Madrid boy
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 895
- 615
Habari zenu wakùu nimatumaini yangu hamjambo.Inavyofahamika katika umoja wa mataifa (UN)kwamba kuna nchi saba tu zinazomiliki silaha za nyuklia nazo ni Marekani,Urusi,China,India,Pakistan Ufaransa,Wingereza.Hizo ndiyo zinaitwa (Nuclear states) nchi kama Iran,Korea kaskazini zinataka zitambulike kama nuclear state lakini umoja wa mataifa umekataa kuzitambua.
Ifahamike bomu kubwa la nyuklia lilowahi kutengezwa na binadamu ni TSAR BOMBA lenye uzito wa 50 megatons za TNT lililotengenzwa na USSR lilofanyiwa majiribio tarehe 30th October 1961 huko kazistan kwenye kisiwa kinachoitwa Nava Zemlin kutoka juu ya ndege.
Baada ya teknologia kubadilika ikawa sio kutegemea ndege ndiyo iangushe kama embe bali Injini za maroketi. zilizokua zinatumika kwenda anga za juu zikawa zinatumika kufungia kwenye makombora hayo kwa maudhui ya kurusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine hasa kipindi cha vita baridi kati ya USSR NA Marekani na washirika wake yani NATO ya enzi hizo.
Hivi sasa USSR imeshakufa Urusi kabakia na washirika wachache kama Chechnia ambayo asilimia 80%ya bajeti ya nchi inatoka kremlin,Serbia,Belarus na mshirika wake mpya india hasa kiuchumi na kijeshi kwa mbali.
Kufuatia tishio la NATO kuwa na kambi za kijeshi kwenye maeneo ya zamani ya USSR na kufanya mzoezi kwenye nchi kama Estonia,Poland nyinginzo na kutokana na mpango wao (Urusi) kutaka kurudia ndoto yao ya kuchimba mafuta yanayopatikana eneo la Artic kufungua njia mpya ya meli kutokea Asia kwenda Ulaya kupitia Juu ya dunia (North pole) kupata upinzani kutoka kwa NATO na Marekani ambayo inampango wa kupeleka mfumo wa(THAAD) nchini Poland ambapo ni jiran na Urusi wenye uwezo wa kutunģua makombora ya nyuklia yakiwa angani kabla hayajafika chini kuleta madhara.
Basi kutokana na hali hiyo Warusi wametengeneza bomu la nyuklia linaloitwa RS-28 SARMATH (Thermonuclear armed ICBM) au SATAN 2 kama wanavyoliita NATO Linauwezo wa kwenda umbali wa 10,000 km au 6200 maili.Bomu hilo linabeba vichwa kumi na Sita vya nyuklia.
Kwa mujibu wa shirika la habari linalomilikiwa na nchi hiyo (Sputnik) Bomu hilo moja likirushwa kwenye nchi kama Ufaransa Linauwezo wa kuiangamiza nchi nzima pia Bomu hilo uwezo wa kuishambulia eneo lenye ukubwa wa jimbo la marekani la Texas.
Inasadikika bomu hili linaweza kutumia dakika 13 kufika London likirushwa kutoka mashariki ya mbali ya Urusi yani katikia visiwa vya Kuril vinavyopatikana Asia karibu na Japan. Kinachofanya bomu hili liwe tofauti na mengine kwanza kubwa kiasi kwamba linafyatuliwa kwenda angani kutokea chini ya ardhi.
Pia bomu hili linakwenda kwa speed kali (supersonic speed) Linauwezo wa kuonekana kwenye rada lakini ukifyatua bomu lakwenda kuliangamiza angani kutoka kwenye (anti misille system ) kama THAAD ya marekani linauwezo wa kukwepa hilo bomu linalotaka kulingamiza na kufika eneo lililokusudiwa.
Mabomu mengi nyuklia kama Korea kaskazini yanatumia mafuta aina (solid fuel) kwa sababu ni rahisi kufyetua na haitumii muda.Lakini hili kutokana na uwezo wake na uzito wameamua kutumia liquid fuel yani mafuta ya kimiminika.
Hilo hapo
Sent using Jamii Forums mobile app