya kufundisha kizazi kingine sheria na amri za Mungu. Jukumu la kufuata hizo sheria na amri za Mungu ni lao wenyewe. Wakitaka baraka watafuata amri za Mungu. Wakitaka laana na mikosi hawatafuata amri na sheria za Mungu.

Mungu amewapa watu namna ya kuyachagua maisha yao. Sio wengine wakuchagulie maisha. Ati kisa ni mchungaji anaweza kukubariki au kukulaani. Yaani kukuchagulia maisha.

Hakuna mtu anayeweza kukulaani asilani. Matokeo ya maisha yako ni wewe mwenyewe. Umasikini wako ni wewe mwenyewe uliousababisha kwa asimilia tisini. Magonjwa na Mikosi mingine wewe ndio chanzo cha yote hayo.

Acha kusingizia wengine na kulaumu wengi. Wewe ndio chanzo cha kuboronga.

Lakini pamoja na kuwa unaweza kuwa umeboronga lakini Mungu ni wa rehema na mwingi wa huruma. Ukimrudia na kumuomba toba atakusamehe. Huenda kwa sasa ni masikini kutokana na uvivu na uzembe. Kutokana na matumizi mabaya ya fedha. Kutokana na kukosa vipaumbele. Basi unaweza kubadilisha mfumo wa maisha kwa kufanya kuacha uvivu na uzembe. Kuwa makini na matumizi yako ya Fedha. Hiyo ndio Toba. Sio uende kanisani kuombewa au kwa waganga wa kienyeji kupoteza muda. Hao hawana watakachokusaidia zaidi ya kukupotezea muda wako.

Toba ya kweli sio kwenda kusali misikitini au Makanisani. Toba ya kweli ni kubadili mfumo wa maisha yako kwa kuamua kutoka ndani. Kuacha umalaya usije pata Ukimwi, Kuacha kuhonga au kunywa pombe kupita kiasi usijekuishia kuwa masikini na kupata magonjwa ya kisukari na ugonjwa wa ini.

Matendo yako ndio yanageuka laana na baraka kwenye maisha yako. Hakuna anayeweza kukulaani.

Wapo waalimu waliowalaani wanafunzi wakiwaambia watafeli mitihani yao na kufeli maisha lakini wanafunzi hao baadhi yao walifaulu na wanapeta kwenye maisha. Wapo wanafunzi waliokuwa wakibarikiwa na waalimu kwa tabia hao ya uoga uoga na unafiki. Wakaambiwa watafika mbali lakini baadhi yao wamefeli pakubwa shuleni na maisha.

Wapo watoto watiifu na wanafiki kwa Wazazi wao. Kila kitu wanawatii wazazi wao hata kama ni kibaya na kinadhuru. Wazazi wao huwasemea mazuri lakini watoto hao hawana mbele wala nyuma. Wanahangaika kutwa kucha hawana wanachofanya cha maana japokuwa wao ni wa maana.

Lakini muda huo huo wapo watoto wasiotii kila kitu kwa wazazi wao. Hasa vitu vya kipuuzi puuzi. Wazazi huwatolea laana lakini watoto hao wanapeta. Wanafanakiwa tena zaidi na zaidi.

Baraka ni kufanya mambo yaliyomema na kusema yaliyomema.

Haiwezekani mzazi atake umnunulie pombe kali au sigara wakati amekatazwa hospitalini au wewe mwenyewe unajua Pombe ni mbaya alafu umnunulie mzazi wako kisa unaogopa atakupa laana. Hakuna laana ya hivyo hata siku moja. Watoto wengi wanaowaendekeza wazazi wao kwa mambo ya kipuuzi huishia kupata laana japokuwa wazazi wao waliwatamkia baraka.

Lakini watoto ambao hawakuwasapoti wazazi wao kwa mambo ya kipuuzi wakatamkiwa laana waliishia kupata baraka.

