Wasaidizi wa Rais Magufuli tafadhali jitahidini kumweleza kipi cha kusema na cha kutokisema kwani anajichanganya mno!

Anachoka kwa lipi hasa?
Kwani natembezwa kwa miguu huko mikoani,mtu anasafiria V8 new model full kiyoyozi % mvinyo, shampen,kuku vipo ndan,choo kipo gari ya nyuma,hafungi vifungo vya shati wala kubrashi viatu,kila kitu anafanyiwa, analala hotel hadhi ya 5*s ..Hata tarifa za kiingereza zilishatafsiriwa na kibudi tena amewekewa kwenye audio yy anasikiliza tu na kumeza, hachapii wala haandai hotuba kila kitu anandaliwa yy kusoma tu,afu mnatudanganya anachoka kwa ziara nyingi. Zile ni ziara au anafanya utalii wa ndani bila malipo kwa mgogo wa ziara, anapoteza tu pesa za walipa kodi sijawahi ona jipya kwenye ziara zaidi ya kukifanyia chama chake kampeni.
 
Kama kuna Kitu ambacho hadi leo kinanisikitisha ni tabia ya Wasaidizi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli hasa Kitengo chake cha Mawasiliano na Propaganda Kutomsimamia vyema Bosi wao kiasi kwamba kuna muda huwa anasema Kauli ambazo Kimsingi huwa ‘ zinamfunga ‘ kama siyo hata ‘ kumhusu ‘ Yeye Mwenyewe kisha anabaki tu kutupa taabu wana CCM katika Kumtetea au Kuzijibu Hoja kutoka kwa ‘ Wakosoaji ‘ wake hasa hasa ( Wapinzani ) ambao kwa bahati mbaya wengi Wao ‘ wamebarikiwa ‘ sana Uwezo mkubwa wa Akili / Kufikiri.

Nina mifano mingi ya tabia yake ya ‘ Kukengeuka ‘ Kimawasiliano ila hii aliyoitoa leo ama hakika imenishtua na kunishangaza mno hadi nawaza labda alijisahau tu au pengine hapati muda mrefu wa Kupumzika na badala yake analazimisha kufanya Kazi kisha anajichosha hadi anachosha pia na Akili zake hasa upande wake wa Kumbukumbu.

Hivi unapowasema Mawakala wa Barabara nchini ( TANIRODI ) kuwa ‘ wanafuja ‘ Pesa za Serikali na kwamba sijui ndani ya Miaka Kumi ( 10 ) wanapanga / wanakodi tu Majengo huku unajua kabisa kuwa Wewe Wewe ambaye leo hii ‘ unawachamba ‘ hivyo ndani ya miaka Mitano ( 5 ) kati ya hiyo Kumi ( 10 ) ulikuwa ndiyo Bosi Wao Mkuu wa Kiserikali ( Waziri ) husika hapa unataka Watanzania tukueleweje labda au unataka Kutuaminisha nini?

Ombi langu Kwenu Wasaidizi wa Mheshimiwa Rais hebu jitahidi muwe mnamuandikia Hotuba zake zote na muwe mnamlazimisha awe anazisoma hizo hizo na siyo awe ‘ anabwatuka ‘ tu kutoka Kichwani kwani huwa anakuwa anatoa ‘ Maboko / Makosa ‘ mengi ambayo huwa yanamfanya aonekane ‘ Kituko ‘ na hata ‘ Kudharaulika ‘ na wenye Akili ambao kwa bahati mbaya ni wengi nchini Tanzania pengine kuliko hata hao wanaomzunguka 24/7 hapo Ikulu / Serikalini.

Halafu siyo lazima Ziara zote awe anazifanya Yeye tu anaweza zingine akawaachia Wasaidizi wake Kiuongozi akina Mama Samia na Mwalimu Majaliwa ili apunguze mzigo mkubwa wa Kimajukumu unaomkabili. Na si lazima awe anafululiza Kufanya Ziara zake katika Mikoa mingi ndani ya muda mfupi kwani kwa Mtazamo wangu nahisi kuwa Ratiba zake nyingi pia huchangia ‘ Kumchosha ‘ na hatimaye hata katika Hotuba zake nyingi huwa ‘ anaharibu ‘ kwa kutoa hayo ‘ Maboko ‘ yake huku pia akiwa anayarudia maneno yale yale tu hali ambayo huwa ‘ inawaboa ‘ pia wanaomsikiliza.

Mlio nae karibu lifanyieni Kazi hili tafadhalini kwani Rais Dkt. Magufuli binafsi namkubali kupita Maelezo hasa kwa ‘ Utendaji ‘ wake uliojaa ‘ Uthubutu ‘ mwingi na pia ni Kiongozi ambaye anaonyesha ana ‘ Uchungu ‘ sana na Maendeleo ya Watanzania na Tanzania kama nchi ila nahisi ama Wasaidizi wake wanamuogopa au Yeye mwenyewe nae ni ‘ Mbishi ‘ hali inayopelekea hao Wasaidizi wake ‘ Kumpigisha Shoti ‘ kwa Makusudi ili akosee na aonekane hana jipya na hafai.

Kwa leo langu ni hili tu Kwenu.
Sidhani kama ni rahisi hivyo kumshauri kichaa akakusikiliza, akakuelewa na kukubalia
 
Yaani wew umepata wapi uwezo na ujasiri wa kuweza kumshauri kiongozi wa Malaika mbinguni???
 
Back
Top Bottom