Washindwa kutekeleza agizo la kamati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Washindwa kutekeleza agizo la kamati

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando

  Joseph Zablon
  AGIZO la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mashirika ya Umma (POAC), limegonga mwamba baada ya jenereta lililopo nyumbani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, kutoondolewa kama ilivyoagizwa.

  Uchunguzi wa Mwananchi umebainisha kuwa jenereta hilo halijaondolewa na hakuna dalili zozote za utekelezaji wa amri hiyo.Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe kutokana na kutumia mafuta kutoka Tanesco.Zitto aliagiza jenereta hilo liondolewe ili mkurugenzi huyo aone adha wanayoipata wananchi wengine mara umeme unapokatika.

  Uchunguzi wa Mwananchi nyumbani kwa mkurugenzi huyo katika Mtaa wa Chaza namba 13 Oysterbay Jijini Dar es Salaam, ubainisha kuwa amri hiyo haijatekelezwa.
  "Halijaondolewa na umeme kwa jirani zake ukikatika kwake kama kawaida," alisema mfanyakazi wa nyumba ya jirani.

  Alisema umeme ukikatika mchama, umeme unawaka nyumbani kwa mkurugenzi huyo.Jirani huyo alisema mgawo unawatesa majirani katika mtaa huo, lakini mkurugenzi huyo anapata huduma hiyo usiku na mchana bila matatizo yoyote.

  Jirani mwingine katika mtaa huo alisema hana uhakika wa ukubwa wa jenereta analotumia mkurugenzi huyo lakini anadhani ni jenereta linalojiwasha lenyewe baada ya umeme kukatika."Tukisikia linaunguruma tu, tunajua umeme umekatika maana wenzetu wanawasha hata mchana," alisema.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco wametaka jenereta hilo lirejeshwe kwenye ofisi zao zilizopo Kurasini.
  Mmoja wa wafanyakazi hao ambaye hakupenda jina lake litajwe kwa kuwa siyo msemaji wa shirika hilo, alisema Tanesco Kurasini wanapata shida kutokana na kuwa na jenereta moja lenye uwezo mdogo ambalo linahudumia kitengo cha malipo.

  "Si vibaya kwa mkurugenzi kuwa na jenereta, lakini siyo sahihi kwa shughuli za ofisi kusimama kutokana na kukosekana kwa huduma ya umeme, tena ofisi za Tanesco," alisema mfanyakazi huyo na kuunga mkono uamuzi wa POAC wa kutaka kuondolewa kwa jenereta hilo.

  Washindwa kutekeleza agizo la kamati
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  ni kawaida kwa hii nchi maagizo yanatolewa lakini hayatekelezwi na hili nadhani litakuwa limeishia hapo hapo. Bongo bwana magumashi tu.
   
Loading...