Huwezi muona mwalimu anatembea na rafiki yako wa kike alafu usimwambie aache upuuzi wake. Ati kisa ni mwalimu. Kisa kakuzidi umri. Kisa atakutamkia laana. Nimeona kwa macho yangu wala sijahadithiwa. Unakuta Mwalimu anawapenda wale wanafunzi wanaojua uovu wake. Marafiki wa yule anayetoka naye kimapenzi anawapa Ofa za hapa na pale. Anawatamkia baraka. Nakuhakikishia kama ulikuwa mwanafunzi uliyependezwa na upuuzi huo na hukuukemea iwe ni kwa rafiki yako au huyo mwalimu kwa kuogopa kuchukiwa na kupewa laana na waalimu. Hakuna utakapofika kutokana na matendo yako hayo labda uombe toba.

Nimalize kwa Kusema kuwa Mungu aliwapa watu uchaguzi wa maisha yao wenyewe. Hata Mungu hakuchahulii maisha. Hata Mungu hakulaani wala kukubariki.

Alishakupa mambo mawili ya kuchagua. Baraka na laana. Ukichagua baraka unabarikiwa. Tena inategemea utafanya jitihada gani kubarikiwa. Jinsi unavyofanya mambo mema ndivyo unavyozidi kubarikiwa. Ukijachugua laana unalaaniwa. Jinsi unavyofanya maovu ndivyo unavyojilaani.

Mtu kamwe hawezi kukulaani wala kukubariki. Yote yapo chini yako. Acha kuwa mateka na mtumwa wa watu wengine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
0693322300
 
Mzee mwanamke aliyekuzaa anakulaani yani usicheze nae kabisa ndio mtu pekee mwenye uwezo huo.
 
Sio mama yako tu hata mkeo anaweza kukulaani wanao hata familia achia mbali wazazi wako na mambo yooye yakaenda hovyo kabisa ili mradi wanacho kilalamikia kiwe cha kweli
 
"hakuna wa kuweza kukulaani,si mama yako mzazi wala baba yako mzazi".

mkuu acha kujitia ujinga.
 
Mtoa mada inaonekana wewe ni rais wa watu wenye viburi Duniani.

Nafahamu kuwa haya mambo ya laana hayana ukweli lakini walioanzisha na wanaotumia sasa wanafanya hivyo kwa nia njema tu hasa katika malezi.
Mbinu hii inasaidia sana kufanya watu kutotenda matendo ya kishenzi wakihofia laana.
Katika jamii kuna watu wana uwezo wa ufahamu wa mambo mkubwa, watu wa namna hii wanaweza kujiongoza katika maadili mema lakini kuna watu ambao uelewa wao wa mambo ni mdogo mtu kama huyo anahitaji vitu vya kumuongoza hasa vitu vya kumtia hofu ili akae kwenye mstari wa maadili.

Ukichunguza sana utagundua hata dini nazo ziko katika mtindo huu wa kutisha watu ili wawe na maadili mema. Ingawa walengwa hasa ni watu wenye uwezo mdogo wa kufahamu mambo ndiyo maana watu wengi wenye akili kubwa hawakuwahi kuamini haya mambo na kama waliamini ni kwa kinafki tu ili jamii isiwafikirie vibaya.
 
Anaweza kukulaani ila chanzo cha kukulaani ni yeye mwenyewe je ninani atabeba hiyo laana?
Kikawaida laana itakuwa juu ya mlaaniwa itatembea naye kizazi hadi kizazi.
.
KIIMANI
Mwanzo 12:3

3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
 
Kinachotokea ukimfanyia fyongo iliyopitiliza binadamu mwenzio ni kujilaumu na kuumia kwa moyo wako na hivyo huleta confrontation kwenye akili yako ndipo watu wanasemaga laana.Ila hakuna chemistry yoyote ya laana
 
Kulaani siyo Kama ulivyoelezea,ila nikukupa "trouble psychological".maana ukijijengea hisia kuwa fulani alinilaani kuwa nitafeli maisha jua kuwa utaishi hiyo Hali maana tiyari utakuwa umejengeka.
Na. Robert Heriel.

Huu nao ni Utumwa niliouona chini ya jua. Mtu kujitaabisha kwa ajili ya wengine. Akiwaogopa na kuwalamba viatu vyao ili apate baraka.

