Wasanii na vituo nani alipwe nini?

Wasanii na vituo nani alipwe nini?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,008
Reaction score
16,660
Wasanii wetu wapo kutokana na kubebwa na media, sasa nimesikia kuwa vituo vya redio na television vinavyotaka kucheza kazi za wasanii nchini vitalazimika kuwalipa wasanii kwa kucheza kazi zao hizo kwenye vituo vyao. Kama hii ni kweli basi kiama cha wasanii wa bongo kimekaribia, maana vituo hivi ndivyo vinavyofanya kazi ya kupandisha hadhi kazi mbovu na zisizo na viwango za wasanii wetu nchini. Wasanii wetu wa ndani hawana uwezo wa ku promote kazi zao badala yake wengi wao walikuwa wanavibembeleza vituo vya utangazaji vicheze kazi zao hewani ili wasikilizaji wapate kuzisikia hatimaye waende wakazinunue kazi hizo mbofumbofu. Kwa mtindo huu tujiandae kusikiliza nyimbo za Bob Marley, Michael Jackson, za kihindi, Nigereia, Afrika Kusini na za congo tena kama zamani. Maana hakuna chombo cha habari kitakachokubali kulipa hela kwa msanii ili kupiga kazi zake mbovu, na huo ndio utakaokuwa mwisho wa wasanii wetu wanaofanya sanaa zao kwa bajeti ndogo na bila kuwa na taaluma kuhusu sanaa hizo.
 
Hilo nalo neno mkuu
Jamaa wa media wanaviburi balaa.
 
wote walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea mbaya zaidi wasanii hawazitambui haki zao na wanao jitambua wanakuwa waoga au kuna aina fulani ya ubebwaji yale mambo ya kuhongana ili wimbo uchezwe redioni yatapotea but si mpaka sheria hiyo ianze kufanya kazi maana watanzania kulitamka jambo ni wazuri sana wa mipango ya mdomoni utekelezaji shughuli
 
Back
Top Bottom