Allien
JF-Expert Member
- Jul 6, 2008
- 5,546
- 1,861
- Thread starter
- #81
Sidhani kama Bab kubwa Magazine linamilikiwa na Emelda. Bali linamilikiwa na Clouds Media Group,na Emelda ninachofahamu anaendesha jarida la 'Bang'.
Ila sidhani kama kuna uhalisia wa asilimia 100 kuhusu hao top 5 kutengeneza mkwanja wa namna hiyo. Pengine wameandika hivyo ili kuuza jarida lao. Na hata tukimchambua msanii mmoja mmoja.
1. Hasheem Thabeet- Jamaa sio msanii bali ni mwanamichezo na hata hicho kipato chake ambacho wameandika kwamba alitengeneza mwaka jana,nadhani ni kwa upande wa mshahara tu na hapo bado ujaondoa makato mbalimbali ikiwemo kodi.
2. Lady Jaydee na Prof Jay-sidhani kama vyanzo vyao vya mapato viko wazi kiasi hicho.
3. Ray na Kanumba-Hawa inaonekana kama wanatengeneza fedha nyingi sana kupitia movies,ila sidhani kama kuna ukweli kwa 1oo% kusema wametengeneza pesa kiasi hicho.
Note: Sijampinga msanii au yeyote aliyepo katika orodha hiyo,ila sitaki kuamini kuwa hiyo habari ina ukweli kiasi cha hata asilimia 40.
Noted with Thanks.
Umiliki - Noted.
Uhalisia - Obvious. Nchi yetu haina mfumo wa kuweza kupata accurate data. Ndo maana hadi leo hatuna list ya Riches. Wewe ukisema ni Mengi, au Rostam, mimi nitasema ni Mzee Sabodo au lowassa nk
Hasheem Thabeet - Agreed. Si Msanii. Ila wote hawa wako katika Enterteinment Industry.
Lady JD na Prof - Share nasi unachojua maana mambo haya huwa yanaandikwa hata magazetini. Na pia fans wanaona assets walizonazo.
Ray na Kanumba - Share na sisi kilicho cha ukweli.
Respect.