Wasaidizi wa Pengo waanza kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasaidizi wa Pengo waanza kazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Kanisa laaswa kuombea uchaguzi  [​IMG]
  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Polycarp Kardinali Pengo, akiwavisha kofia Maaskofu wapya baada ya kuwasimika jijini Dar es Salaam. Maaskofu hao, Salutarius Libena (kulia) na Eusebius Nzigilwa, wanakuwa wasaidizi wa Askofu Kardinali Pengo katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam.  Serikali imeliomba Kanisa Katoliki kuliombea taifa wakati wa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba, mwaka huu ili wananchi waweze kuchagua viongozi waadilifu, wema na wanaomwogopa Mungu.
  Kadhalika, Serikali imeliomba kanisa hilo mchango wake wa hali na mali ili kuwezesha kufanikisha tukio hilo la kihistoria nchini.
  Ombi hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, alipokuwa akitoa salamu za Serikali wakati wa ibada ya kuwaweka wakfu Maaskofu Wasaidizi wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam.
  Maaskofu waliowekwa wakfu ni Salutarus Libena na Eusebius Nzigilwa ambao watakuwa wasaidizi wa Askofu Mkuu wa jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pengo.
  Marmo ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye ibada hiyo, alisema Serikali inamatumaini makubwa na kanisa hasa kuwajenga wananchi katika maadili mema kiroho na kiimani ili wawe raia wema.
  "Baadaye mwaka huu wananchi wenye sifa watapata fursa ya kuchagua viongozi mbalimbali wa Serikali...tunadhani pia ni jukumu la kanisa na viongozi wake kutoa mchango wa hali na mali kufanikisha tukio hili kubwa," alisema na kuongeza kuwa "Sote tungependa kupata viongozi waadilifu, wema na wanaomwogopa Mungu."
  Aliahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na kanisa katika kuwaletea wananchi maendeleo yaliyokusudiwa.
  Awali, baada ya ibada ya kuwaweka wakfu maaskofu hao, Kadinali Pengo alieleza majukumu yao, alisema Askofu Nzigilwa atashughulikia kurugenzi kadhaa ikiwemo ya Elimu, Fedha, Afya na Karitasi wakati Askofu Libena atashugulikia mawasiliano, Liturijia na vijana.
  Alisema kutokana na mgawanyo huo wa majukumu, yeye (Pengo), pamoja na mambo mengine atasimamia jumuiya za kanisa hilo ikiwemo ya Watoto, Wanaume, Wanawake, Halmashauri ya Walei na Mahakama ya Kanisa hilo ambaye yeye ndiye jaji Mkuu.
  Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wakiroho akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe mama Anna, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. John Magufuli na mkewe, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Stephen Ihema na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Willliam Lukuvi.
  Wengine ni Askofu na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa, Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki nchi nzima, Mwakilishi wa Papa Bedenicto wa XVI, Mapadre, Mashemasi na Watawa wa kanisa hilo.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...