Wasanii mnakera sana na majibu yenu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,267
Kwema wanajamvi.!?
-Wasanii wa muziki wa dansi, rhumba, bongo flava ,baadhi yenu kitendo cha kila mkifanya mahojiano na vyombo vya habari kuhusu labda kuimba mlianzia wapi.?

Majibu yanakuwa eti madrasa au kanisani hii haikubaliki kabisa, kwasababu hapo kwanza unakuwa umeifanyia kitu mbaya sana dini yako na unahitaji toba, vilevile tafsiri inakuja kuwa ili msanii aweze kuimba vizuri sauti ya kuvutia na kupata mafanikio basi aanzie kuimba qaswida au kwaya kwanini msitafute namna ya kumjibu huyo mwandishi wa habari vyovyote vile pasi na kutaja madrasa na kanisani?

kwa vile hizo sehemu ni za mafundisho ya ibada kumwelekea muumba,hazifundishi usanii ambapo vipo vyuo vyake.

Achenii..!
 
Mungu pekeake ndiyo anauwezo wa kumuhukumu mwanadamu.

Kama wanakukera usiwasikilize siku zote ukweli hapendwi.
 
Mkuu uzi si umeeleza utafute namna lakn si pande hizo mbili
 
Heeeh ! Nimeishia kucheka tu. Utawezaje kuwa muimbaji mzuri ikiwa hukuwahi kuimba madrasa na kanisani. Labda kama wewe ni Pagani.
 
hahahah unajua mi madrasa nimeimbisha sana qaswida, sasa kuna wale anakuja madrasa kwa mwez mara moja, au anaposkia maulid inakaribia na kwnye qaswida anakua anamung'unya tu afu anasema kaanzia madrasa kha, na mfano ni jamaa mmoja ni staa mkubwa tu nliish nae kitaa, nkashangaa et nae akat anahojiwa alisema kajifunzia kuimba madrasa, kwani Allah anapotoa kipaji cha muziki lazma kipitie kwa ustaadh au mwana kwaya?
 
Hahaaaaa....... hivi ule msemo wa "Sanaa bongo" uliishia wapi?
 
Wengi wao sio kweli ila wanataka jamii iwaone kuwa walianza tangu kitambo na katika maadili ya dini.
 
Back
Top Bottom