Wasichana wa kindamba

Wachoyo...hiyo utakuta kwa familia nzima...na mababa hawajali familia yaan wanalea watoto kama kuku wajitafutie wenyewe riziki...
 
kwa tabia za wadada sijajua ila za wakaka ziko pouwaaa hawana tatizo
 
Mwa kindamba umechikia helokoputa ya mzungu inalia akabu akabu!!! Ilitua chambani hapa
 
Uki shampendezesha ie. kuvaa vizuri,katako kakaonekana nk. Jiandae kero yakwenda kwenda kwao mara kwa mara ili kuwaringishia kijijin kwao kuwa na yeye ni wa mjini. Pili fanya hima kwako roba la mpunga lisipungue...wanapenda ubwabwa na somba(samaki).
 
mkishaoana niambie niende kutalii wa utalii wa uvuvi nikajionee live vboko na mamba na mashemeji zako, maana ninauhakika katka familia yao haikosi mvuvi
 

Gwenga Wakashina
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa napitia uzi huu nikakuta kuna mtu alitaka kujua kuhusu tabia za wadada wa Kabila langu la Wandamba. Ok, kwa ufupi ni kabila dogo linalomezwa na kabila la Wapogoro kutoka Mkoa wa Moro kuanzia sehemu za Mang'ula, Ifakara makao wakuu ya Wilaya ya Kilombero, kuteremkia Mofu,Luipa,Mbingu7(Mbingu),Mngeta,Chita,Merela,Mlimba,Ngombo,Biro,Malinyi,Itete kurudi Ifakara kwa njia ya kuvuka mto Kilombero. Mazingira ya makazi ni bonde la mto Kilombero, kuanzia chanzo cha mto Kilombero wenyewe wanaita Mnyera mpaka Ifakara. Kutokana na kuishi bondeni eneo chepechepe, chakula kikuu ni Mpunga(kwa maana ya wali) wenyewe wanaita 'Ubagha'=ubwabwa na mboga ni samaki. Vyakula vingine lkn ni kwa uchache kutegemea msimu ni mihogo ya kuchemsha,kula ugali wake wanaita undimbali ni kuleta mkosi nyumbani, pia mahindi ya kuchemsha, kuchoma,maboga,viazi n.k. ugali wa mahindi unaliwa wakati wa njaa tu, yaani kuanzia mwezi Dec mpaka wa March kabla ubwabwa mpya haujaingia. Pia wanakula nyama haswa za pori kwani pia humo undambani ni makazi ya wanyama pori. Hawana asili ya kufuga kwani wanyama pori walikuwa wengi mno kabla serikali kuleta makabila ya wafugaji kama wamasaai sehemu za Biro,Mang'ati sehemu za Itete na Wasukuma kuanzia Mngeta,Merela,Ngombo sehemu zilizobaki. Vile ni kabila la bondeni na kujitenga, wamekuwa wakarimu,undugu,nidhamu na heshima. Si watu wa kulima mashamba makubwa wala biashara kubwakubwa, bali ni ndogo na rahisi sana kuridhika na akipatacho, umasikini na ufukara na uduni wa maisha havimsumbui mladi anaheshimika kwa jamii yake. Misiba kwao ni kitu kikubwa mno pengine kuliko hata kuuguza mgonjwa. Mathalani utakaa naye Dar huyo mkeo, anaweza kukuambia tu kuwa nyumbani(undambani) kuna mgonjwa wala asikusisitize kutaka kwenda au kupeleka msaada wa matibabu, lkn akisikia msiba lazima atataka kwenda, tena sio mara moja ila stegi tatu za msiba(Kuzika,kulalia kuanua tanga na Arobaini ambayo inafanyika kunapokuwa na chakula na pombe ya kutosha). Kuhusu eti 'umama huruma' huo ni uongo kwani ni kabila lenye watu wa aibu hata kazi ya uhouse girl hawafanyi! Kama kuna ma barmaid wa kindamba basi atafanyia mbali kabisa kkn kuanzia Ifakara mpaka Mlimba wanafanya wageni tu(naogopa kuwataja). Tabia ya kununa ni kweli wanayo pia ya kunung'unika akihisi ameonewa. Ogopa mwanamke au Wandamba kwa ujumla akikata tamaa, anaweza kufanya kitu ambacho kinaweza kumdhuru mwenyewe, kama kuzira ndoa(tendo), mke, mume, kazi,wadhifa,watoto,wajibu bila kujali matokeo yake yaliyodhahili mbele yake! Ukipata mke wa kindamba Orijino umepata mke mladi umjali, kumheshimu na kujali ndugu/wazazi wake si mtu wa makuu wala umalaya,tamaa,uchoyo,ukatili. Pia ujue hapo kwako patakuwa pahala pa furaha,kicheko na amani sio kwako tu hata kwa jirani kwani ni wacheshi na waongeaji sana! Ndiyo hayo ndugu yangu, shemeji mtarajiwa, karibu Ngombo ule samaji bila kuchambua miba nje bali mdomoni kwani samaki anaingia mdomoni upande huu na miba inatika upande huu. Yule aliyetaka kujua tabia za wanaume,zote ni sawa na hapo juu ila wanaume ni mamwamba na wababe hata kwenye ndoa,kazini,biashara,mpirani. Ila woteni watu wa dini(wengi ni wakatoliki). Samahani nitakapokuwa nimekosea ila kuna makabila yamejichanganya na wandamba, hao wana tabia zao hivyo wapo baadhi ya wandamba wameziiga nayo ni Wangoni,Wahehe,Wangindo,Wabena,Wapogoro nahats Wanyakyusa. Usije kushangaa mndamba akawa na tabia za hao zinazojulikana
 
Duh!yaani midomo yao kama separator machine minofu huku miba kuleee!hii kiboko kwelikweli.
 
Ukiyavulia nguo maji shurti uyaoge, ukianza kuuliza kwa watu watakupa ushauri ambao unaweza kukuvunja moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…