Wasanii hawa wana vipaji, ila 'wanazingua'

Kuna kitu hua najiuliza kila siku kwanini watu wenye vipaji bongo hua wanajisahau na kuishia kubaya mfano,
chid benz- jamaa alikua anaweza sana na hutochoka kumsikiliza, ila sasa kila mtu anajua yuko wapi.

Tid mnyama- ni miongoni mwa legends wachache waliofanikiwa kudumu hadi leo lakini ngada inaelekea kumpoteza.

Q-chilla- jamaa alikua fundi sana na ile sauti yake lakini nilisikia ngada ilimpoteza.

Ngwea- kila mtu anajua habari yake.

Hiyo ni mifano michache tu nawewe waweza kuongezea!

TID mtoe hapo...mbahatishaji huyu, ameisha hata afanyeje kwa sasa
 
1.Belle 9 dogo anajua bt anabaniwa
2.Nuluel anajua sana bt sijui tatizo nini
3.Hard Mad ni fundi lkn daa kimya..
 
Hao uliowataja hapo ngada imewaharibu..licha ya hivyo wasanii wetu wanaridhika mapema na kidogo wanachopata,starehe nyingi na kuiga maisha ya mbele.wenzao wanatumia madawa pure sio kama hayo makapi wanayotumia wao,wenzao wanapiga misosi fresh na wanafanya checkup za mara kwa mara
 
Hao uliowataja hapo ngada imewaharibu..licha ya hivyo wasanii wetu wanaridhika mapema na kidogo wanachopata,starehe nyingi na kuiga maisha ya mbele.wenzao wanatumia madawa pure sio kama hayo makapi wanayotumia wao,wenzao wanapiga misosi fresh na wanafanya checkup za mara kwa mara

'umarekani mwingi'
 
Unahitaji zaidi ya kipaji kwenda mbele...na sijui ni kwa nini wengi huwa mnakimbilia hii dhana ya "kubaniwa".

Nini maana ya kubaniwa, na kwa nini hao "wabanaji" wakuchague wewe/nyie na sio hao wengine ?..labda kuna uwezekano mkubwa kuwa unadhani tu kuwa una kipaji ili hali sio kweli kuwa unacho hicho kipaji...na ndio maana unaishia kuungwa mkono na mashabiki wachache wanaodhani kama wewe...au pamoja na kipaji ulicho nacho unakosa ziada inayohitajika na mashabiki ili waendelee kukkunga mkono.

Mwisho wa siku muamuzi wa mwisho wa ubora wako ni mashabiki na sio "wabaniaji"...na kama unabaniwa na mashabiki basi ni dhahiri kuwa unapaswa kutafuta shughuli nyingine.

Ni akili gani kwa mwenye kipaji cha kupika maandazi kushinda kwenye geti la kempisky kung'ang'aniza apewe kazi ya upishi...na akikosa hiyo kazi anaishia kulalamika kuwa ana kipaji lakini anabaniwa...pamoja na kipaji chako labda Hoteli inahitaji zaidi ya hicho kipaji...na huna hiyo ziada...na kwa nini usitumie hicho kipaji chako kuhakikisha tu wale jirani zako wa Mburahati hawajahesabu siku bila kula maandazi yako ?

Kwa watanzania zaidi ya milioni moja kutambua uwepo wako ni hatua moja, na ungepaswa kumshukuru Mungu kwa hilo...yaliyobaki ni juu yako wewe kujiongeza ni nini cha kufanya uende mbele, kumbuka bado kuna maelfu ya watanzania wana vipaji na wengine hata zaidi yako na wangetamani kuipata walau fursa ya kutambuliwa uwepo wao na japo Watanzania laki mbili tu ili waende mbele.

.......INAHITAJI ZAIDI YA KIPAJI KWENDA MBELE.......
 
Q chief moja ya wasanii wakali lakini hana nidhamu na kazi yake napenda sana mziki wake lakini nasikitika hana mafanikio yanaendana na kipaji chake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom