Warioba awapiga 'stop' RC, DC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba awapiga 'stop' RC, DC

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Aug 15, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]

  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amewapiga marufuku viongozi wa serikali kuhudhuria katika mikutano ya wananchi ya kukusanya maoni ya katiba.
  Jaji Warioba alitangaza zuio hilo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, alipotembelewa ofisini kwake na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), jijini Dar es Salaam jana.
  Alisema maoni yanayokusanywa awamu hii ni ya wananchi, na kwamba ni vyema kuwaachia wakatoa maoni yao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu.


  “Mchakato huu ni shirikishi, kila mtu atapata nafasi ya kutoa maoni yake, tukimaliza kwa wananchi tutakuja katika kada nyingine, hivyo hakuna haja ya kuwaingilia wananchi, waachwe watoe maoni yao wenyewe,” alisema na kuongeza:  “Tukimaliza kwa wananchi tutakuja katika kada nyingine, kama vile wanaharakati, walimu, wakulima na nyingine zote.”  Aliotakiwa kufafanua viongozi hao ni kama kina nani alisema ni wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa kwa kuwa kama watakuwa kwenye mikutano ya wananchi, kuna uwezekano wa wananchi kutokuwa huru kutoa maoni yao kwa

  sababu viongozi hao kuwako.  "Mwananchi wa kawaida ambaye anakwenda kutoa maoni yake ya Katiba mpya kama akimkuta kiongozi wake kama Mkuu wa Mkoa au Wilaya ataogopa kusema," alisema.  Alisema kuwa wananchi wanawaheshimu viongozi wao, kwa hiyo uwepo wao katika mikutano yao unaweza kukwaza uhuru wa utoaji wa maoni.  Alisema jumla ya watu 27,000 walipata nafasi ya kutoa maoni yao katika
  awamu ya kwanza, na kwamba zoezi la ukusanyaji wa maoni kwa upande wa wananchi linatarajiwa kumalizika Novemba mwaka huu.  Aliongeza kwamba katika zoezi la ukusanyaji wa maoni, hakuna uchakachuaji wala kutishiwa kama inavyodaiwa, kwa sababu kila mtu anapewa nafasi ya kutoa maoni yake.  “Hatutaki dalili zozote ambazo zitakuwa zinaonyesha kutishia wananchi kutoa maoni yao, wala sisi hatuwatishii, isipokuwa nia yetu ni kuwafanya wananchi wawe huru kutoa maoni,” alisema na kuongeza:  “Tunakubali maoni yoyote yanayohusiana na katiba, hata yale yanayotolewa katika mitandao au yanayotolewa kupitia vyombo vya habari yote tunayakusanya.”  Alisema katika awamu hiyo wanatarajia kuongeza idadi kubwa zaidi ya wananchi katika mchakato huo wa kupata maoni ya katiba.
  CHANZO: NIPASHE


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Vizuri sana... Wengine wanajifanya ni Marais wa Mikoa kama yule wa MWANZA na wa ARUSHA; Wa Mwanza anaingilia

  kila kitu hadi Masuala ya Madiwani Wilayani; Kuingilia polisi kuweka wapinzani Jela... na ni Engineer by Profession; Wakati

  Meli Mbovu zilikuwa zinabeba Mizigo Baharini zimeletwa kwenye Ziwa zinabeba Abiria anachekelea... Vitu vya profession

  yake anavikimbia, vitu ya UDAKU ndio vyake...
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  tUNA IMANI SANA na Warioba na Salimu maana nyie ndiyo hazina iliyobaki iliyohifadhiwa na nyerere, hata mwalimu huko aliko anafurahi kwamba utungaji wa katiba umeangukia mikononi mwa watu sahihi, hata kama ni wachafu lakini ni udhaifu wa kibinadamu tofauti na manyang'au kama mkapa, JK na wengine waliomgeuka mwalimu.Safi sana mzee sinde,2015 lazima kitu chenye rangi ya kijani alama ya jembe na nyundo kirudi kijijini
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu wala sio maengineer unamkumbuka yule bibi anayejiita Eng Stella Manyanya kumbe ni Fundi Mchudo baada ya CV yake kumwagwa hapa jamvini
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Gravitas ya kuweza kusema kama hili imebaki kwa wachache sana bongo.

  Asante baba.
   
Loading...