Mkereketwa_Huyu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 10,588
- 7,965
Naomba kuuliza, hivi ni kwa nini ma dj wetu wanapenda kupromote vitu vya kijinga kama bongo fleva na kuubatiza kuwa muziki wetu? Kwa sasa karibia kila mmoja hapa Tanzania anajuwa kuwa huu muziki uko sampled (copied) from other artists, kinachofanywa tu ni kutia sauti na kutoa redioni. Kwa mpangilio huu, mtu kama Diamond, Linah, Mwasiti, Mr. Ble, na wengine feki hivi wanastahili kuitwa wanamuziki kweli? Utashangaa wanalilia kazi zao zilindwe na serikali kwa jasho gani wanalotoa kujituma kupiga vyombo na kupanga muziki? Yaani wanalilia serikali iwalindie kazi zao wakati ki uhalali si zao wameziiba kwa wasanii wengine, inawezekana kweli? Huu muziki unafaa kuimba uchochoroni ama kuwaimbia walevi baa maana hauna tofauti na anayeimba karaoke baa ama shereheni. Ma-dj wetu wacheni kupokea rushwa za wasanii na kuwabeba, huu si muziki katika jamii yetu na unatakiwa kupigwa marufuku mara moja!