Wasanii wa bongo movie msichekelee kuhusu tamko la jeshi la polisi

Ng'egera

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
766
419
Wasalaam wanajf
Hivi karibuni nimemsikia kamanda Wa jeshi la polisi akitoa tahadhali na muda kuhusu kusitisha usambazaji Wa mikanda ya filam za nje ili kulinda soko la wasanii wetu.

Nafikili kwa wazo hili wasanii wangelipinga sana kwani linawadhalilisha ya kwamba hawawezi kuigiza ndio maana hawana soko mpaka serikali iingilie kati

Suluhisho :Serikali isingezuia ila ingewapa usaidizi tasnia hii ya uigizaji ili iboreshe kazi zake na kupendwA moja kwa moja na watazamaji badala ya kutumia ubabe
Angalizo: Unaweza kumpeleka ng'ombe mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji
 
Ndugu tatizo mnalipoti vibaya ili uonekane unachokiongea kipko sahihi,wanasema watazuia mikanda yote kutoka nnje ambayo haifuati utalatibu kama kupitia cosota ,yra na nk hivi hujihurumii hata wewe soko moja mnatengeneza bidhaa moja mwenzio halipi kodi wewe unalipa kodi unaweza kumshinda kweli huyu kibiashara?
 
Tatizo la kushuka au kufa kwa soko filamu Za kibongo mchawi wala sio filamu Za nje kama inavyozungumzwa na watu.... 1.Mchawi ni wasanii wenyewe kutokuwa na chombo cha kukagua filamu hii imepelekea kila mtu anayejisikia anafanya filamu anapeleka sokoni Haya yamepelekea kazi mbovu ambazo hazina viwango wala ubora kuingia sokoni kwa wingi na hatimaye mlaji kuchoka na kuamua kugeukia upande mwingine 2. wasanii kujiingiza kwenye siasa na kutoa kashifa kwa watu mbalimbali bila kujua kama wanajiharibia kwenye tasnia yao ...ni ngumu na haitokuja kutokea filamu kurudi kama zamani... Yaani unaenda kwa muhindi unauza filamu yako 20-25m tena hiyo nazungumzia msanii wa level za Kati hao wanaojiita masuper star walikuwa wanauza mpaka 35-40m leo... Kutokana na madudu mengi waliofanya bongomovie ni ngumu kumbadirisha mtazamani arudi kuangalia filamu Za kibongo
 
Ndugu tatizo mnalipoti vibaya ili uonekane unachokiongea kipko sahihi,wanasema watazuia mikanda yote kutoka nnje ambayo haifuati utalatibu kama kupitia cosota ,yra na nk hivi hujihurumii hata wewe soko moja mnatengeneza bidhaa moja mwenzio halipi kodi wewe unalipa kodi unaweza kumshinda kweli huyu kibiashara?
Achilia mbali kodi watu wamechoka na kazi mbovu ambazo hazina ubora stori za kuungaunga na mambo mengi machafu wanayofanya hao waigizaji
 
Nina mda sana sinunui cd nadownload tu movie nizipendazo na kwa ubora niutakao.
Kuusu kuzuia filam za nje me naona wanazuia tu ugali wa watu ambao walikuwa wamejiajiri barabarani wakiuza cd.
Hao bongo movie wawe serious na tasnia yao watu tutanunua. Hakuna atakaependa kitu kibovu.
 
Wasalaam wanajf
Hivi karibuni nimemsikia kamanda Wa jeshi la polisi akitoa tahadhali na muda kuhusu kusitisha usambazaji Wa mikanda ya filam za nje ili kulinda soko la wasanii wetu.

Nafikili kwa wazo hili wasanii wangelipinga sana kwani linawadhalilisha ya kwamba hawawezi kuigiza ndio maana hawana soko mpaka serikali iingilie kati

Suluhisho :Serikali isingezuia ila ingewapa usaidizi tasnia hii ya uigizaji ili iboreshe kazi zake na kupendwA moja kwa moja na watazamaji badala ya kutumia ubabe
Angalizo: Unaweza kumpeleka ng'ombe mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji
Filamu ya mwisho kuiangalia ya Bongo movie ni Gate Keeper hii ya Ray ambaye ndiyo kaishabikia hii, mnajua huyu jamaa ni mbishi sana. Filamu nilichokiona ni rangi nzuri za video kama vichupa vya wasanii wa Bongo fleva. Story ya filamu hakuna kitu na Director hakuna, unajua huyu jamaa alishaambiwa kuwa director hapamfai ila anakumbatia tu. Nimeona sehemu Kajala anapigwa yaani wapigaji kama wanatomasa ngano, hii action Director alikuwa wapi?

