Wasafiri na mabasi/ vyakula vya barabarani kwa afya

Dec 20, 2023
23
26
Habari wanaJf wote,

Story hii inahusu safari yangu kutokea Zanzibar kurudi Moshi, Kilimanjaro.

Ee bana dah nakumbuka ilikuwa ni sa 12 asubuhi makunduchi kwa mwenyeji wangu nikapewa chai ya maziwa na vitumbua kama sita na madonut nikafuta vyote.

Kosa linaanza nilipo sahau kwenda chooni halafu tumbo limejaa najifanya nina haraka, kizaa zaa kinaanzia kwenye boat namna mawimbi yanaenda nkaanza kusikia kama vitu tumboni vinapanda Hadi kooni half vinarudi.

Nikajikaza kiume maana tayari kichefuchefu kilishaanza.
Basi hadi kufika Dar Mida ya saa4 asubuhi nkashuka kwa boti nikakata tiketi ya basi chapu chapu, kwenye basi nikabahatika kukaa na classmate wangu wa o-level anaitwa Mgure ee bana we ilo ni kosa la pili, huyu Mgure ni mlaji sana anaweza kufuta kindoo Cha makande mwenyewe

Kumbe Mgure alikuwa hajaacha tabia ya kula kula alikuwa amefungasha rojo la nyama, chipsi, ndizi za kukaanga na kachumbari kwenye mfuko limejaa vizuri kabisa, hadi nasikia kulia yaani safari ilivyoanza tuh tunaitafuta njia kuu Mgure akasema tule maana wote bado tulikuw vijana damu ya moto unajijua huna ela yanini ukatae basi na me nkasema apa ndo pakuhemea Yani duh🥲 ulafi mbaya kwakweli, kwanza chips zilikuwa zishapoa ametengeneza mwenyewe usiku nkajiachia kiroho safi tukaanza kula Hadi abiria wengine wanatushangaa sema ujana maji ya moto hatujali nkapiga ivo ivo nkamaliza, nlivyofika korogwe mjini nkapiga na juisi yake kwenye kopo duhh.

Ee bana dah kizaa zaa tena kikaanza nilivyofika makuyuni tumbo linaniuma, mbaya nikafungua mkanda jasho la atari Mgure yeye Yuko freshi tuh ananishangaa mbona nahangaika nikaanza kusikia kwenye boksa kama kitu kinapiga hodi nikajikaza tena likapoa.

Tulivyofik Mombo Mgure akanunua paka la mbuzi dah kweeli tamaa mbaya nikasahau jinsi nlivyokuwa nahangaika na tumbo nikajiunga nae tukala na mimi nkajitolea kununua wali maharage Ili asije akaona nakula tu mali zake.

Dah nlishiba hadi nkajisikia vibaya kwakuwa nlikuwa na utoto akilini nikasema sipunguzi mzigo wala nini hivyo sikwenda vile vyoo vya pale mombo.

Picha kamili linaanza tu baada ya gari kuwashwa Moshi wa matajiri ukanipiga nikaanza kusikia kichefuchefu mara tumbo kama linacheza mara tena nasikia kitu kinagonga hodi kufika maeneo ya chekelei nkamwambia konda asimamishe niende kwenye mapori akakataa akasema gari inasimama kwenye vituo tu.

Hapo hata kukaa siwezi nimelala kwenye floor ya basi watu wanadhani me kichaa kumbe Hali sio Hali dah watu wakaanza kusema konda anisaidie duh ye mgure Yuko fiti tuh ananishangaa.

Gari likasimamishwa sikutaka kujua Cha kubeba maji wala nini nikaingia kwenye katani nikaharisha viby mno, watu kwenye basi wakasema nawalia mda nkajikaza mwanaume dk10 zmepita hata mapaja hayana nguvu kiuno kama kimekatika duhh ilikuwa so mchezo na bado apo nasikia kuendelea kuharisha nngeweza kukaa ata wiki nmechuchumaa mana so kitoto ile kumaliza sijui nitawaze na nn nkavua Sweta langu nkavua t-shirt nkachukua vest nkatawaza Kisha nkatupa uko kwenye makatani Narudia zangu kwenye basi watu wote wananiangalia kwa madirisha wanachekacheka tuh dah,nkarudi kwenye basi nkakaa nkapiga maji kwanza mana ata mwili umekauka.

Sijakaa vizuri baada kama ya dk 20 nasikia tena tumbo iloo,eeh bana wee nkaanza kusema dereva paki kwa nguvu akagoma nkalala tena chini mana ndo napata nafuu nkamwambia konda akifika hedaru apaki nipunguze kilo tena ,akakubali nkafurahi nakumbuka mbinu za shule ya msingi kuweka jiwe la moto mfukoni lakini ata io mbinu ilikataa mana hamna ata mawe hahahah .

Ilipofika hedaru nikaingia kwenye mashamba tena nkaanza swala la matikiti kudondoka , hahahah, ilikuwa so kitoto.

Had kufikia Moshi nilimshukuru MUNGU sana maan so kwa moto wa siku io na nilijifunza sana Yan had Leo ikitokea safari nakula bites tuh na soda kwisha.
#safari

Kama Kuna mwenye story yake na yeye anaweza kutushirikisha na sisi tujifunze, asanteni
939779829.jpg
1283437935.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom