Wasanii walivyoboronga nyimbo za maombolezo

Wasanii walivyoboronga nyimbo za maombolezo

Dumelang

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
3,267
Reaction score
5,854
Nimesikiliza nyimbo za maombolezo za msiba wa John Pombe Magufuli zaidi ya 100

Msanii wa pekee alieweza tengeneza HIT ni PETER MSECHU.

Katoa melody (ala) ya pekee na mashairi safi yanafariji, yanaenzi pia, yanaburudisha, yanatia moyo, yana enzi.

Haihtaji kuimba kwa huzuniiii kama unalia ndio uwe Mwanamuziki, au uoneshe ni wimbo wa maombolezo, pengine ndio maana wasanii wengi nyimbo zimekuwa za kawaida, nyingine hata hutaki kusikiliza kabisa. OVYO

Ukimtoa Msechu na wimbo wake "Umetuacha salama", ni kipande Cha Christina Shusho alichoimba "Umeenda, umeenda baba" kwenye wimbo wa wasanii wengi wa aoina Diamond, Ndio Bora, ingekuwa ni wimbo binafsi ingekuwa Hit Pengine. Zilizobaki duh. Ni miborongo tu

Lakini pia Wimbo wa MSECHU ndio wimbo wa kwanza kabisa wa maombolezo kutoka lakini umekuwa HIT, jamaa katembea na melody kwa namna ya pekee juu ya mashairi yake ya kawaida tu lakini HOT

Nimemkumkumbuka Kepten Komba. Wanamuziki ni wachache sana Tanzania. Ukiondoa leo studio za kisasa za kuingiza sauti na ku modify hatuna wanamuziki, wengi ni wasanii tu kama Bongo Movie

Eko Msechu.
 
Kasikilize nyimbo ya Aslay wa maombolezo kisha uje u edit tena
 
Pia weka Wimbo wa Rosa ree nafasi ya pili
 
Mkuu Hata Mimi Nilijipa Muda Kusikiliza,Kiukweli Msechu kwa Hili Nimempa Kongole.
 
The fact kuwa ni wimbo mzuri ila kakopi kutoka nigeria ,
 
Nataman Christina Shusha angefanya tu wimbo wa peke yake....
 
Sasa mtu atoe his/her best work kwa kitu cha msimu ?

Jamani hizi kazi ngumu sio kama tu kuweka mchanga na cement kwenye mashine ya tofali na kukandamiza tofari linatoka...

Cha maana wabadilishe badilishe baadhi ya nyimbo zao siku akiondoka mwingine wanabadilisha tena (kwani TOT wapo wapi hii ndio ilikuwa kazi yao)
 
Kasikiliza pia wa shusho "tutakukumbuka daima" ni wimbo mzuri sana na binafsi ndo niliupenda japo kautoa kwa kuchelewa

Achana na collabo na kina Diamond
 
Sasa mtu atoe his/her best work kwa kitu cha msimu ?

Jamani hizi kazi ngumu sio kama tu kuweka mchanga na cement kwenye mashine ya tofali na kukandamiza tofari linatoka...

Cha maana wabadilishe badilishe baadhi ya nyimbo zao siku akiondoka mwingine wanabadilisha tena (kwani TOT wapo wapi hii ndio ilikuwa kazi yao)
Komba alipokufa na TOT nayo ilikufa.
 
Tangu nione hizi nyuzi za kuhusu nyimbo lazima nione umeguswa wakina Mond "ukiacha ule" "sio ule"....
 
Wewe ndo Peter Msechu uliyeiba melody ya wimbo wa Ekueme halafu unakuja hapa kujisifia?
Unajitia aibu... Umeambiwa wimbo wa nenda salama... Ni wimbo wake wakwanza anasema Kautunga mwenyewe.. sio.. achana na ekueme.
 
Back
Top Bottom