Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa wabunge jimbo la Arumeru Mashariki baada ya kutokea kifo cha muheshimiwa Sumari, lilijitokeza dosari moja kutoka kwa wanaojiita wazee wakimila wanaojulikana kama Washili kua hawatakubaliana na musheshimiwa Godbless Lema kufanya kampeni kwa mgombea wa Chadema kwakua alitoa maneno ya kashfa kwenye mazishi ya muheshimiwa Sumari ambayo kwao Washili hao wameona kitendo hicho kimewazalilisha.
Basi habari zinazoendelea hapa maeneo ya Usa River na vitongoji vilivyojirani na jimbo hili la Arumeru Mashariki ni kua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepata habari kua vizee hivyo vinavyojiita Washili ni usanii fulani kukwamisha juhudi za chama cha chadema kukosa nguvu kumbe vizee hivi vinatumia kinga hii ya kikwako kwakujiita wazee wa jadi huku wakipeleka nguvu kwa watoto wao wanaogombea kinyanganyiro hiki cha ubunge Arumeru Mashariki.
Mtakumbuka pia vizee hivi ndivyo vilivyotoa kauli na kuweka matangazo mji mzima wa Arusha kua watavunja chungu kwa wale woote waliohusika na sakata lile lililopelekea kwa kijana wao ambae ni mfanyabiashara maarufu aliyetumikia kifungo cha miaka mitano jela kwakile walichosema alihusika na mauaji yakutumia silaha na kupora madini ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia. Washili hawa walitaka waliohusika wajitokeze ili waombe msamaha ama sivyo watavunja chungu, lakini tukio hili likaishia hewani.
Chadema imeshashtukia njama hizi zinazoendelea kupitia kwa vizee hivi vinavyojiita Washili ili kukwamisha juhudi za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo lakini shime Chadema tusonge mbele! ALUTA CONTINUE!
jibu tuhuma za kwa nini lema alifanya uhuni na kusababisha fujo msibani
jibu tuhuma za kwa nini lema alifanya uhuni na kusababisha fujo msibani
Ndalo lugha uliyotumia siyo nzuri ukizingatia wazee hawa wamesha kanusha kukutana tendwa na wakaahidi kufanya kikao leo ili watoe tamko la nini cha kufanya pengine wakaamua kufikisha mahakamani tendwa...basi tusubili tamko lao ndiyo tuwalaumu au tuwapongeze ikumbukwe tuko kwenye kampeni ccm wanatumia njia yoyote kupunguza kura za chadema tuepuke kucomment kwa kukurupuka..
Mkuu akili zako ziko miguuni??? Wewe si ukaandamane Ubungo na wana magamba wenzio kumpinga JJ Mnyika!!!!!!!!hata bila hao wazee,lema hatumii busara kwenye mambo ya msingi
Kumbe Lema anawanyima usingizi Wameru?
Na inakuaje Washili haohao wakubali viongozi wengine wa Chadema watawakubali waende kumkampenia mshiriki wa Chadema lakini si Lema hapa ndipo napopata shida kujua ni nini kinawasumbua kuhusiana na muheshimiwa Lema.
Mkuu jana ulilala Shivaz au Picnic? Tumia lugha nzuri asee isije ikakurudi. Washili ni real deal, kama hauamini Kamuulize Kimaro(aliekuwa Mbunge Vunjo kwa ticket ya CCM), au waulize wale wazungu wa kule doli.
Kama kweli uko Arumeru embu nenda Akheri pale kanisani karibu kabisa na kwa Marehem Sumarri, uulize wale wazungu walozikwa pale ilikuaje? Na ni kwa order zipi?
Uliza habari za kina Askofu Kweka.
Mangi unakosea sana unapowaita Vizee, wape heshima yao. Tena angalia kauli yako isionekane kama msimamo wa chama chetu kipendwa. Au umetumwa na CCM nini?
Hiyo Usa-River ulosikia hizi habari ni usa-river ipi?
Crashwise,uliyoyasema ni kweli.Kimsingi Ndallo amekurupuka!
Samahani blaza....... hivi wewe ni mchga au?Nachofahamu kuhusiana na hapo kwenye RED kuhusiana na hao wazungu mliwaua halafu mkawazika halafu bado hamkurizika kama wamekufa mkawafukua halafu mkawafanyia Tohara! Hizi ndizo mila za Kishili sio?