Tatizo hata wanaijeria wenyewe hawalipi suala hilo kipaumbele. Sasa wasitegemee jamaa wengine kufanya hivyo.Lakini naona alipewi kipaumbele kama ilivyo habari za Malaysian Airway na habar za NBA katika vyombo vingi vikubwa vya habari, sasa sijui ni kuwadharau waafrika au kutowapa kipaumbele wanawake wa kiafrika. inauma sana.
hao wanafunzi ni wazungu hadi watafutwe na madege makubwa?
Sidhani kama Nigeria wameomba kusaidiwa kwa mambo yao ya ndani.
Ni wiki ya pili sasa tangu wanamgambo wa Boko haram wavamie shule na kutoweka na wanafunzi wa kike zaidi ya 223. Mpaka sasa haijulikani kama wanafunzi hao wako hai au laa. Sasa swala kujiuliza: Ile ndege ya malaysia ilipotoweka ikiwa na abiria zaidi ya 200 tuliona dunia nzima ime react, ikijitolea kwa hali na mali,na sasa wamehamua kuitafuta kwa mwaka mmoja Mwaka 1 kuitafuta ndege ya Malaysia - BBC Swahili - Habari. Lakini kwa hili tukio la Nigeria hatuoni hata kama tukio limetiliwa umuhimu katika vyombo vya habari. Humu duniani inaonekana kuna double standard. Mimi nilitegemea vyombo vya kipelelezi na majeshi kadhaa wangeisha kwenda Nigeria ili kuweka nguvu katika kuokoa hao watoto. Huko waliko haijulikana kama kweli wanapewa chakula maana ni wengi kuwalisha katika maficho, au wameuawa na kuzikwa kwenye kaburi la pamoja, haijulikana. Very sad
Waafrika wengine mkisaidiwa mnasema mnaingiliwa mambo yenu ya ndani, mkiachiwa mfanye mambo yenu wenyewe mnalalamika dunia haiwajali.
Huwezi kulinganisha tukio la kupotea ndege lililotokea kwa kupitia anga na bahari za kimataifa na kubeba watu wa mataifa tofauti na kitendo cha watoto wa Nigeria waliotekwa Nigeria.
Rai yangu kwa Jonathani kuomba Msaada kwa Mashirika ya Usalama nje ya Nigeria ili kutokomeza hiki kikundi.
Evidence? inategemea ni msaada wa mambo yapi
Unaomba msaada marekani ipambane na CIA?....kalagabaho!