Wasanii wanachokifanya ni ubaguzi

Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,733
1,646
Habari wakuu,

Kwa sasa kumeibuka wimbi la wasanii wengi kutunga na kuimba nyimbo za kumsifia na kumpongeza Mhe. Rais Magufuli. Siyo tatizo ni vizuri kumpongeza ili kumtia moyo Rais wetu kuendeleza mapambano.

Mimi binafsi naona kama ni wabaguzi na wanafiki, kwa sababu katika marais ambao walikuwa karibu na wasanii alikuwa ni Rais mstaafu Kikwete. Mara kadhaa amewaita Ikulu, aliweka tararibu za namna ya kulinda kazi zao na pia alitoa fedha kwa ajili ya kuwajengea studio. Lakini sijawahi kusikia hata wametunga nyimbo kumsifia kwa lolote zaidi ya kipindi chake waliweza kutunga nyimbo za kusisitiza kulinda muungano na umoja.
 
Jimmy George

Una uhakika kwamba hata Awamu ya JK hakuna Wasanii ambao waliwahi Kumuimba hadi Kumfagilia katika Nyimbo zao? Tafuta albums za bendi za Tam Tam iliyokuwa chini yake Muumini Mwijuma, Bendi ya TOT, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Wasanii wa Kufokafoka wa hii Miziki yenu ya akina Juma Nature, Kala Pina na wengineo kisha rudi hapa utupe mrejesho. Muwe mnafanya utafiti kabla ya Kukurupuka na Lawama zenu.
 
Una uhakika kwamba hata Awamu ya JK hakuna Wasanii ambao waliwahi Kumuimba hadi Kumfagilia katika Nyimbo zao? Tafuta Albums za Bendi za Tam Tam iliyokuwa chini yake Muumini Mwijuma, Bendi ya TOT, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Wasanii wa Kufokafoka wa hii Miziki yenu ya akina Juma Nature, Kala Pina na wengineo kisha rudi hapa utupe mrejesho. Muwe mnafanya utafiti kabla ya Kukurupuka na Lawama zenu.
Wewe unayezijua hizo nyimbo hebu zitaje!!
 
Una uhakika kwamba hata Awamu ya JK hakuna Wasanii ambao waliwahi Kumuimba hadi Kumfagilia katika Nyimbo zao? Tafuta Albums za Bendi za Tam Tam iliyokuwa chini yake Muumini Mwijuma, Bendi ya TOT, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Wasanii wa Kufokafoka wa hii Miziki yenu ya akina Juma Nature, Kala Pina na wengineo kisha rudi hapa utupe mrejesho. Muwe mnafanya utafiti kabla ya Kukurupuka na Lawama zenu.
Usiongelee kutajwa kwenye wimbo mtoa mada anaongelea wimbo mzima atungiwe yeye asifiwe km huyu wa sasa!
 
Diamond ana wimbo, Nikki Mbishi ana wimbo, miziki ya bendi ina wimbo nimesaha jina la bendi. Fanya uchunguzi kabla ya kuleta mada.
 
Back
Top Bottom