Wasanii wa kibongo kweli mbumbumbu

kukumdogo

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
2,766
2,523
Nimepewa taarifa kwamba wasanii wengi wa kibongo ni mbumbumbu ndo mana wanaibiwa sana kazi zao na kuishia kulipwa hadi elfu kumi kwa kazi anayofanya hii ni kweli nije kuwekeza bongo!?
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
wangekuwa na akili kidogo tu wasingemuunga mkono JK ambaye ameongeza idadi ya masikini nchini ambao kwa namna moja au nyingine wamekata mauzo yao ya CD.
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
wasanii wetu kwa kweli hawana uelewa achana na shule ila wanatakiwa wabadilike sana
 
AirTanzania

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
1,139
1,032
Nimepewa taarifa kwamba wasanii wengi wa kibongo ni mbumbumbu ndo mana wanaibiwa sana kazi zao na kuishia kulipwa hadi elfu kumi kwa kazi anayofanya hii ni kweli nije kuwekeza bongo!?

Sasa unataka kuja kuwekeza kwa wasanii wanaotumia Masaburi kufikiria, Wasanii wanojikomba kwa Mafisadi kama Kikwete. Wasanii wanaovaa Majaketi kwenye Joto, Wasanii wanaoshindia Mohogo ya kukaanga kutwa nzima, Wasanii wengi wa bongo naojipendekeza kwenye kampeni za CCM kwa kufuata Kofia, Khanga na Pilau, njaa ndio zinawasumbua

Na wewe unataka kuwekeza kwao wao au kwa ajili ya chaguzi za CCM? upo Tayari kupokea Kofia, Khanga na kula Pilau za CCM? Uchagazi ukiisha na wewe unatupwa na CCM mpaka Chaguzi nyingine
 
Pdraze

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
616
321
Wajinga watupu wale wanainvest kwenye mademu na njaa zao zisizoisha wanatumiwa na ccm kwa kupewa tshirt na hela kidogo tu af yanakurupuka na kuwadanganya ndugu zetu vijijini mi yananikera eti mtu kama fid q unamkuta kavalisha linguo la kijani anasifia chama..jinga
 
figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
19,596
24,125
mabovu,d knob,karapina wangekuwepo kwenye ule wimbo wa uhuru ningewadharau sana.roger
 
Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,236
4,041
Ukiongelea sanaa ni pana sana. Kuna wasanii wengi sana wamepata maendeleo kutokana na kazi zao.
Sanaa Tanzania inakuwa kwa kasi. Vijana wengi wamejiajiri kutokana na sanaa na wamepata maendeleo.
Tunaweza tukawasample wasanii wa maigizo kama akina Kanumba na Ray, Ze Comedy! Wote hawa wana maendeleo.
Kwenye muziki pia unaweza ukawaona kama akina Lady Jd, Mrisho na wengine wengi wamenufaika sana kutokana na kazi zao
 
MwafrikaHalisi

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
1,742
509
Wajinga watupu wale wanainvest kwenye mademu na njaa zao zisizoisha wanatumiwa na ccm kwa kupewa tshirt na hela kidogo tu af yanakurupuka na kuwadanganya ndugu zetu vijijini mi yananikera eti mtu kama fid q unamkuta kavalisha linguo la kijani anasifia chama..jinga

Ilitokea wapi hiyo, au ni mfano tu wa kufikirika?
 
Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,712
1,244
Sijui maendeleo mnayosema ni yapi? Naona kama mnaponda CCM na wasanii wanashiriki kampeni za CCM. Anyway wasanii wachache bado hajafika pick ya kupata hela, wengine tayari wanakula matunda ya kazi zao. Wezi ni sisi tunaoiba kazi zao baada ya kwenda kununua CD unaenda kuburn bila hata aibu.

Ebu elimikeni wananchi acheni wizi wa kimacho!
 
mwacheni77

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
763
209
Nimepewa taarifa kwamba wasanii wengi wa kibongo ni mbumbumbu ndo mana wanaibiwa sana kazi zao na kuishia kulipwa hadi elfu kumi kwa kazi anayofanya hii ni kweli nije kuwekeza bongo!?
Swali lako tata sana na ndio maana hakuna aliyekujibu kukizi mahitaji yako wote wameweka chuki na itikadi za vyama,unataka kuja kuwekeza kwa sababu mambumbumbu ili uendalee kuwaibia au unataka kuja kuwekeza ili uwakomboe kutoka kwenye kuibiwa?
 
Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,610
6,274
wasanii wa bongo shenz.i zao wapuuzi sana,wao ni wanyenyekevu kwa mafisadi.hivi mbona Obama hakuwatumia 50 cent,jay z,niki minaj au drake kumpigia kampeini? Wasanii wa huku wapuuzi sana..
 
jouneGwalu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,683
1,724
Nimepewa taarifa kwamba wasanii wengi wa kibongo ni mbumbumbu ndo mana wanaibiwa sana kazi zao na kuishia kulipwa hadi elfu kumi kwa kazi anayofanya hii ni kweli nije kuwekeza bongo!?

Kama we ni mgeni kabisa wa music industry hapa home!
Huu mziki umegawanyika katika namna ambavyo watu wanavyoutazama na harakati zake!
Kuna kundi kama hili hapa chini.......
Wengi wenye mtazamo huu ndio wale "wadau wakuu" na wapo karibu na watawala na ndio wenye ushawishi sana kwenye mambo ya muziki...
Ninaweza kusema "wadau" hawa wanaongozwa na "Ruge Mutahaba" katika kushughulikia mambo mengi tu ya kiburudani...!

Ukiongelea sanaa ni pana sana. Kuna wasanii wengi sana wamepata maendeleo kutokana na kazi zao.
Sanaa Tanzania inakuwa kwa kasi. Vijana wengi wamejiajiri kutokana na sanaa na wamepata maendeleo.
Tunaweza tukawasample wasanii wa maigizo kama akina Kanumba na Ray, Ze Comedy! Wote hawa wana maendeleo.
Kwenye muziki pia unaweza ukawaona kama akina Lady Jd, Mrisho na wengine wengi wamenufaika sana kutokana na kazi zao

Kuna upande mwingine ni wa wanaharakati ambao hawaridhiki na namna soko la muziki linavyoendeshwa,
Kuna madai kadhaa ya kuitaka serikali irasimishe shughuli hii ili iweze kupata mapato zaidi na wasanii pia wawe nanguvu zaidi katika kazi zao...
Kundi hili linaonekana kuongozwa na Joseph mbilinyi aka SUGU, ila kuna wadau huru amabo hawafungamani na upande wowte ila wanatamani hali iboreshwe zaidi kisheria na kisera (sera nzima ya sanaa)

Kazi kwako mkuu, unataka kuingia kwa kupitia mlango gani kati ya hiyo...
Kwa ujumla music ni biashara ngumu sana kwa hali ya sasa hapa home.....
KARIBU.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom