Vyama vingi Tz vina karibu miongo miwili sasa tangia kupitishwa na kutambuliwa kisheria, sijui labda wewe unaona vinaendana na maendeleo ya kiuchumi ???. Hongera kwa kuona vitu ambavyo sie wengine HATUVIONI.
Halafu hapa hatuzungumzii UTUMWA ule wa forced labor n.k, tunazungumzia uhuru wa watu kutoa maoni. Kaa ni forced labor ukiichambua unaeza kuta hata mtumishi wa serikali ni forced labor vilevile.
Again,
FVCK THIS STUPID 'DEMOCRACY'!
Demokrasia na uhuru wa kiuchumi ni vitu vinavyoenda pamoja, kama una sehemu ambapo demokrasia na uhuru wa kiuchumi vinaweza kusigizana, kuvioanisha viwili hivi kutakuwa ni rahisi zaidi kuliko kuleta mfumo usiofuata demokrasia.
Mi nadhani kuliko huu tulionao natamani nilio highlight
Waacheni vijana wafanye biashara bana, kwani kama CCM wamewatumia (kibiashara) ili kuhamisisha watu kuwachangia kuna ubaya gani? Si ndo kazi yao?
Hata vyama vingine vikitaka kuwatumia hao wasanii, naamini watakubali kwa sababu hayo ndo kazi zao eti. Watu wanaowalaumu hawa wasanii sijui kama wao wangekuwa na bidhaa au huduma ya kuwauzia CCM wangekataa!
Waachane vijana waendeshe maisha yao bana.
Nilisema,
Maana yake ingawa demokrasia ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi, si lazima kila mara demokrasia ipalilie maendeleo ya kiuchumi.
Naelewa kuna kusigizana kati ya demokrasia na maendeleo ya kiuchumi.Ndiyo maana nikakwambia "kama kuna sehemu ambapo demokrasia na uhuru wa kiuchumi vinaweza kusigizana, kuvioanisha viwili hivi kutakuwa ni rahisi zaidi kuliko kuleta mfumo usiofuata demokrasia.
Kama umeelewa kwamba nimemaanisha Tanzania kuna "maendeleo ya kiuchumi" kwa sababu kuna demokrasia, hujafanya comprehension ya maandishi yangu. Kwanza one can argue hata democracy Tanzania hatuna.
Hebu tuache abstracts kidogo tuangalie mifano.
Mimi naangalia nchi za BRIC (Brazil, Russia, India, China) na maendeleo yake ya kiuchumi. Hususan India na China. Kuna case inakuwa advanced kwamba China inaweza kupiga hatua kubwa kiuchumi kwa sababu haifuati demokrasia, kwa sababu bureaucrats wa Kichina hawana lengthy processes za kufuata, wakiamua wameamua, wakitaka kujenga barabara na power plants hakuna lengthy environmental studies na parliamentary hullaballoo. Kuna watu wanasema hii ni advantage kwa China ambayo a noisy democracy like India could never afford.
But I believe this is only true if you are focused on short term goals, kwa sababu ukienda kwenye long term picture utakuta hii hii advantage ya kuharakisha vitu kwa mfano, inabeba rushwa na environmental risks just to mention a few factors.System ina lack transparency. Na ukweli ni kwamba, wachina wakishakuja kuwa affluent en masse watadai demokrasia tu.Kwa hiyo utaona demokrasia na economic prosperity vinaenda hand in hand.
The debate on whether to postpone political freedom in order to first attain economic freedom - the reverse of that Nkrumah adage- or adopt Nkrumah's "Seek ye political freedom and everything shall be added", is a delicate and philosophical one.
The Chinese embrace economic freedom and gradual political freedom (some say the Communist party is just manouvering to stay in power as long as it can). The Indians, by virtue of their history and colonial legacy, work with political freedom at the expense of instantly gratifying their economic desires.
Mimi naona China hawana jinsi ila ku gradually democratize, ama sivyo wata face economic na political catastrophies ambazo zitafanya Tiananmen Square massacre iwe kama mchezo wa watoto. Tayari kuna minong'ono kwamba China ina respond kwa pressures za kuitaka ii float Yuan.
Tayari tunaona dissent ambayo haikufikirika hata miaka mitano tu iliyopita. Economic prosperity ina wa empower watu kutaka democracy zaidi. Tatizo tunapoikandya democracy tunaangalia our very narrow brand of it, which is really more of electocracy than democracy, kwa sababu huwezi kuwa na democracy halisi kama wananchi hawana elimu, na hata hizo elections zenyewe ziko questionable.
Kwa hiyo ili kuikandya democracy, inabidi uiqualify demokcacy gani. Na ukiiqualify utakuta unakandya some brands of it.Hata dini kuna some brands za ajabu.
Unless you are going to pull a Menckean critique of democracy hapa, nitaona disillusioned POV yako imetokana na failure ya watu kuimplement democracy, na si democracy yenyewe.
Either that or you are turning yourself into the last bastion of the Nazi laughingstock this side of the last 100 years.
Binafsi sikulitegemea hili kufanywa na kijana yoyote mwenye umri chini ya miaka 40. Ni miaka zaidi ya 50 toka nchi yetu ipate uhuru lakini bado majority ya watanzania tumetopea kwenye lindi la umasikini uliovuka kipimo cha utu. Hii yote imesababishwa na serikali mbovu, dhaifu na isiyo na mipango madhubuti ya kuleta maendeleo katika taifa letu.
Binafsi, sikumbuki kama nilishawahi kuvaa ama kushika ama kusogea karibu na either bendera ama Tshirt ama khanga ama skafu ama chochote kile kinachohusiana na CCM hata kwa kupewa pesa, pombe na pilau za bure.
Je hawa vijana wanajua wanachokifanya?
Je nyimbo zao za kulaumu utendaji kazi wa serikali ya CCM hasa katika masuala ya Rushwa na ufisadi zina maana gani kama leo hii wanashiriki ku support serikali mbovu iendelee kutawala?
Au ni njaa inayowafanya washiriki kwenye hizi kampeni?
Au hawajui walifanyalo??
Cheki picha hizo hapo chini.........
Wasanii nyota wa bongo fleva wachangia CCM
![]()
Profesa J
msanii au mwandishi akiwa CHADEMA anapongezwa na akiwa CCM analaumiwa........!
we are not giving equal and fair grounds on this.....WANAPOKUWA CCM TUWAPONGEZE PIA KWA KUJIWEKA WAZI NA BAYANA.....! MBONA ADEN RAGE NI CCM? MBONA DALALI NI CCM.....!
kuhusu blog ....ikitoa habar za CHADEMA inakuwa poa na ikitoa habari za CCM ni kibaraka.....is JF CHADEMA BRANCH?
Eti huyu ndiye alitunga na kuimba wimbo wa 'NDIYO MZEE'!!! naye sasa anasema 'NDIYO MZEE' ...Aibu kwako Joseph Haule.
Majority ya wasanii wa Tz hawana ELIMU ya kutosha wala UPEO wa kutosha kuwa na INDEPENDENT IDEAS. Hivyo wanakuwa manipulated.
Hivi sasa wanatumiwa tu na wanasiasa. Wananunuliwa kwa VIPANDE 30 VYA FEDHA.
Msishangae baadaye mkasikia wanamichezo akina Mussa Mgosi, Mrisho Ngassa, Juma Kaseja nao wakakusanywa na kutangazwa kihivyo kuwa wamechangia CCM.
La muhimu ni WANANCHI KUTAMBUA WANACHOKIHITAJI, na kamwe SIYO KUWASIKILIZA HAO WASIO NA UPEO.
