wasichana dsj wabakwa kwa zamu na vibaka

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,617
LEO tumechapisha taarifa za wanafunzi wa kike wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) kilichoko Ilala, Dar es Salaam, kuvamiwa na vibaka, wakaporwa mali, fedha na kisha kubakwa kwa zamu. Vibaka hawa wamepita kwenye lango linalodaiwa kuwa halifungwi muda wote.

Inadaiwa kuwa mlinzi aliyekuwa mlangoni, Mmasai alikamatwa akawekwa chini, akafungwa kamba, kisha vibaka hao wakaingia kwenye vyumba vya wanafunzi wa kike na kuanza kufanya maasi hayo. Hapa tunadhani yapo matatizo mengi kimsingi. Ukiacha uzembe kwa upande wa uongozi wa shule kutokuwa na lango imara, tatizo ni zaidi ya hilo.

Kwamba maelezo yaliyopo ndani ya habari hii, yanaonyesha muda tangu vibaka hao wamefika getini, wakapambana na Mmasai, kufunga kamba, kuingia tena katika vyumba vya hosteli kimoja baada ya kingine wakikusanya fedha, mali na kubaka mabinti hao, ulikuwa mrefu.

Katika eneo la ulinzi shirikishi, chuo kama hiki ambacho ni cha waandishi wa habari, tulitarajia hawa wangekuwa wa kwanza kuwasiliana na polisi. Hawa wangeweza kupiga simu polisi, wakaeleza hatari inayowakabili, na hakika polisi kwa sasa wana ushirikiano mkubwa, hivyo wangeweza kusaidia.

Lakini tunachokiona pia, Polisi sasa wanapaswa kuongeza kasi. Kinachotokea, ni kwamba wezi wa kutumia silaha nzito wamepungua, lakini idadi ya vibaka wenye kufanya wizi inazidi kuongezeka siku hadi simu. Jana usiku kucha, wananchi wa Kitunda, Ilala Dar es Salaam, walikesha wakifukuzana na vibaka.

Tena vibaka hawa wana jeuri kweli. Wanapita nyumba kwa nyumba wakigonga mlango na kuwataka wenye nyumba wafungue na kuwapa watakacho utadhani wanalipisha kodi. Kimsingi eneo kama Kitunda, wanapata athari za waliokuwa wakazi wa Kipawa, ambao wengi wamevunjiwa nyumba zao kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege, ambao wamemwagika Kitunda.

Tunasema vitendo vya vibaka kutumia nguvu kupora wananchi, tulikuwa tumevisahau. Kwa sasa hali hii imerejea kwa kasi ya ajabu, hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi kurejesha utaratibu wa doria katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Tunaamini polisi wakifanya juhudi za makusudi, ni rahisi kukamata watu hawa wanaosumbua.

Kwa sasa vibaka wanavamia maduka ya kuuza vocha za simu, vibanda vya maji, lakini hatukutarajia waende hadi kwenye hosteli za wasichana na kufanya uasi wa aina hiyo. Tunataka hatua kali
zichukuliwe kuepusha aibu hii.

Source:
Polisi Dar changamkeni
 
pole yao dada zetu hawa ni ngumu sana kwenu waadhulika kusahau na kusamehe kama sisi tulivo umbiwa kusamehe lakini mungu ndiye ajuaye poleni tena poleni sana pia hili ni angalizo pia kwa wanachuo wengine maeneo mbalimbali hapa nchini kwetu maana haya matukio yana tokea mara kwa mara japo kuwa serikali inafumbia macho kama haioni na inakua ngumu kwa wadhulika wa namna hii kufuatilia haki yao.

Poleni

valex
 
Duh hii ni kali, sisi tunaoishi maeneo ya pembezoni inabidi tujiandae kwa sungusungu. Kama wanaweza hata kubaka hii ni hatari sana naomba polisi watumie teknologia ya DNA kuwapata wote waliofanya uhaini huu na washitakiwe kwa kosa la kujaribu kuu, kwa maana kumbaka mtu kwa sasa ni sawa na kumunywesha sumu ya kumuua pole pole ikiwa mbakaji ana virus na ni maluweluwe ya miaka yote, wengi watapata wakati mgumu kuendelea na uhusiano na wapenzi wao kwa hofu ya kuambukizwa malazi... poleni sana dada zetu. Nawapa changamoto muitumie hii kama kichocheo cha kupambana na huu uhuni mkitumia kalamu pindi mtakapo maliza masomo. Mnaweza mkaleta mabadiliko katika siasa na jinsi wanasiasa wanavyoutazama usalama wa raia wao, kwa sasa tunalindwa na Mungu peke yake. Hawa kama wangeamua kuua wangeliweza kuua wengi kwa jinsi walivyofanikiwa kubaka kwa zamu bila kukamatwa wala kuogopa.
 
