Washauri kura zipigwe kwa njia ya mtandao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Washauri kura zipigwe kwa njia ya mtandao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Aug 31, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  TANZANIA imetakiwa kutumia mfumo wa kupiga kura kwa njia ya mtandao ili kupunguza vurugu zinazotokea wakati wa uchaguzi na malalamiko ya wizi wa kura. Rai hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Tume ya Sayansi nchini, Dk. Raphael Mmasi wakati wa kugawa zawadi kwa washindi wa shindano la ubunifu katika masuala ya kompyuta lililohusisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

  Dk. Mmasi alisema wazo hilo limetolewa na washindi wa nafasi ya tatu katika shindano hilo waliobuni mfumo utakaosaidia uchaguzi kuwa huru na kuwawezesha Watanzania wanaoishi nchi za nje kupiga kura. “Wazo la kutumia mfumo huu ambao unatumiwa na nchi za Ulaya, ni zuri na litasaidia kutatua tatizo la uchaguzi na tutatakaa na wadau ili tujadili na kuwasaidia,” alisema.

  Wakizungumza na gazeti hili, wanafunzi hao walisema waliobuni mfumo huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi ya viongozi na wananchi juu ya ucheleweshwaji na upotoshaji wa matokeo ya uchaguzi. Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ruth Swai alisema mfumo huo utasaidia katika upigaji kura, unarahisisha kuhesabu kura na kutocheleweshwa kwa matokeo. Alisema mfumo huo utasaidia kupunguza migogoro na malalamiko ya baadhi ya viongozi na wagombea wanaodai kuwa wanaibiwa kura na ucheleweshwaji wa matokeo.

  Naye Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Godfrey Magila, alisema kutakuwa na ulinzi katika kutumia mfumo huo na mtu ataruhusiwa kupiga kura mara moja kama ilivyo katika mfumo wa kawaida. Shindano hilo lilifanyika Agosti 6 hadi 8 mwaka huu na kuwashirikisha wanafunzi na wajasiriamali 54 ambao waligawanywa katika makundi, ambapo mshindi wa kwanza alipewa Dola za Marekani 400, wa pili dola 300 na wa tatu dola 200.

  HabariLeo
   
 2. k

  king11 JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanashauri hivyo waibe kura kama daftari la wapigakura limewashinda kulitunza
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tanzania bado sana kwenye mfumo wa mawasiliano ya kompyuta! Mfano tunaona kwenye kutumia simu kwenye matumizi kama vile kununua bidhaa!
  Luku leo siku ya tano watu wameshindwa kununua tunambiwa hamna network!
  sasa siku ya Uchaguzi wapiga kura wameisha piga halafu unasikia tangazo kutoka tume ya Uchaguzi kuwa network hamna tusubiri mpaka kesho. Kutakuwa na Uchaguzi tena hapo
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  labda iwe ina display kura through out the process ili kuwe na uanagalizi wa moja kwa moja. Hope Ngeleja, Malima na Jairo watakuwa waangalizi tu na si watendaji wa wizara ya Umeme
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama wanaopendekeza hivi wamefanya japo preliminary analysis vizuri.

  • Kwanza ni asilimia ngapi ya wapiga kura wna access na mtandao?
  • -Na katiko mfumo wanaotumia sasa tatizo kubwa ni nini? Je nii
   • idadi ya wapiga kura kuwa kubwa
   • wafanyakazi wa tume, kutoolewa taratibu na matumizi ya vifaa
   • wagombea wa vyama na wasimamzi wa vyama kukubali matokeo
   • mlolongo wa taribu za kisheria
   • Tume ya uchaguzi na mkurugenzi wa halmashauri
  • Mfumo mpya wa kutumia mtanda utayadress vipi matatizo haho hapo juu
  kwenye system development wataalam wanasema true problem ndio inatakiwa kutafutiwa suluisho sio suluisho litafute problem ya kutatua. Hii ya kupiga kura kwa mtandao itakuwa ni njia zile zile amabazo zimetumika kuanzisha computer system za taasisi nyingi Uachambuzi yakinifu unatakiwa. waifanya huo watagundua hata mfumo uliopo unaweza kufanya kazi vizuri kwa marekebisho madogo.

  Kwa hiyo kabla ya kukimbilia kutumia mtandao watafutwe system analyst wafanye tahamini what are true problem in the current system. Bil hivyo wataishia kunuanua vifaa vya kisasa kama walivyotumia uchagui ulipita kwa style copy and paste ya sehemu nyingine lakini bado sehemu nyingine vifaa hivyo ndio vikawa chanzo cha kuchelewesha.

  Matatizo yalipo kwenye uchaguzi ni sbabau watu hawataki kufuata computer systemd develoment process. So wanakuta coputer system inakuwa part of the problemand headche badala kuwa part of the solution.

  Nawasilisha.
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kama tanesco wanashindwa kumaintain mtandao unaowaingizia maelfu na maelfu ya hela tume ya uchaguzi itaweza kumanage zoezi la kupiga kura kwa mtandao?

  Watu huwaga wanaamka na hangover na kujisemea tu.

  Cheki tovuti yao, nenda: The National Electrol Commission of Tanzania - Homepage sioni chochote kuhusu uchaguzi mdogo wa Igunga
   
Loading...