Acheni hizo bana.......Pia acheni kuwadharau hawa wasanii kuwa hawana upeo...Kosa lao lipi hapa kwani?,kuwahamasisha wananchi waichangie CCM ama?.....Vipi wangeonekana wakiwahamasisha wananchi waichangie CHADEMA,CUF,UDP,NCCR ama CCJ....bado mngewaita hawana upeo?????...Cmon
Kumbuka kwamba Tanzania ni nchi ya Kidemokrasia na kila mtu anao uhuru wa kushabikia,kusaidia ama kujiunga na chama chochote akitakacho mradi tu havunji sheria....Hawajafanya kosa lolote hapa,ni haki yao,wanao uhuru bana....Ni sawa na kesho usikie mwanamuziki fualni anahamasisha wananchi waichangie CHADEMA,CUF,CCJ n.k,hatakuwa amefanya kosa.......ni haki yake kikatiba...........Tusiwaingilie uhuru wao hata kidogo
Pia unapaswa kufahamu kwamba hao wanamuziki wapo kibiashara zaidi......Hawatangazi bure hapo,wamelipwa kutumika katika uhamasishaji huu....Ni sawa na wangetumika kutangaza wananchi kununua bidhaa za Coca Cola,Pepsi,TBL,SBL....AZAM n.k........wenzenu wako kimaslahi zaidi...Ndio matunda ya umaarufu haya,unatumiwa kwa matangazo(kuwahamasisha wananchi kutokana na umaarufu wako) na unalipwa....Ni mbinu inayotumiwa katika nchi nyingi tu duniani,si Tanzania pekee
CCM wajanja na nawasifu kwa njia hii(wamewapiga bao la nguvu wapinani wao).......Vyama vingine vinalala sana,viamke badala ya kuishia kulialia tuuuuuuu kusiko na faida.....Visije vikakumbuka shuka kukiwa kumekucha na jua la asubuhi lishashika nafasi..........
Si ajabu CCM wakawatumia wasanii hawa(kwa malipo0 katika kampeni na kupata ushindi wa kishindo.................Upinzani uamke sasa kabla hakujakucha
Ni hayo tu
Mkuu sikubaliana na wewe hata kidogo labda wewe utakuwa sio mtanzania CCM imeiba hela zetu siku zote EPA na sasa hivi bado wanakula hela zetu inakuwaje leo hii wanaomba tuwachangie wakati hela zetu wambetuibia??? jamani na wewe kuwa muungwana hapa, Hawa wasanii wana njaa na upeo mdogo ndo mana wamewatumia
Mkuu sikubaliana na wewe hata kidogo labda wewe utakuwa sio mtanzania CCM imeiba hela zetu siku zote EPA na sasa hivi bado wanakula hela zetu inakuwaje leo hii wanaomba tuwachangie wakati hela zetu wambetuibia??? jamani na wewe kuwa muungwana hapa, Hawa wasanii wana njaa na upeo mdogo ndo mana wamewatumia
Ngosha et al,
Mosi, hao wasanii kwanza wengi wao hawana viwango, tunawapa airtime , attention, love and affection tu kwa sababu bongo hatuna substitute entertainment kulingana na mifuko yetu iliochoka.
Pili, hakuna mtu anayewalazimisha kuchagua chama tafauti na CCM, sielewi hoja hii mnaitoa wapi.
Tatu, kuhusu elimu yao, tz nzima inajua wanamuziki wengi likimbia umande na kaa walimaliza shule walizungusha, as simple as that. Hiyo ndio bottomline, and thats sounds louder to their thinking capabilities and intelligence quotients. Na mbaya zaidi ukichanganya na njaa na ubinafsi u know what to expect, and thats whats is happening here.
Nne, kuhusu kuchagua vyama vingine thats is not even a question. CCM ndio responsible and guilty party inaowachakaza watz kwa umaskini wa kutupa.
Hahaaaaaaaaaaaa.....Asante....Nshazoea miye.............Ila Bayern bingwa leo......Enjoy the gameNgosha unanifurahisha sana..
Mosi, I agree ndio 'wanamuziki' wetu , binafsi siwakubali, maana sioni kiapji chochote au creativity..na zaidi baada ya kujiattach na oppressing class, the class which administer deprivation and deterioration to static of this country, ndio kabsaa nimewavua nguo and they will never earn my respect, never ever. Thats my personal view.
Pili, vijana wana makosa kwa kuwatosa watz wa kawaida ambao hawana channels za kusikika na kuelezea madhila ya jamii. Kwa ku-join hands na tabaka tawala, damu ya wanyonge ipo juu yao. Sio wao tu na wote wenye kujali ngozi zao tu.
Tatu, elimu inaendana na upeo, ndio maana wahenga walisema elimu ni ufunguo wa maisha. Pasi na elimu uelewa lazima uwe finyu and thats what is happening here.
Nne, what is happening to 'vyama vya upinzani' is independently exclusive na kadhia hii.
Tano, namalizia Bacardi yangu hapa zikiwa zimebakia takriban dakika 14 unusu kwenda kifikra kule Santiago Bernabeu kushuhudia the special one na vijana wake wakichukua kikombe cha mabingwa wa ulaya.
Pole in advance though.