Wakuu kabla ya kuwahukumu hawa viumbe tujikumbushe kuwa wasanii ni watu wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii kuliko hata wanasiasa walio wengi. Kwa mfano Diamond peke yake ana ushawishi mkubwa kuliko wanasiasa wote wa nchi hii... kidunia hakuna Rais, mfalme au mtawala yeyote aliyekuwa akimzidi ushawishi hayati Michael Jackson kipindi akiwa hai.
Tawala karibu zote zinajua hilo ndo maana huwa zinawaweka karibu wasanii kwa kuwashawishi au kuwalazimisha kwa sababu kwa ushawishi walio nao ni hatari kuwaacha tu. Wakihamia kambi pinzani ni hatari kubwa. Wasanii wengi wamewahi kujikuta matatizoni kwa kusimama na itikadi tofauti na serikali iliyoko madarakani.
Mfano mrahisi ni majirani DRC zamani wakiitwa Zaire chini ya Dikteta Mobutu. Wasanii walipitia magumu kila walipokuwa wakionyesha misimamo yao inayokinzana na serikali. Hayati Franco aliwahi kukimbia nchi. Koffi Olomide mwaka 97 kama sio 98 aliwahi simamishwa barabarani na kushushwa kisha kucharazwa viboko na askari kama mtoto mdogo. Werrason alishushwa jukwaani akiwa anatumbuiza na kushushiwa kipigo cha mbwa mwizi. Kimsingi ni hatari kwa msanii kuwa na itikadi tofauti na serikali iliyopo madarakani. Hapa Tanzania mifano ipo na mnaijua.
Ninawasihi watanzania wote tusamehe hawa vijana kwa sababu wasingeweza kuepuka kukinywea kikombe walichokinywea.