Ni wiki ya pili sasa tangu wanamgambo wa Boko haram wavamie shule na kutoweka na wanafunzi wa kike zaidi ya 223. Mpaka sasa haijulikani kama wanafunzi hao wako hai au laa. Sasa swala kujiuliza: Ile ndege ya malaysia ilipotoweka ikiwa na abiria zaidi ya 200 tuliona dunia nzima ime react, ikijitolea kwa hali na mali,na sasa wamehamua kuitafuta kwa mwaka mmoja
Mwaka 1 kuitafuta ndege ya Malaysia - BBC Swahili - Habari. Lakini kwa hili tukio la Nigeria hatuoni hata kama tukio limetiliwa umuhimu katika vyombo vya habari. Humu duniani inaonekana kuna double standard. Mimi nilitegemea vyombo vya kipelelezi na majeshi kadhaa wangeisha kwenda Nigeria ili kuweka nguvu katika kuokoa hao watoto. Huko waliko haijulikana kama kweli wanapewa chakula maana ni wengi kuwalisha katika maficho, au wameuawa na kuzikwa kwenye kaburi la pamoja, haijulikana. Very sad