Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
UPI MCHANGO WETU ?
1)wapo watakao bisha,kwani kawaida yao.
Wataona nawangusha,hili ni letu na lao.
Macho tunajipofusha,ama tuwaache wao.
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu.
2)ama tuwaache wao,wale waimba muziki.
Wajengao fani yao,kwa ala pia mikuki.
Sisi twasikiza zao,redio hiyo ni haki ?
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu.
3)Redio hiyo ni haki, zipigwe zao si zetu.
Ama kuna mamluki,wameviiba vya kwetu.
Tunandika habakuki,iwe kawaida yetu.
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu.
4)iwe kawaida yetu,tufanye iwe ni pesa
Hii ndo fani ya kwetu,bongo muvi inatesa.
Hipapu na bakulutu,mjini lanesanesa.
Washairi nauliza,uwapi.mchango wetu.
5)mjini lanesa nesa,godoro la madijei.
Mtego wamewanasa,hadhira wakijidai.
Hivi twaona anasa,tamasha likifurai.
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu
6)tamasha likifurahi,tuendeni majukwani.
Jamii tuisabahi,ituone hadharani.
Zingani tungo na rahi,iwe khabari mjini.
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu.
7)iwe khabari mjini,tuhameni tandaoni.
Tumebaki wasapuni,kama vile tu kapuni.
Ama twapikwa jikoni,semeni tusubirini.
Washairi nauliza,mwenye jibu sema kweli.
Shairi=UPI MCHANGO WETU
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
1)wapo watakao bisha,kwani kawaida yao.
Wataona nawangusha,hili ni letu na lao.
Macho tunajipofusha,ama tuwaache wao.
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu.
2)ama tuwaache wao,wale waimba muziki.
Wajengao fani yao,kwa ala pia mikuki.
Sisi twasikiza zao,redio hiyo ni haki ?
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu.
3)Redio hiyo ni haki, zipigwe zao si zetu.
Ama kuna mamluki,wameviiba vya kwetu.
Tunandika habakuki,iwe kawaida yetu.
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu.
4)iwe kawaida yetu,tufanye iwe ni pesa
Hii ndo fani ya kwetu,bongo muvi inatesa.
Hipapu na bakulutu,mjini lanesanesa.
Washairi nauliza,uwapi.mchango wetu.
5)mjini lanesa nesa,godoro la madijei.
Mtego wamewanasa,hadhira wakijidai.
Hivi twaona anasa,tamasha likifurai.
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu
6)tamasha likifurahi,tuendeni majukwani.
Jamii tuisabahi,ituone hadharani.
Zingani tungo na rahi,iwe khabari mjini.
Washairi nauliza,uwapi mchango wetu.
7)iwe khabari mjini,tuhameni tandaoni.
Tumebaki wasapuni,kama vile tu kapuni.
Ama twapikwa jikoni,semeni tusubirini.
Washairi nauliza,mwenye jibu sema kweli.
Shairi=UPI MCHANGO WETU
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.