Wasanii wa Bongo, ubunifu ndio tatizo

Wasanii wa Bongo, ubunifu ndio tatizo

nanya

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2016
Posts
672
Reaction score
523
Habari wana JF.

Nimeona niwasilishe hili dukuduku langu kwenu tulichambue ili tujue tunawasadiaje hawa wasanii wa Bongo Movies. Hawa watu mara nyingi huwa wanatengeneza filamu zenye jumbe zinazofanana, kama filamu haihusu mapenzi basi inahusu ujambazi, hapo ndio ukomo wao wa kufikiria ulipofika.

Kwanini wasiwe wabunifu na kusoma vitabu vya historia ili mwisho wa siku watengeneze movie kutokana na hio historia? Kwa mfano historia ya Tanzania kabla na baada ya ukoloni inapaswa ielezewe kwa vitendo na ikiwezekana mwisho wa siku itumike hata mashuleni kufundishia na ukiangalia historical sites yani makumbusho tunayo ya kutosha kwa ajili ya kuigizia movies za kihistoria, sasa tatizo ni nini? Hebu wawe wabunifu na kuwaza nje ya boksi sababu sasa hivi filamu za kibongo zimepoteza soko.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom