Wasichotaka kukisikia ccm kwenye mikutano yao,ila kipo kwenye mikutano yao. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasichotaka kukisikia ccm kwenye mikutano yao,ila kipo kwenye mikutano yao.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mubezi, Oct 28, 2010.

 1. Mubezi

  Mubezi Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Niliwaoji watu wa makamo kama 50 hv kila nilipohuzuria mikutano ya CCM hasa ya urais,kila mtu alikuwa na maoni yake ila yote yalilenga hapa,Ebu soma,"Ndugu zangu watanzania ni wazi kwamba kwa uchaguzi huu ndipo tunaweza kuchambua pumba tukazitupa na mchele wetu tukauweka ndani ya gunia ili kuwa chakula chetu kitamu cha baadae. Mgombea wa CCM na wapambe wake bado hawezi kutofautisha kati ya sera na ahadi kwa wapiga kura, Tangu siku ya kwanza ya kampeni hajamsikia akiongelea sera yoyote ya chama ndiyo maana imekuwa vigumu sana hata wagombea wa chama hicho kueleza sera kwa wananchi.Tunachokisikia ni ahadi na misaada na mikopo toka hapa na pale na mapicha mengi yaliyojaa gilba.
  Sera ni kama kanuni ya chama kufutana na katiba ya chama husika ilivyo. na sera inapaswa imguse kila mwananchi kwa nchi nzima, tofauti ya ahadi ambazo zitawahusu watu wa Mafia tuu, sisi wa Iringa haituhusu. watu wa Kigoma tuu sisi wa Maswa haituhusu,mfano kuwapa wakulima pemebejeo,je wasio wakulima?. lakini Mgombea wa CHADEMA anapozungumzia elimu bure,cement kushuka bei, hiyo ni sera na itamhusu kila mwanachi, na Afya bure ni kwa kila mtu n.k., n.k.
  Inaelekea CCM hawana sera ila uzushi na kukomalia mambo binafsi ya kuchafua wagombea wanaoonekana tishio kwa ufisadi. kuzusha Umwagaji damu na kufanya ndiyo sera yao labda iliwasaidia huko nyuma lakini kwa sasa sijui? mawefikia mwisho kwa hiyo mengi mtayaona na kuyasikia lakini watambue TZ ya leo si ya Jana watu wanataka mabadiliko".Hicho ndicho nilichokisikia kwenye mikutano ya ccm,ambacho wao CCm hawataki kukisikia.
   
 2. J

  Jobo JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Umesema vyema! Ahadi za JK zimezidi. Ambacho sijasikia ni kwa jinsi gani Serikali yake fisadi inaweza kupata fedha za kukidhi hizo ahadi. Wakisemwa wanadai wametukanwa, lakini wao wakisema wengine ni "majuha", wanadai hilo si tusi! Yaani CCM ni majuha kweli kweli.
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ukiwauliza kuhusu yale matundu ya choo yaliyojengwa kwa milioni 700 watasema hiyo haihusiani na uchaguzi
   
 4. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ni nzuri nimeipenda na huo ndo ukweli
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wanachofanya mafisadi ni kuwafukarisha wananchi ili wawe maskini wa kutupwa. Wakati wa kampeni kazi yao itakuwa ndogo tu ni kuorodhesha ahadi za nitawanunulia bajaji, nitapandisha hadhi hospitali kana kwamba kupandisha hadhi kunaambatana na muujiza wa kuongezeka kwa madawa, madaktari, vitendea kazi, mazingira bora ya watumishi, n.k, n.k. hiyo ndiyo sera ya mafisadi na chichiem yao. kwa hiyo, miye simshangai mkwele kwa staili yake ya kuahidi ahadi zisizo na miguu wala kichwa.
   
 6. b

  boybsema Senior Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Jamani CCM basi....sitaki hata kusikia hilo jina tena....buriani /ccm
   
Loading...