Taarifa za hivi punde kutoka Chalinze ni kuwa kikundi maarufu cha Taarab cha Five Stars kimepata ajali mbaya maeneo ya Chalinze na kisababisha vifo vya takribani robo tatu ya wanamuziki wote.
Ajali hii imetokea usiku huu. Idadi kamili ya waliokufa ama kujeruhiwa haijawekwa wazi kinagaubaga. Tunaendelea kufuatilia.
Pia haijajulikana walikuwa wanatokea wapi, ila inaaminika walikwa wanarudi jijini Dar baada ya Show ya weekend katika mikoa ya jirani.
Pole kwa ndugu, jamaa, marafiki wa marehemu na majeruhuu, pia na wadau wote wa muziki wa taarabu.
Kuna taarifa zisizo rasmi kwamba kundi la taarabu la five star wamepata ajali mbaya ya gari maeneno ya kibaha na robo tatu ya wanamuziki wamepoteza maisha.
Kama kuna mtu alipita maeneo hayo au kuwa na taarifa rasmi tunaomba atujuze.
Hapo hakuna siasa ila ukweli ni kuwa serikali inayo simamia miundo mbinu ndiyo inapaswa kubeba lawama zote kwani ajali Tz ni nyingi sana na zinasababishwa na miundombinu mibaya
Nini wa taarabu, roho za watanzania wasiojuilikana zinatoka hakuna anayeleta ufukunyuku hapa, ila hawa waimba taarabu na wauza sura ndiyo mtulazimishe tupay attention kuangalia na kusikiliza. Its not fair, kila mtu ana haki ya kujadili anachojisikia.
Ni kweli ila watu wanaleta utani kwenye issue za msingi, inasikitisha sana, Mwenyezi Mungu na mwingi wa Rehema azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amen!
Hawa clouds, yaan badala ya kuweka habari za msingi kuhusu huo msiba, wao wanaleta malumbano ya kimapenzi kati ya diamondi ,diva na wema sepetu, Usupa star kazi kwelikweli,,,
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.