Wasichana wa kileo wapo 'insecured' sana

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Hali?

Naamini mara moja au zaidi wewe mwanaume utakuwa umewahi kuhisi au kugundua kabisa hili.

Kuna ile mmekaa sehemu au kwenye mkusanyiko fulani, mmechanganyika wanaume kwa wanawake. Sasa mara wanawake wanaanza kujiongelesha kwa kusimulia stori za kuji expose kwa makusudi... nasema kwa makusudi kwa sababu wengi wao huwa si ya kweli wanayoongea.

Unakuta anaanza kusimulia kwa sauti, mara "natafuta mtu anayeuza kiwanja kuanzia ml 40", mara mwingine anasema "mmmh nataka ninunue gari nimechoka boda" nk.

Si vibaya kwa wao kusema haya, ila kwa nini huwa wanatengeneza mazingira ya maongezi yao kusikiwa na wanaume hasa walio karibu yao? Na more enough kuna wengine unaweza ukawa unawajua ila wao hawafahamu.

Kwa nini mabinti wanakuwa inferior kiasi hicho? Yaani wakikutana na mkiwa pembeni wanaume, tena mkiwa wanaume si pangu pakavu basi stori zao huwa ni za pesa tu na wanafanya juu chini mpaka msikie.

Binafsi hii inanisononesha mno. Kwa nini watu hawajiamini? Hofu inatoka wapi? Unamuogopa nani wewe dada?
Eti dada anakwenda kununua fungu la mchicha analificha ndani ya pochi yake ili asionekane kama ananunua mchicha, for what?

Wanawake mmekuwa miyeyusho mno, sasa hamjui kuwa mnawaumiza wanaume wengine ambao ni pangu pakavu. Binafsi siumii ila nabaki kushangaa na kucheka moyoni tu, kwa kuwa hakuna cha kunifanya niwe inferior. Ila ukiwa pangu pakavu ni lazima uanze kuwachukia wanawake na kusema wanapenda hela. Kumbe wao wanakurusha roho tu!

Kuwa wewe!
 
Back
Top Bottom