Wakuu habari.
Jana nimekaa zangu hapa geto sina hili wala lile, ghafla nikaona kwenye simu yangu ile text nzuri kuliko zote duniani( Imethibitishwa umepokea.....) imeingia kwenye simu yangu. Ilikua takribani tsh laki 5 . Nikapiga hesabu za haraka haraka sikupata kumbukumbu za mtu yeyote ninayemdai wala niliyeongeanae kuhusu kunitumia pesa kwa muda huo, hivyo nikaona nikimbie fasta kwa wakala kabla aliyetuma bahati mbaya hajaongea na wahusika waireverse transaction.
Nikachomoa pesa zooote kisha nikazima simu, na kwakua ni pesa ambayo sikuitegemea tukashauriana na washkaji tukaenda zetu viwanja kujipongeza kwa kuwa na nyota ya kufatwa na hela.

Tuliitumia kwa kuikomoa maana haikua pesa ya jasho lakini hatukufanikiwa kuimaliza yote. Leo asubuhi tukaamkia grocery Fulani kitaa kwetu tukachukua bia zetu za kutosha tukaanza kushusha taaratibu geto wakati tunasubiri saa 10 ifike bar zifunguliwe.
Jioni nikapata wazo la kuwasha simu na ndipo nikakutana na mauzauza. Zilikua text za mdogo wangu aliyepo chuo kikuu kumbe alikua ametuma ile pesa ili nimnunulie laptop kwaajili ya matumizi ya chuo kwakua huku dar bei ni rahisi kulinganisha na dodoma anaposoma. Kumbe baada ya kutuma pesa alituma na msg za maelekezo ila sikuziona kwakua nilifunga simu baada ya kutoa pesa. Muda si mrefu akapiga simu kuuliza kama nimeshanunua tayari,yaani hadi ulabu ukakata kabisa

.. Hapa nimebaki na elfu 40 tu na baada ya kuwaambia masela wanichangie kila mmoja utasikia sijui nadaiwa Kodi, sijui nasomesha, sijui mshahara bado, yaani hakuna msela wa kweli hata mmoja.
Mods naomba marekebisho ya heading. "Washkaji wengine sio wana kabisa".