Washkaji wengine sio wana kabisa

Washkaji wengine sio wana kabisa

pipi mti

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
764
Reaction score
515
Wakuu habari.

Jana nimekaa zangu hapa geto sina hili wala lile, ghafla nikaona kwenye simu yangu ile text nzuri kuliko zote duniani( Imethibitishwa umepokea.....) imeingia kwenye simu yangu. Ilikua takribani tsh laki 5 . Nikapiga hesabu za haraka haraka sikupata kumbukumbu za mtu yeyote ninayemdai wala niliyeongeanae kuhusu kunitumia pesa kwa muda huo, hivyo nikaona nikimbie fasta kwa wakala kabla aliyetuma bahati mbaya hajaongea na wahusika waireverse transaction.
Nikachomoa pesa zooote kisha nikazima simu, na kwakua ni pesa ambayo sikuitegemea tukashauriana na washkaji tukaenda zetu viwanja kujipongeza kwa kuwa na nyota ya kufatwa na hela.
Tuliitumia kwa kuikomoa maana haikua pesa ya jasho lakini hatukufanikiwa kuimaliza yote. Leo asubuhi tukaamkia grocery Fulani kitaa kwetu tukachukua bia zetu za kutosha tukaanza kushusha taaratibu geto wakati tunasubiri saa 10 ifike bar zifunguliwe.

Jioni nikapata wazo la kuwasha simu na ndipo nikakutana na mauzauza. Zilikua text za mdogo wangu aliyepo chuo kikuu kumbe alikua ametuma ile pesa ili nimnunulie laptop kwaajili ya matumizi ya chuo kwakua huku dar bei ni rahisi kulinganisha na dodoma anaposoma. Kumbe baada ya kutuma pesa alituma na msg za maelekezo ila sikuziona kwakua nilifunga simu baada ya kutoa pesa. Muda si mrefu akapiga simu kuuliza kama nimeshanunua tayari,yaani hadi ulabu ukakata kabisa .. Hapa nimebaki na elfu 40 tu na baada ya kuwaambia masela wanichangie kila mmoja utasikia sijui nadaiwa Kodi, sijui nasomesha, sijui mshahara bado, yaani hakuna msela wa kweli hata mmoja.
 
Iwe ni chai au kweli

Funzo kuu, Ukitumiwa Pesa kwenye mtandao na namba usioifahamu tulia kwanza wala usikimbiliea kuitoa au mpigie simu muulize wewe ni nani!

Usijidanganye sijui ukatoe utupe laini , Dunia imebadilika utagundulika tu.
 
Ama kweli kuna watu wanajua jinsi ya kutumia pesa....

Duniani kuna mambo...
 
Ww ulikuwa unakula tu pesa hujui imetoka wapi. Principle za pesa zipo wazi pesa yyte inayoingia kwenye himaya yako ni lzma ujue imetoka wapi.
 
Hapo hata mimi nisingechanga aise, hela yenyewe ya bumu dogo namchana tu aendelee kuazima laptop kwa masela wake labda kama anasoma computer related courses. Kama ni baed tupa kule
 
Wakuu habari.

Jana nimekaa zangu hapa geto sina hili wala lile, ghafla nikaona kwenye simu yangu ile text nzuri kuliko zote duniani( Imethibitishwa umepokea.....) imeingia kwenye simu yangu. Ilikua takribani tsh laki 5 . Nikapiga hesabu za haraka haraka sikupata kumbukumbu za mtu yeyote ninayemdai wala niliyeongeanae kuhusu kunitumia pesa kwa muda huo, hivyo nikaona nikimbie fasta kwa wakala kabla aliyetuma bahati mbaya hajaongea na wahusika waireverse transaction.
Nikachomoa pesa zooote kisha nikazima simu, na kwakua ni pesa ambayo sikuitegemea tukashauriana na washkaji tukaenda zetu viwanja kujipongeza kwa kuwa na nyota ya kufatwa na hela.
Tuliitumia kwa kuikomoa maana haikua pesa ya jasho lakini hatukufanikiwa kuimaliza yote. Leo asubuhi tukaamkia grocery Fulani kitaa kwetu tukachukua bia zetu za kutosha tukaanza kushusha taaratibu geto wakati tunasubiri saa 10 ifike bar zifunguliwe.