Nami nikasema, mambo haya ni mabaya. Nayo hayafurahishi. Tena ni mateso makubwa kwa wale wageuzwao watumwa na Wanadamu wengine. Basi nakuandikia mambo haya ili usijekuwa mtumwa kama wale waliowengi.

Hakuna awezaye kukulaani chini ya Jua. Sio Mama yako aliyekuzaa wala Baba yako aliyekuzaa. Sio Mama yako mlezi wala Baba yako mlezi. Tena sio walezi wako na Waalimu wako.

Sio Mchungaji wa kanisa lako wala sio Sheikh wa Msikiti unaoenda kufanya Ibada. Hakuna anayeweza kukulaani chini ya Jua.

Wapo Watu huwatisha watu wengine kuwa watawalaani. Wapo Wazazi na Walezi ambao huwatisha watoto wao kuwa watawalaani. Na watoto kwa ujinga wao wa ukosefu wa elimu ya Mungu wanajikuta wakiingia katika utumwa kwa Wazazi wao waliowazaa.

Wapo Wachungaji na Mashekhe huwatisha na kuwasomea visomo vya kipumbavu watu ili kuwatisha watu. Huwageuza waumini mateka na Watumwa hapa duniani.

Hata Shuleni walikuwepo Waalimu wapuuzi waliokuwa wakiwatisha Wanafunzi kuwa watafeli maisha. Walikuwa wakiwalaani lengo. Ili kuwafanya wanafunzi wao Watumwa na mateka.

Kwa kawaida watu wanaotoa toa laana au kuwahukumu wengine washindwe kwenye maisha. Huwa na tabia zifuatazo:

Mosi, Huwa na tabia ya kulazimisha heshima hata katika mambo ya kipuuzi. Kwa mfano, Waalimu wengi hupenda kulazimisha makosa kwa wanafunzi hata kama mwanafunzi hajafanya. Na kama mwanafunzi atabisha huanza kumtolea maneno ya karaha. Pia Waalimu hawapendi kubishiwa hata kwa jambo ni la kweli. Huo ni upuuzi. Mimi nilikuwa ni mwanafunzi nimeyaona hayo. Na sasa ni Mwalimu nayaona hayo.

Hata Wazazi nao kuna wakati hupenda kulazimisha heshima hata kwa mambo ya kipuuzi. Na kama mtoto hutofanya hivyo basi huanza kukutisha na kukulaani.

Pili, Hupenda kugeuza watu Mateka na Watumwa. Hupenda kunyenyekewa kama miungu watu. Hapa Wapo Wachungaji na Mashekhe. Wapo viongozi wa dini, wapo Pia wazazi. Ili umgeuze mtu mateka lazima umuogopeshe kwa Maneno ya vitisho na laana. Kwa mfano, Kuna wapuuzi wengi husema viongozi wa dini hawapaswi kunyoshewa vidole. Hawapaswi kuonywa kisa wao ni watumishi wa Mungu. Waulizeni swali, nani sio mtumishi wa Mungu.

Ukiwanyoshea kidole wanajitia kukutisha na laana kibao. Ukitaka usinyoshewe kidole fanya mapenzi ya Mungu. Sio kwa vile wewe ni mchungaji sijui sheikh. Sijui unajiita nabii ati ndio usiambiwe makosa yako unapoboronga. Lazima watu wajue kuwa ni laana kumnyooshea kidole mtu atendaye mema na haki ya Mungu. lakini sio kisa mchungaji, sijui Sheikh, sijui Mzazi na nani huko. Fanya Mema hakuna atakayekunyooshea kidole.

Narudia Mama hawezi akakulaani. Baba yako hawezi kukulaani. Wala mtu yeyote kamwe hawezi kukulaani.

Kinyume chake ni kuwa kama hakuna anayeweza kukulaani basi hakuna anayeweza kukubariki.

Wewe ndiye unaweza kujilaani au kujibariki. Wewe ndiye utabeba msalaba wako mwenyewe. Wewe ndiye unaamua ujilaani au ujibariki.

Nimesikia na kuona wala sijahadithiwa. Kuna watu wamejigeuza watumwa kwa ujinga wao. Ati Mama au Baba anakuambia njoo nikubariki au usipokuja nitakulaani. Huo ni upuuzi mkubwa sana.