Haitoshi story imepangwa hovyo, haya makosa kila siku wanaambiwa na wanarudia yaleyale tu. Sasa huyo mtazamaji ataachaje kuangalia za kigeni kama kila siku mnarudia kitu hichohicho mnachokosea. Nilichogundua ubovu wa filamu za bongo si teknolojia bali ni uzembe wa Director, ubovu wa story na watu kubeba majukumu wasiyo na taaluma nao. Tanzania wapo wabobezi wa filamu chuo kikuu cha Dar es salaam, kuna Professa pale aliwahi kuigiza filamu ya kimarekani na pia Director mkubwa. Huyu wanamwacha na kujitwalia wao madaraka tu, wenzao hizo kazi wanaingia darasani.

Haya wamekataza Dar ambapo watazamaji wa filamu za nje za kutafsiriwa ni wachache, vipi huko mikoani walipojaa itakuwaje? Hapa ni kucheza tu hakuna jingine, kama ni shimo la panya wameziba kwa mkate.

Dawa ni kuboresha kazi zao tu, kutumia nguvu maana yake wameshindwa sokoni. Watu watadownload tu, pia Vibaka wataongezeka tu maana unaharibu ajira ya mtu.

Sirro na Makonda nao wamebugi, wajiandae kupokea ongezeko la wizi jijini.
 
Achilia mbali kodi watu wamechoka na kazi mbovu ambazo hazina ubora stori za kuungaunga na mambo mengi machafu wanayofanya hao waigizaji
Hoja ya msingi mbona huijibu mnafanya biashara ya aina moja wote na sehemu moja ila mwenzako halipi kodi zote we unalipa hivi unaweza kushindana naye huyu,kuhusu filamu siyo kweli zote ni mbovu zipo nzuri ambazo watu wanazifurahia,hata zhizo za nnje zipo ambazo unaweza kuangalia na usizifurahie,jibu swali la msingi hilo la mwanzo
 
Kiufupi hatuwataki....
 
aise sikumbuki mara ya mwisho kuangalia Bongo movie ni linii kama sio awamu ya kwanza ya kikwete......maana hata nikisafiri kwenye basi wakiweka bongo movie huwa napatwa na usingizi mzitoo..

kiufupi Bongo movie hazivutii yaan hata wakizuia hizo za nje ni kama kuwanyima fursa vijana waliokuwa wamejiajiri barabarani kuuza Cd zao
 
Watu wenye akili kubwa wanashindana kwa hoja kusema tu huwataki wakati nao wanauhuru wa kudai haki yao ni kuonyesha kiwango cha akili yako
Bila Shaka wewe utakuwa mmoja wao... Waambie WENZIO msiturazimishe kuangalia bongomovies hela zetu wala hakuna aliyesaidia wakati tunazitafuta....
 
Naomba unijibu maswali haya machache kama utaweza.

1.Nini kiliuwa soko la movie za Kinaijeria ambazo zilikuwa zinaangaliwa sana hapa nchini!?

2. Nini kiliuwa soko la muziki kutoka Kongo!?

3. Nini kimeua soko la muziki Wa dansi la akina Twanga na wenzao!?

4. Bongo fleva ilipoanza wasanii wake walipigania miziki kutoka nje kuzuiwa ili wasikilizwe wao tu.?

Mimi naamini kila zama zina changamoto zake. Kama Nigerian movie zilivyochokwa hata bongo movie imeshachokwa, msitafute visingizio. Kwa sababu bongo movie iliibuka hizo movie zikiwepo na ilifanya vizuri. Leo imeanza kushuka ndio mnatafuta visingizio!?

Hoja ya msingi mbona huijibu mnafanya biashara ya aina moja wote na sehemu moja ila mwenzako halipi kodi zote we unalipa hivi unaweza kushindana naye huyu,kuhusu filamu siyo kweli zote ni mbovu zipo nzuri ambazo watu wanazifurahia,hata zhizo za nnje zipo ambazo unaweza kuangalia na usizifurahie,jibu swali la msingi hilo la mwanzo.

Mwisho naomba niongezee changamoto nyingine ni mabadiliko ya teknolojia. Ujio Wa ving'amuzi umewapa watazamaji wigo mpana zaidi Wa kuona channel nyingi za movie na matukio mengine. Kwa hiyo ni wazi muda na fedha ambayo ingetumika kununua bongo movie lazima imegwe.
 
Cha kuongezea, ujio Wa ving'amuzi nao umechangia maumivu kwa bongo movie. Zamamni mtu akiangalia TV za hapa nchini akiona program hazina mvuto anapata ushawishi Wa kuangalia japo movie moja ya bongo . sasa hivi MTU ana utittiri Wa channel kwenye decoder tena channel za moviee kali mpya. Unadhani ataikumbuka bongo movie tena hapo!?
 
Back
Top Bottom