Tujenge utamaduni wa kupongeza jitihada zao wakiwa hai ili wafanye vizuri zaidi

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,147
7,721
Tumekuwa na utamaduni wa kuwapongeza na kuwasifia wakiwa wametutoka ila wakiwa hai kazi yetu ni kukosoa tu na kuwabeza!! Ila wakifa hata mkosoaji mkuu anageuka kuwa fundi wa kusifia na kupongeza, tuache hiyo tabia.

Awamu hii ya 6 chini ya Mama wa Taifa letu Dkt. Samia kaituluza nchi, nchi imekuwa na utengamano, wanasiasa wazunguka huko na kule, huku wakipata ulinzi wa Askari kumbe inawezekana! Asante sana Mama.

Kumbe inawezekana kufuata utawala wa kisheria, sasa hakuna kamatakata wala utekaji!!! ahsante sana Mama.

Kumbe inawezekana kukusanya kodi bila kutishiana au kutumia ubabe. Sasa wafanyabiashara raha mustarehe. Ahsante sana mama.

Kumbe inawezekana kutoa maoni yako bila kubughudhiwa wala kutishiwa. Wananchi sasa wapo huru kukosoa na kutoa maoni yao bila kuhofia chochote. Ahsante sana Mama.

Kwa sasa Nchi yetu imekuwa na mahusiano mazuri na Mataifa mengi na pia tunatambulika na kuheshimika kimataifa. Ahsante sana Mama kwa kutuheshimisha.

Tunakuombea kwa Mungu akupe nguvu na maarifa zaidi utuongoze hadi 2030.
 
Kwanza nimshukuru mama Samia Kwa kuamkia salama Hakika mama anapiga mwingi.

Tukirudi kwenye mada wanaccm inawezekana Wana ubongo wa kwao peke yao, Kwa sababu akili zao zingekuwa ni Bluetooth zisingeweza kupair na device nyingine.
 
kuna mstari mdogo sana kati ya utamaduni wa kupongeza na kizazi cha machawa
 
Tumekuwa na utamaduni wa kuwapongeza na kuwasifia wakiwa wametutoka ila wakiwa hai kazi yetu ni kukosoa tu na kuwabeza!! Ila wakifa hata mkosoaji mkuu anageuka kuwa fundi wa kusifia na kupongeza, tuache hiyo tabia.

Awamu hii ya 6 chini ya Mama wa Taifa letu Dkt. Samia kaituluza nchi, nchi imekuwa na utengamano, wanasiasa wazunguka huko na kule, huku wakipata ulinzi wa Askari kumbe inawezekana! Asante sana Mama.

Kumbe inawezekana kufuata utawala wa kisheria, sasa hakuna kamatakata wala utekaji!!! ahsante sana Mama.

Kumbe inawezekana kukusanya kodi bila kutishiana au kutumia ubabe. Sasa wafanyabiashara raha mustarehe. Ahsante sana mama.

Kumbe inawezekana kutoa maoni yako bila kubughudhiwa wala kutishiwa. Wananchi sasa wapo huru kukosoa na kutoa maoni yao bila kuhofia chochote. Ahsante sana Mama.

Kwa sasa Nchi yetu imekuwa na mahusiano mazuri na Mataifa mengi na pia tunatambulika na kuheshimika kimataifa. Ahsante sana Mama kwa kutuheshimisha.

Tunakuombea kwa Mungu akupe nguvu na maarifa zaidi utuongoze hadi 2030.
"Ahsante sana Mama kwa kutuheshimisha.

Tunakuombea kwa Mungu akupe nguvu na maarifa zaidi utuongoze hadi 2030", haya tu uliyomalizia kwenye insha yako yangetosha.
 
Back
Top Bottom