Jioni nikapata wazo la kuwasha simu na ndipo nikakutana na mauzauza. Zilikua text za mdogo wangu aliyepo chuo kikuu kumbe alikua ametuma ile pesa ili nimnunulie laptop kwaajili ya matumizi ya chuo kwakua huku dar bei ni rahisi kulinganisha na dodoma anaposoma. Kumbe baada ya kutuma pesa alituma na msg za maelekezo ila sikuziona kwakua nilifunga simu baada ya kutoa pesa. Muda si mrefu akapiga simu kuuliza kama nimeshanunua tayari,yaani hadi ulabu ukakata kabisa .. Hapa nimebaki na elfu 40 tu na baada ya kuwaambia masela wanichangie kila mmoja utasikia sijui nadaiwa Kodi, sijui nasomesha, sijui mshahara bado, yaani hakuna msela wa kweli hata mmoja.

Mods naomba marekebisho ya heading. "Washkaji wengine sio wana kabisa".
Ndiyo Ukomee
 
Aisee mtoto wa kiume unashangangilia kupokea salio kutoka kusikojulikana{hata kama uwongo}tena unakimbilia kabisa kwa wakala kuitoa na ni usiku we ni mzima kweli?hela nyengine sizo kuna siku utaota ndoto mbaya usiyojua ilikotoka.
 
Wakuu habari.

Jana nimekaa zangu hapa geto sina hili wala lile, ghafla nikaona kwenye simu yangu ile text nzuri kuliko zote duniani( Imethibitishwa umepokea.....) imeingia kwenye simu yangu. Ilikua takribani tsh laki 5 . Nikapiga hesabu za haraka haraka sikupata kumbukumbu za mtu yeyote ninayemdai wala niliyeongeanae kuhusu kunitumia pesa kwa muda huo, hivyo nikaona nikimbie fasta kwa wakala kabla aliyetuma bahati mbaya hajaongea na wahusika waireverse transaction.
Nikachomoa pesa zooote kisha nikazima simu, na kwakua ni pesa ambayo sikuitegemea tukashauriana na washkaji tukaenda zetu viwanja kujipongeza kwa kuwa na nyota ya kufatwa na hela.
Tuliitumia kwa kuikomoa maana haikua pesa ya jasho lakini hatukufanikiwa kuimaliza yote. Leo asubuhi tukaamkia grocery Fulani kitaa kwetu tukachukua bia zetu za kutosha tukaanza kushusha taaratibu geto wakati tunasubiri saa 10 ifike bar zifunguliwe.

Jioni nikapata wazo la kuwasha simu na ndipo nikakutana na mauzauza. Zilikua text za mdogo wangu aliyepo chuo kikuu kumbe alikua ametuma ile pesa ili nimnunulie laptop kwaajili ya matumizi ya chuo kwakua huku dar bei ni rahisi kulinganisha na dodoma anaposoma. Kumbe baada ya kutuma pesa alituma na msg za maelekezo ila sikuziona kwakua nilifunga simu baada ya kutoa pesa. Muda si mrefu akapiga simu kuuliza kama nimeshanunua tayari,yaani hadi ulabu ukakata kabisa .. Hapa nimebaki na elfu 40 tu na baada ya kuwaambia masela wanichangie kila mmoja utasikia sijui nadaiwa Kodi, sijui nasomesha, sijui mshahara bado, yaani hakuna msela wa kweli hata mmoja.

Mods naomba marekebisho ya heading. "Washkaji wengine sio wana kabisa".
Ahahahahahahhaah aisee nmecheka
 
Ama kweli kuna watu wanajua jinsi ya kutumia pesa....

Duniani kuna mambo...
Yani kuna watu wana enjoy sana maisha nna rafkiangu siku akipata pesa tu labda laki tatu hivi kesho yake kazini haonekani tena kuonekana siku ya nne labda
akiwa hana hata hela ya supu
Namfananisha na huyu jamaa
 
Kwakweli wanafanana 100% maana kumbe hana hata akiba ya kulipa hilo deni.
Kapesa alikodhani kamepotea njia ndo kakateketezea kwny pombe
 
Mkuu hiyo heading hata isinge kuwa hivyo, Then hao wana unawapa lawama za bure tuu, hiyo heading ingemuhusisha huyo mdogo wako bhana na sio hao washkaji
 
Iwe ni chai au kweli

Funzo kuu, Ukitumiwa Pesa kwenye mtandao na namba usioifahamu tulia kwanza wala usikimbiliea kuitoa au mpigie simu muulize wewe ni nani!

Usijidanganye sijui ukatoe utupe laini , Dunia imebadilika utagundulika tu.
We utakufa maskini
 
Inawezekana kweli lakini Ungeona Jinaa la mdogo wakoo kama yeye ndo alikutumia hiyo pesaa...!! Me ilinitokea lakini sikuitoa ilee helaa ilikuwa laki mojaa...ilaa baadae nkakuta Jina la kaka angu limerudisha pesa zile kwa wakala... Daa nkasema je ningetoa na kutupa line so ingekuwa noma sanaa na Nlikuwa na shida hapo bumu limekataa
 
Back
Top Bottom