Nimeona makundi kwa makundi wakienda kwa Wachungaji na masharifu kupokea maji ya baraka sijui upako. Huo ni upuuzi mkubwa na kujigeuza mwendawazimu. Hata mbuzi hawezi kufikiri kwa kiwango hicho. Ni dalili ya ukichaa.

Na ndipo hapo wajanja wanaojifanya Wachungaji hujipatia pesa kwa ulaghai wao wa kuuza maji sijui ya baraka. Sijui upako. Kuuza maji kanisani au msikitini sio dhambi. Dhambi ni kuwadanganya watu. Kwani mlishindwa kusema maji haya ni ya kanisa, tunaomba waumini mnunue maji ya Kanisa au msikiti uweze kupata faida kupitia maji. Lakini mnawalagahi watu kwa ujinga wao na udhalimu wenu.

Kama ulikuwa hujui Mtu anajilaani mwenyewe na kujibariki mwenyewe. Unapotenda haki unajibariki. Unapotenda dhuluma unajilaani.

Haki ni ipi sasa. Haki ni kufanya inayokupasa kulingana na mapenzi ya Mungu ambayo ni kanuni za asili. Kwa mfano ishi kwa upendo na watu wengine. Wape sitahaki watu kwa jinsi inavyowafaa.

Hunalaaniwi kwa maneno ya watu kama vile Wazazi wako, Waalimu wako, Viongozi wako wa dini. miongoni mwa watu wengine wanaojifanya wao ndio vihere here wakijipa mamlaka ya kutoa laana na baraka.

Laana inatokana na matendo yako. Kipi unafanya na kipi unasema.

Mtu anayedhani kuwa kuna mtu anaweza mlaani au kumbariki ni mtu asiyejitambua vyema. Ni mtumwa na mateka wa watu wengine.

Hakuna aliyepewa Mamlaka ya kulaani wala kubariki hapa duniani. Wanaojipa madaraka hayo ni kwa mapenzi yao wenyewe na upungufu wa kibinadamu. Upendeleo wao kwa watu wanaowapenda na chuki zao kwa wanaowachukia.

Mungu aliwapa Wazaz na makundi mengine mamlaka ya kufundisha kizazi kingine sheria na amri za Mungu. Jukumu la kufuata hizo sheria na amri za Mungu ni lao wenyewe. Wakitaka baraka watafuata amri za Mungu. Wakitaka laana na mikosi hawatafuata amri na sheria za Mungu.

Mungu amewapa watu namna ya kuyachagua maisha yao. Sio wengine wakuchagulie maisha. Ati kisa ni mchungaji anaweza kukubariki au kukulaani. Yaani kukuchagulia maisha.

Hakuna mtu anayeweza kukulaani asilani. Matokeo ya maisha yako ni wewe mwenyewe. Umasikini wako ni wewe mwenyewe uliousababisha kwa asimilia tisini. Magonjwa na Mikosi mingine wewe ndio chanzo cha yote hayo.

Acha kusingizia wengine na kulaumu wengi. Wewe ndio chanzo cha kuboronga.

Lakini pamoja na kuwa unaweza kuwa umeboronga lakini Mungu ni wa rehema na mwingi wa huruma. Ukimrudia na kumuomba toba atakusamehe. Huenda kwa sasa ni masikini kutokana na uvivu na uzembe. Kutokana na matumizi mabaya ya fedha. Kutokana na kukosa vipaumbele. Basi unaweza kubadilisha mfumo wa maisha kwa kufanya kuacha uvivu na uzembe. Kuwa makini na matumizi yako ya Fedha. Hiyo ndio Toba. Sio uende kanisani kuombewa au kwa waganga wa kienyeji kupoteza muda. Hao hawana watakachokusaidia zaidi ya kukupotezea muda wako.

Toba ya kweli sio kwenda kusali misikitini au Makanisani. Toba ya kweli ni kubadili mfumo wa maisha yako kwa kuamua kutoka ndani. Kuacha umalaya usije pata Ukimwi, Kuacha kuhonga au kunywa pombe kupita kiasi usijekuishia kuwa masikini na kupata magonjwa ya kisukari na ugonjwa wa ini.

