WASALITI WA KISIASA 2016

Meropenem

Member
Dec 14, 2016
23
14
Za mchana wana jukwaa.Leo nimeona niwaletee list ya wanasiasa ambao kwa namna moja au nyingine wamesaliti vyama na watu wanaowaongoza.

1.Freeman Mbowe
Huyu ni kati ya wanasiasa wanaofanya siasa biashara bila kujali jamii itamchukuliaje na madhara ya usaliti wake kwa anaowaongoza.Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 Chadema iliaminika kama chamba chenye msimamo usiolega linapokuja swala la kupinga ufisadi.Maamuzi ya Huyu bwana pamoja na washauri wake yamefanya msimamo wa chama juu ya ufisadi kulega na kuonekana chama kisicho na msimamo wa moja kwa moja yanapokuja maswala ya ufisadi

2.Edward Lowasa
Anaaminika kama mwanasiasa anaependwa kuliko yeyote kwa nyakati hizi.Tukisema kila mwanasiasa avuliwe chama tuwapambanishe huyu ataibuka champion.Kabla ya mbio za kumteua JPM kama mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM jina la EL ndio lilikua neno linalotamkwa kuliko mtu yeyote ndani na nje ya chama chake ila kilichotokea wote tuliona.Baada ya pale kama mwanasiasa aliyekua na anaeamini kwenye sera za Ccm alitakiwa kukubaliana na hali na kuungana na JPM kujenga chama upya.Kuonyesha kwamba nae ni mfanya siasa za kushinda lazima akasaliti aliyoyaamini kwa zaidi ya miaka 30 na kuingia Chadema.

3.Moses Machali
Moja ya wanasiasa vijana na machachari katika kujenga na kusimamia hoja zao.Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 NCCR MAGEUZI ilikua na tumaini la kudhinda baadhi ya majimbo hasa jimbo la huyu jamaa ila jamaa kwa maamuz sijui yanatoka wapi akasaliti alichokiamini na kuingia Act the rest is history.Yeye kapoteza na chama kimepoteza
 
Kuna wengine wakiandikwa unakikuta umepotea.Ngoja nipite.
 
haha mi napendaga jinsi wanavyowawaza mbowe na lowasa kila siku hii inanipa faraja wanawaogopa to death
 
Back
Top Bottom