Wapo viongozi wa kisiasa nchini mwetu,ambao wanaonekana kuguswa sana na matatizo ya mtu mmoja mmoja na hivyo kupenda kuwasikiliza hadharani kwenye mikutano yao ya kisiasa.
Hutokea watu wachache wakapata nafasi ya kujielezea shida zao,na kiongozi hutoa maelekezo na hivyo kuonekana shujaa kwa haraka.
Lakini kiongozi kushughulika na mtu mmoja mmoja,ni ngumu sana kwa sababu kila mwananchi anazo shida na kero zake ngumu kabisa. Hivyo kiongozi makini ni vizuri kushughulika na mifumo inayogusa watu wengi kwa wakati mmoja.
Aidha sifa kwa kiongozi mmoja mmoja sio tija kwa mwananchi,bali tija ni uwajibikaji wa serikali yote,au kama ni chama cha siasa inapendeza kuona jambo la chama linakuwa la viongozi wote na sio kiongozi mmoja.Enzi za kuhangaika na sifa kwa mtu mmoja, zilishapitwa.
Vyama vya siasa, viendelee kuelezea sera zao na serikali iliyopo madarakani iendelee kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa kanuni zilizopo.Kama kuna kunyosheana vidole, hayo wayafanye kwenye kikao vyao vya ndani.
Mbwembwe za kwenye majukwaa,ni vizuri zikabaki kwa wasanii wa muziki.