Yaani naweza nikaanza kuwatukana Kova na wenzake lakini naamini humu hapiti na haitasaidia kitu. Ni kitendo cha aibu kwa jeshi la polisi, na hakuna kiumbe atakae wajibika maana hao partrol wa usiku kazi yao kuzungukia kwenye mabaa tu usiku kucha, Lukuvi wajibisha kina Kova au level yako ni wakina Masatu tu? Kova ondoka tuachie jiji letu :A S-alert1:
:embarrassed:
 
Too sad... hata nashindwa niseme nini... ngoja nipate lunch kwanza..
 
too sad.................yaani.........nashindwa hata nisemeje..............huo ni unyama ambao....................damn
 
LEO tumechapisha taarifa za wanafunzi wa kike wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) kilichoko Ilala, Dar es Salaam, kuvamiwa na vibaka, wakaporwa mali, fedha na kisha kubakwa kwa zamu. Vibaka hawa wamepita kwenye lango linalodaiwa kuwa halifungwi muda wote.

Inadaiwa kuwa mlinzi aliyekuwa mlangoni, Mmasai alikamatwa akawekwa chini, akafungwa kamba, kisha vibaka hao wakaingia kwenye vyumba vya wanafunzi wa kike na kuanza kufanya maasi hayo. Hapa tunadhani yapo matatizo mengi kimsingi. Ukiacha uzembe kwa upande wa uongozi wa shule kutokuwa na lango imara, tatizo ni zaidi ya hilo.

Kwamba maelezo yaliyopo ndani ya habari hii, yanaonyesha muda tangu vibaka hao wamefika getini, wakapambana na Mmasai, kufunga kamba, kuingia tena katika vyumba vya hosteli kimoja baada ya kingine wakikusanya fedha, mali na kubaka mabinti hao, ulikuwa mrefu.

Katika eneo la ulinzi shirikishi, chuo kama hiki ambacho ni cha waandishi wa habari, tulitarajia hawa wangekuwa wa kwanza kuwasiliana na polisi. Hawa wangeweza kupiga simu polisi, wakaeleza hatari inayowakabili, na hakika polisi kwa sasa wana ushirikiano mkubwa, hivyo wangeweza kusaidia.

Lakini tunachokiona pia, Polisi sasa wanapaswa kuongeza kasi. Kinachotokea, ni kwamba wezi wa kutumia silaha nzito wamepungua, lakini idadi ya vibaka wenye kufanya wizi inazidi kuongezeka siku hadi simu. Jana usiku kucha, wananchi wa Kitunda, Ilala Dar es Salaam, walikesha wakifukuzana na vibaka.

Tena vibaka hawa wana jeuri kweli. Wanapita nyumba kwa nyumba wakigonga mlango na kuwataka wenye nyumba wafungue na kuwapa watakacho utadhani wanalipisha kodi. Kimsingi eneo kama Kitunda, wanapata athari za waliokuwa wakazi wa Kipawa, ambao wengi wamevunjiwa nyumba zao kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege, ambao wamemwagika Kitunda.

Tunasema vitendo vya vibaka kutumia nguvu kupora wananchi, tulikuwa tumevisahau. Kwa sasa hali hii imerejea kwa kasi ya ajabu, hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi kurejesha utaratibu wa doria katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Tunaamini polisi wakifanya juhudi za makusudi, ni rahisi kukamata watu hawa wanaosumbua.

Kwa sasa vibaka wanavamia maduka ya kuuza vocha za simu, vibanda vya maji, lakini hatukutarajia waende hadi kwenye hosteli za wasichana na kufanya uasi wa aina hiyo. Tunataka hatua kali
zichukuliwe kuepusha aibu hii.

Source:
Polisi Dar changamkeni

Oooh dear! mlinzi wa kimasai ??? analinda chuo???....ooh Almighty GOD help us!!!!
mix with yours
 
Kwa mtazamo wangu naona kamanda Kova ngoma zinamponyoka.Naona kama anabwabwaja tu kwenye vyombo vya habari zaidi mara wanapofanya kitu kidogo lakini kuna mambo mengi yanaendelea huku mjini yanayohitaji kazi yao ya kutosha!
 
Waandishi wamedunguliwa na vibaka?!Ina maana simu zao zilizimwa au America alipitisha mtambo wa kuzima simu?
Pamoja na hayo poleni kwani utamu mlioupata hamkuutegemea na ambao umebadilika na kuwa uchungu,sasa tusubiri mimba zisizotarajiwa
 
Eti kisiwa cha Amani maweee. Tunambeep Mungu sana
Yes ni kisiwa cha amani kwani WAHALIFU WANAFANYA UNYANG'AU HALAFU WANAACHWA WAENDE NA KUTAMBA KWA AMANI.
only in Tanzania
halafu polisi wanapokea kodi zao kutoka kwa wahalifu ili wasiwatie mbaroni

hii ni nchi nayo jamani
 
Back
Top Bottom