Wasanii walivyoboronga nyimbo za maombolezo

Nimesikiliza nyimbo za maombolezo za msiba wa John Pombe Magufuli zaidi ya 100

Msanii wa pekee alieweza tengeneza HIT ni PETER MSECHU.

Katoa melody (ala) ya pekee na mashairi safi yanafariji, yanaenzi pia, yanaburudisha, yanatia moyo, yana enzi.

Haihtaji kuimba kwa huzuniiii kama unalia ndio uwe Mwanamuziki, au uoneshe ni wimbo wa maombolezo, pengine ndio maana wasanii wengi nyimbo zimekuwa za kawaida, nyingine hata hutaki kusikiliza kabisa. OVYO

Ukimtoa Msechu na wimbo wake "Umetuacha salama", ni kipande Cha Christina Shusho alichoimba "Umeenda, umeenda baba" kwenye wimbo wa wasanii wengi wa aoina Diamond, Ndio Bora, ingekuwa ni wimbo binafsi ingekuwa Hit Pengine. Zilizobaki duh. Ni miborongo tu

Lakini pia Wimbo wa MSECHU ndio wimbo wa kwanza kabisa wa maombolezo kutoka lakini umekuwa HIT, jamaa katembea na melody kwa namna ya pekee juu ya mashairi yake ya kawaida tu lakini HOT

Nimemkumkumbuka Kepten Komba. Wanamuziki ni wachache sana Tanzania. Ukiondoa leo studio za kisasa za kuingiza sauti na ku modify hatuna wanamuziki, wengi ni wasanii tu kama Bongo Movie

Eko Msechu.
Watu wenye matumbo na miili mikubwa sijui kwann wamebarikiwa sana kuimba.
 
KAMA HUJASIKILIZA WIMBO WA PETER MSECHU NAKURUHUSU UPINGE TU... LAKINI TULIOUSIKILIZA NDO WIMBO BORA SANA UNAENZI,UNAFARIJI,UNABURUBISHA LAKINI PIA UNAHUZUNISHA SANA..
MAGUFULI NENDA SALAMA KAZI UMEIMALIZA.......
 
Hivi umeiskiza track ya p mawenge "mavumbini"?
 
Hivi umesikiliza Badae ya Lavalava

Moja ya vesi anasema
Viwanda mandege Mabombadia mbona wewe hujayatumia Baba,
Aisée siyo siri huu ubeti huwa unaniliza sana
 
Nimesikiliza nyimbo za maombolezo za msiba wa John Pombe Magufuli zaidi ya 100

Msanii wa pekee alieweza tengeneza HIT ni PETER MSECHU.

Katoa melody (ala) ya pekee na mashairi safi yanafariji, yanaenzi pia, yanaburudisha, yanatia moyo, yana enzi.

Haihtaji kuimba kwa huzuniiii kama unalia ndio uwe Mwanamuziki, au uoneshe ni wimbo wa maombolezo, pengine ndio maana wasanii wengi nyimbo zimekuwa za kawaida, nyingine hata hutaki kusikiliza kabisa. OVYO

Ukimtoa Msechu na wimbo wake "Umetuacha salama", ni kipande Cha Christina Shusho alichoimba "Umeenda, umeenda baba" kwenye wimbo wa wasanii wengi wa aoina Diamond, Ndio Bora, ingekuwa ni wimbo binafsi ingekuwa Hit Pengine. Zilizobaki duh. Ni miborongo tu

Lakini pia Wimbo wa MSECHU ndio wimbo wa kwanza kabisa wa maombolezo kutoka lakini umekuwa HIT, jamaa katembea na melody kwa namna ya pekee juu ya mashairi yake ya kawaida tu lakini HOT

Nimemkumkumbuka Kepten Komba. Wanamuziki ni wachache sana Tanzania. Ukiondoa leo studio za kisasa za kuingiza sauti na ku modify hatuna wanamuziki, wengi ni wasanii tu kama Bongo Movie

Eko Msechu.
Peter msechu ndio kafunika, nyimbo mbili very touchy na mpangilio wa kiakili.
 
Aslay alijitahidi kuimba mwanachato,Aly kiba naye sio mbaya sana wengine ni peter msechu cover ya ekueme na magufuli nenda....wengine ilikuwa ushuzi tu...kama kina diamond hakuna kitu
 
Back
Top Bottom