Wasanii 5 Wa Tanzania Wenye Pesa

nadhani kwa kumtia urefu si kilema katika list bora heading ingesomeka 'wasanii (na WANAMICHEZO )wa 5 Tanzania wenye pesa(WANAOONGOZA KWA PESA)'
 
Hii list ni kwa mujibu wa chanzo gani? Mtu pekee kati ya hao unayeweza kupata kipato chake na faida baada ya makato mbalimbali ya kodi ni Hashim tu, hao wengine ni urongo mtupu na hakukna data zozote zinazoweza kuthibitisha vipato vyao!!!! Sijaona "maprodyuza" walioanza kujikusanyia ngawira toka hao uliowabandika hapo hawajaacha kunyonya maziwa ya mama! Na unapoongelea "wasanii" haimaanishi waigizaji na waimbaji tu, kuna watu wengi umewasahau au hauwajui kabisaa!
Hata mimi najishangaa jina langu halipo kwenye hiyo list
 
Kwani Hasheem anamzidi JK mkwanja? Mbona hamjamuweka JK kwenye nafasi yake. Kama hana ya kwanza basi mpeni hata ya pili msanii wetu wa kizazi kipya Jakaya Kikwete! Kazi zake za kiusanii kila mmoja wenu anazijua, ila kama huzijui ni ruhusa kuuuliza...........
 
ana single ipi kwani! au kwa heshima yake juu ya anavyoisaidia hiyo industry!
 
alaaa kumbe, ndiyo maana naona hawa vijana wanawachezea mabinti kwa jinsi watakavyo
 
Hashim sio msanii,ni mwanamichezo unatakiwa umuweke kwenye orodha ya wanamichezo tajiri tanzania apambane na kina mbwana samata,henry joseph,mrisho ngasa,kina juma kaseja etc,mwanadada jide ndio msanii wa kizazi kipya ukiongea kwa mbali tunakuckiliza anaweza waongoza wenzie kuwa na band,studio,mgahawa,maji yake mwenyewe kibongobongo sio kitu kidogo

yaan apambane na wakina ngasa wanaopokea mil.moko kwa mwez?
 
full of guess work....inasemekana, inakadiriwa etc.....

nionyeshe balance sheet ya japo mmoja wa hao watu kisha tukae na kujadili au laa nionyeshe tax returns za watu hao then tutaweza ku-deduce their taxable profits na mwisho their cash flows...

by the way kwa vile source yako ni Emelda na Bab kubwa yake....sikulaumu bali nashauri uwe a bit objective...nenda hatua moja mbele, usiishie copy and paste kama ulivyotufanyia hapa....changanua kama alichoandika Emelda kinajitosheleza na kinaweza kujisimamia na kujitetea kama ukweli usio na shaka.

asante kwa taarifa anyway.
 
Linamilikiwa na Binti moja makini sana anaitwa EMELDA. Sifahamu mengi sana juu yake ila najua she is good na ni mfano wa kuigwa.

Kuna something good coming from huyu binti. Atakuwa na TV shows yake itakayoitwa "The Emelda Show" Hii itakuwa ni show ambayo mlengo wake ni kuwa- inspire na to encourage pamoja na kuwasaidia watu kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha, so they can have hopes. Walengwa zaidi wa show hii kwa asilimia 80% itawahusu wanawake wenye umri kati ya miaka kati ya 18-35.

So far Emelda bado yupo location na ana-shoot na kampuni ya GRM Production na pia yupo katika mazungumzo na vituo tofauti vya TV. So anytime soon show itaanza katika TV.

Haaaa haaa leo natumia Kiswanglish cha mjini. Ndo lugha ya Wasanii hiyo, au vipi bana, au siyo mchizi wangu!

Emelda ni mmiliki wa Bang! Magazine sio Bab Kubwa Magazine naomba kumrekebisha mwana jamvi
 
Takwimu nzuri sana ila nimeguswa na kufurahishwa kwa mafanikio ya Hasheem maana hua tunaona movie na kusoma story mbali mbali za watu waliokua wakidharaulika katika jamii na baadae kuja kuheshimika katika kiwango kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom