Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
WASHAIRI MAPOKEO.
1)ni kweli tumeridhika,kwa kuishia kutunga.
Huku tukifurahika,kwa tungo twaunga unga.
Ama tunahuzunika,wa bara hata wa tanga.
Washairi mapokeo,mbona hatusongi mbele.
2)wenzetu wa mambo leo,wanazidi kutushinda.
Wanafungua na komeo,sisi ndo kwanza twadunda.
Nitaposhusha zomea,sitaki wakuniwinda.
Washairi mapokeo,mbona hatusongi mbele.
3)tumebaki kubanana,na sheria kuzitunga.
Wenzetu wanajichana,na kuviruka viunga.
Sisi kutwa twabishana,na tenzi kuunga unga.
Washairi mapokeo,mbona hatusongi mbele.
4)wanaivuka mipaka,na kufanya matamasha.
Mapokeo tunacheka,kama meno yanowasha.
Lini tutaja shituka,ushairi ni maisha ?
Washairi mapokeo,mbona hatusongi mbele.
5)tumebakia kughani,na kutuma tandaoni.
Twatungia radioni,sana ni zile za pwani.
Hii fani ya zamani,wengi waona utani.
Washairi mapokeo,mbona hatusongi mbele.
6)haya wale wabishani,njoni na zenu hoja.
Mkija kasirikeni,nitawaona vioja.
Ila vyema nijibuni,nasubiri na kungoja.
Washairi mapokeo,mbona hatusongi mbele ?
Shairi=WASHAIRI MAPOKEO.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.