Matendo yako ndio yanageuka laana na baraka kwenye maisha yako. Hakuna anayeweza kukulaani.

Wapo waalimu waliowalaani wanafunzi wakiwaambia watafeli mitihani yao na kufeli maisha lakini wanafunzi hao baadhi yao walifaulu na wanapeta kwenye maisha. Wapo wanafunzi waliokuwa wakibarikiwa na waalimu kwa tabia hao ya uoga uoga na unafiki. Wakaambiwa watafika mbali lakini baadhi yao wamefeli pakubwa shuleni na maisha.

Wapo watoto watiifu na wanafiki kwa Wazazi wao. Kila kitu wanawatii wazazi wao hata kama ni kibaya na kinadhuru. Wazazi wao huwasemea mazuri lakini watoto hao hawana mbele wala nyuma. Wanahangaika kutwa kucha hawana wanachofanya cha maana japokuwa wao ni wa maana.

Lakini muda huo huo wapo watoto wasiotii kila kitu kwa wazazi wao. Hasa vitu vya kipuuzi puuzi. Wazazi huwatolea laana lakini watoto hao wanapeta. Wanafanakiwa tena zaidi na zaidi.

Baraka ni kufanya mambo yaliyomema na kusema yaliyomema.

Haiwezekani mzazi atake umnunulie pombe kali au sigara wakati amekatazwa hospitalini au wewe mwenyewe unajua Pombe ni mbaya alafu umnunulie mzazi wako kisa unaogopa atakupa laana. Hakuna laana ya hivyo hata siku moja. Watoto wengi wanaowaendekeza wazazi wao kwa mambo ya kipuuzi huishia kupata laana japokuwa wazazi wao waliwatamkia baraka.

Lakini watoto ambao hawakuwasapoti wazazi wao kwa mambo ya kipuuzi wakatamkiwa laana waliishia kupata baraka.

Huwezi muona mwalimu anatembea na rafiki yako wa kike alafu usimwambie aache upuuzi wake. Ati kisa ni mwalimu. Kisa kakuzidi umri. Kisa atakutamkia laana. Nimeona kwa macho yangu wala sijahadithiwa. Unakuta Mwalimu anawapenda wale wanafunzi wanaojua uovu wake. Marafiki wa yule anayetoka naye kimapenzi anawapa Ofa za hapa na pale. Anawatamkia baraka. Nakuhakikishia kama ulikuwa mwanafunzi uliyependezwa na upuuzi huo na hukuukemea iwe ni kwa rafiki yako au huyo mwalimu kwa kuogopa kuchukiwa na kupewa laana na waalimu. Hakuna utakapofika kutokana na matendo yako hayo labda uombe toba.

Nimalize kwa Kusema kuwa Mungu aliwapa watu uchaguzi wa maisha yao wenyewe. Hata Mungu hakuchahulii maisha. Hata Mungu hakulaani wala kukubariki.

Alishakupa mambo mawili ya kuchagua. Baraka na laana. Ukichagua baraka unabarikiwa. Tena inategemea utafanya jitihada gani kubarikiwa. Jinsi unavyofanya mambo mema ndivyo unavyozidi kubarikiwa. Ukijachugua laana unalaaniwa. Jinsi unavyofanya maovu ndivyo unavyojilaani.

Mtu kamwe hawezi kukulaani wala kukubariki. Yote yapo chini yako. Acha kuwa mateka na mtumwa wa watu wengine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
0693322300
 
Nilijua humuamini Mungu ila katika andiko lako umemtaja. Ye mwenyewe anasema waheshimu baba na mama yako siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana Mungu wako, sasa usipowaheshimu si maana yake inakuwa kinyume chake?
 
Kuna jamaa mmoja anaitwa kamugisha muhaya huyu alilaaniwa na mama ake but mwamba kadiri siku zinavyokenda anazidi kutusua sio kawaida huyu jamaa alijenga nyumba ya ghorofa ndani ya mwezi tuu nyumbani ana gari km 10 hivi sasa najiuliza hiyo laana mbona haifanyi kazi kwa jamaa?
 
Back
Top Bottom